MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA (1korintho 12:7-9 “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;”) Safari hii Karama za imani zinaenda kuumbika kwenu, ukipita unatabiri jinsi vitu vyako vitakavyokuwa, Imani ni kitu kingine na ndiyo inayosababisha mambo yawe, yote yanawezekana kwa yeye aaminiye. Ukiwa huna kitu usiombe muujiza omba karama ya Imani iumbike kwako ili ikutoe mahali ulipo na kukufikisha kwenye Utukufu. Mtu uliyeokoka kama huna Imani tafuta mtu akuongoze sala ya toba. Imani inaumba uzima kwa wengine, ukishapata Roho wa Imani kuponya wagonjwa ni rahisi. Ukifanya biashara bila Roho wa Imani utafilisika.


Comments