PASTOR MICHAEL OLAWORE KUTOKA UK (KATIKA KUSANYIKO KUU 2016) Mungu anatangaza mwisho tangu mwanzo, katikati ya ukame, njaa na hali ngumu isiyofuraisha MUNGU atakubariki. Yesu alikupenda hata akafa msalabani kwa ajili yako, na ni mpango wake yeye kukutoa kwenye huo ukame unaopitia. Katika hali yoyote unayopitia MUNGU hataacha kukupenda kwasababu asili yake ni Upendo na hakuna kinachoweza kumbadilisha. Mpango wa Mungu kwako ni mkubwa sana hata katika hayo maumivu unayopitia atakubariki. Amesema amekuchora kwenye viganja vya mikono yake na anakujua vizuri kiasi kwamba hata idadi ya nywele zako anaijua, na kabla hujaingia katika tumbo la mama yako alikujua. Kama hujui kama MUNGU anakupenda na kukujali ujasiri wa kuomba utapotea.


Comments