Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira: Kazi za Roho wa Bwana juu yangu: 1. Kuhubiri injili, 2. Kuponya na kufanya miujiza, 3. Kufungua macho ya vipofu na kuwapa watu mafunuo, Mithali 8:17-20 “Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, .....” 4. Kuwekwa huru, huwezi kupata uhuru kama hujajua kweli na kweli tunaipata kupitia macho yetu, ukishawekwa huru ndipo unaweza kuomba, kama hujakombolewa au hujawekwa huru utakuwa hauabudu bali unalia tu. Ukombozi sio kumtoa mtu pepo bali ni kumwamisha mtu kutoka katika maisha aliyoyazoea. 5. Yuko ili akupe amani. Unapokuwa na vurugu mahali anakupa amani na usipokuwa na huyu Roho utaona vurugu kila mahali hata mtu anafika mahali anasema watu hawanipendi. Roho wa Bwana anapokuja kwa mtu kitu cha kwanza anampa amani.


Comments