Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Saturday, June 25, 2016

Mchungaji Daudi Urio:
4) Alituchagua ili tuitwe wana.
Efeso 1:5" Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake"
5)Alituchagua ili tuzae matunda na matunda yapate kukaa na kudumu.
Yoana 15:16 "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni"

6)Alituchagua ili tupate msamaha wa dhambi.
Efeso 1:7"Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake"
Mchungaji Daudi Urio:
Kwanini alituchagua?
1) Alituchagua kwasababu tulikuwa mahali pengine.
Zaburi 58:3 "Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo"
2) Alituchagua ili tuwe hivi tulivyo.
Yoana 15:16a"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."
3)Alituchagua ili tuwe marafiki zake.
Yoana 15:15" Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Mchungaji Daudi Urio.
Somo: Nimechaguliwa:
Mimi na wewe tumechaguliwa kuitenda kazi ya MUNGU.
1Wakolosai 13:14" Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; "

Efeso 1:4" Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Ratiba ya ibada Efatha Ministry Mwenge siku ya Jumapili: 
- Ibada ya Kwanza; saa 1:00 - 4:00 Asubuhi.
- Ibada ya Pili; saa 4:00 - 7:00 Mchana.
- Ibada ya Tatu; saa 7:00 - 10:00 Jioni.

Haleluya wana wa MUNGU, ni jumpili ya tarehe 26/6/2016 tunakutanika hapa Efatha Ministry Mwenge na katika vituo vyetu vilivyopo Tanzania nzima na nje ya Tanzania kumfanyia MUNGU wetu ibada. Tunawakaribisha wote, pia mnaweza kufuatilia ibada za siku ya leo kupitia www.mixlr.com/efatha-ministry