NENO JUMAPILI TAR. 16-10-2016 : UTAKATIFU NDIO KUMCHA BWANA



Mathayo 5:21-34 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho. Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.  Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; “
Lazima tujue kama tunasafari. Mambo matakatifu na maisha matakatifu  ndio yatamfanya Mungu ayafurahiye, Mungu hatuta muona bali utamuona, Yule jirani yako  akifurahi na Mungu anafurahi na akichukia jirani yako  Mungu pia anachukia,
Ndio maana  tumeambiwa  tuishi kwa amani na watu wote, mtu akikosea msamehe maana bila kusamehe hakuna amani. Wewe uliye okoka unatakiwa kuumia  kwa ajili ya mwingine ili akoke. Kwa hiyo usimwapize ndugu yako ,  usimuonee hasira ndugu yako, wala usimfyonze.
Maana mwanzo  wa hasira ni ugomvi,   kama hutokua na hasira na ndugu yako huwezi kugombana  nae. Kwa hiyo hata na wewe kama  ndugu yako amekukosea msamehe bure.
Waebrania  12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; “ ukiwa  na amani na watu wote   hutowaza   ugomvi na mtu bali utawaza ukuu wa Mungu  juu yako, kama mtu  akikukwaza    ukimwambia  nimekusamehe bure Mungu atakupa  taji. Makwazo yana anzia rohoni ndipo  yanakuja katika mwili kwa sababu  rohoni  ndipo una waza sana, kwa hiyo  unapo kwazika rohoni unafarakana na Baraka  zako. Shetani  atakuja kwetu  kwasababu   anaona  tuna hasira, chuki na  misonyo, Usimwapize mtu  bali tuonyane kwa upendo.
Efeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; “ Dhambi yeyote unayoiona huku chini ya jua,  haikudondoka  kutoka juu bali ilikuja kwa mawazo, kwa nini  Bwana       Yesu alisema hivyo? kwasababu  rohoni ndio kuna kila  kitu, kama unaona  ukimwangalia  binti  ukamtamani au kuna dhambi inayokusumbua sana weka mkakati wa kuicha maana hakika hutaingia mbinguni.
Kwa hiyo unapozini unafarakana na mbingu  na safari ya  mbinguni inakua haipo tena. Jiwekee mkakati wa kukaa mbali na dhambi, zinaa isikutenge na  safari ya mbinguni. Wadada wengi  wanasema hatuolewi, lakini wengi wana boyfriend na usipokuwa na  boyfriend unaonekanaa mshamba, hivyo hivyo na wavulana. Nikupe siri siku unapoanza kuwa na boyfriend au girlfriend mbinguni   wanakuhesabu  umeoa au umeolewa, sasa uko na boyfriend/girlfriend alafu unamuomba Mungu akupe mume/mke, haiwezekani hata waswahili wanamsemo wa moja havai mbili. Wewe ukiokoka acha mambo ya boyfriend na girlfriend, kaa na Mungu mwambie    najua  mume/mke  mzuri  anatoka kwako.
Ukikaa mahali penye  harufu mbaya   ukazoea  hata wenzako wakikuambia  mbona hapa kuna harufu mbaya wewe utasema  mbona sisikii,  ndivyo na dhambi ilivyo  hata watu wakikuona  una dhambi wewe utajiona uko sawa.
Nataka nikulize swali wewe umeoa na kuolewa alafu unachepuka akili yako iko vizuri?
Imeandikwa mtu akimwacha mke ampe  haki ya talaka  isipokua kwa habari ya uasherati na uzinzi, Kwa hiyo kama   ukimfumania  aina haja  ya kumwacha bali  ni kumsamehe maana  Yesu ana samehe dhambi  zote,  wewe umefanya mangapi kwa  Yesu na  kakusamehe?   hakuna kitu kizuri kama kati ya  wawili mmoja  kujishusha maana ndoa  ina utaratibu. Ni kweli mume  amekosea  lakini sio sababu ya kupandisha  sauti kua ya juu, maana  ata bosi wako akikukalipia  mbona  unanyamaza ndivyo  inavyotakiwa kwa mume wako. Unatakiwa ujifunze kwenye  Biblia jinsi ya kuishi na  wanaume  wenye  hasira. Unatakiwa uende kama Delila japo Samason alimdanganya  lakini hakukasilika  bali aliendelea  kumbembeleza.  Uasherati husisababishe uvunje ndoa bali unatakiwa ujiulize ni wapi umekasea, maana kuna kitu kimekoseka ndiyo maana akachepuka, rekebisha hayo samehe na usonge mbele.
Hatuendi mbunguni kwa  sababu tuna mali, bali tunaenda mbinguni  kwa kushika amri na sheria  zake.
Zaburi 92: 7 “Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;” Mimi  ni mali  ya   Bwana  pia  ni mrithi pamoja na  Kristo,  kila ninapo  endelea  kustawi  ndio wakati mzuri  wa kumwambia  Yesu asante maana wakati huo ndio  unakutana na watu mbali mbali. Roho  mtakatatifu  anapokuletea neno haleti kwa ajiri ya kukudhalilisha  bali anakuletea  ili uweze kurudi katika njia yake.  Hakuna  kosa baya  kama lile ambalo umeolewa alafu ukapata mtoto wa nje ya ndoa kila unapoomba Mungu akusamehe  alafu ukimuona tu yule  mtoto unasikia  sauti inasema huyo mtoto ni  wa nje ya ndoa, huyo ni shetani sasa unatakiwa  umwambie,  sikiliza  shetani  ni kweli huyu mtoto ni wa nje ya ndoa lakini nataka nikuambie  kuwa  Yesu  amenisamehe na  mbinguni  naenda  mimi na mwanangu, maana hata huyu mtoto kuzaliwa na uwezo wa Mungu. Usijihukumu kwa makosa ya huko nyuma bali amini Mungu amekusamehe na usikumbuke, weka nia ya kuishi maisha matakatifu kila siku.

Comments