Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Sunday, May 22, 2016

Amen

Haleluyah

USHUHUDA: Naitwa Jacqueline Joseph ninamshukuru Mungu kwa matendo yake makubwa kwangu. Nimekaa bila kupata mtoto katika ndoa yangu kwa muda wa miaka tisa (9) Mungu amenitendea mambo ya ajabu kwa kuwa nilitukanywa sana kwa muda wa miaka yote hiyo, na siku moja Mtumishi wa Mungu alikuja Bukoba wakati wa ufunguzi wa kanisa na siku hiyo nilikuwepo katika hiyo ibada iliyofanyika mwezi wa sita mwaka jana. Na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii akiwa ndiye anayeongoza hiyo ibada mara akaniita mbele nami nilipomkaribia akasema nyoosha mkono wako ushike mkono wangu, lakini alipokuwa anasema vile mimi katika ile mikono yake niliona Damu tu inatililika na yeye alizidi kusema gusa huu mkono, nilipougusa akasema Efatha, Efatha , Efatha mara tatu Mungu akanifungua na leo Mungu amenifuta machozi ninawatoto watatu mapacha ambao wote watamtumikia Mungu pamoja nasi wazazi wao. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu muweza wa yote.

Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira: Zaburi 34: 1-9" Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. Katika Bwana nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja..." Daudi anasisitiza kumwabudu MUNGU kwakuwa yeye anaondoa hofu na kukufanya uwe huru mbali na taabu. Unapokuwa mtakatifu yeye huondoa uitaji na ufukara. Ndege wa angani wanakula na kulisha watoto wao, maua ya kondeni yanavaa je nyie sio zaidi? Tatizo watakatifu wa Mungu tunaviburi.

Saturday, May 21, 2016

IBADA YA MFUNGO WA MWEZI WA TANO SIKU YA KUMI NA SITA IBADA YA MAOMBI

MAOMBI:
1.    Bwana Yesu wewe ni kiongozi na Bwana wetu wewe ni Mfalme wetu nipe kutumia Heshima yako katika kuenenda kwangu mbele zako, ili kushinda kila aina ya kikwazo cha adui shetani na mawakala wake.

2.    Bwana Yesu nipe kushinda kwa ajili ya Ufalme wako, nikitumia kweli yako, upendo wako na Imani niliyonayo kwa BWANA MUNGU wetu. Mathayo 5:1-48.

3.    Bwana Yesu kwa neema yako nataka nikae hemani mwako, chini ya mbawa zako, nifurahie uwepo wako daima siku zote za maisha yangu uliyonipa siku za uhai wangu.


Naibariki Jumamosi yangu..............Jumamosi yangu INANG'AA, Vyote Nilivyonavyo Vimebarikiwa na VINANG'AA, Mimi NINANG'AA, USHINDI ni WANGU, Hakuna cha KUNIZUIA, NIMEBARIKIWA.

You can get us live from www.mixlr.com/efatha-ministry

Kipindi cha sifa kwa Mungu wetu! wema wako tumeuona Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Praise God Man,Woman of God its another Day God has given unto us,The 21st day of this month of praying and fasting,Join us this hour as we continue with prayers and Teaching from Man Of God Josephat Elias Mwingira!