SOMO: MASKINI WA ROHO

MCHUNGAJI VICTOR GASPA
Mathayo 5:3, 8 “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. ...8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.”
Maskini wa Roho ni nani? Ni Yule ambaye anatamani kumuona Mungu akigusa maisha yake na anatamani afanye jambo ili Mungu atukuzwe. Huwezi kumuabudu Mungu kama wewe si maskini wa roho. 

Zaburi 42:1-3 “Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako".
Maskini wa roho ni yule mwenye kiu na shauku ya kumuona Mungu katika maisha yake, maskini wa roho siyo yule anayezunguka huku na kule kwenye kila semina anayosikia, huyu ni mzururaji na siyo maskini. 
Maskini wa roho ni yule anaye mng’oja Bwana, hatakama leo hajamtendea anaamini ipo siku atamtendea, ni mtu ambaye anajua kuwa akimng'oja Bwana atapata kile anacho hitaji.
Zaburi 27:14 “Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.”

Comments