Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira:
Usipokuwa na Kipawa uwepo wako kwenye familia na kundi lolote unalokuwa unatoweka, lakini ukiwa na KIPAWA usipokuwepo kwenye kikao kikao kinahairishwa. Kuanzia leo kipawa chako kitaonekana. Kipawa chako kinakupa kufikia hitimisho la maisha yako hapa duniani.
-Kipawa kinakuhamisha kwenye ubinadamu na kukufanya kuwa mwana wa MUNGU, ukitembea wachawi wanakimbia. Kipawa kinakufanya kuwa WAKIUNGU.
-Kipawa kinakufanya adui zako kunyenyekea. Kipawa ni muhimu katika maisha yako lakini adui mkubwa ni TABIA YAKO.
-Tabia yoyote isiyompa MUNGU UTUKUFU na HESHIMA itabomoa na kuharibu kipawa chako, na hiyo tabia inajengwa katika maeneo mawili ambayo ni JINSI UNAVYOONGEA NA JINSI UNAVYOTENDA.

Comments