Posts

Showing posts from 2016

Naitwa Godluck Massawe: shuhuda1Namshukuru Mungu kwa kuniokoa katika ajali ya pikipili iliyotokea eneo la Ubungo, mimi nikiwa kwenye pikipiki mbele yangu kuna shimo kubwa lililochimbwa na watu wa Dawasco na upande mwingine kulikuwa na gari ambayo ilinifuata baada ya kuona lile shimo. Mwenzangu alinigonga nami niliumia mkono na vidole vitatu vilikuwa vimeumia na kimoja kikawa kinaninginia nilipelekwa Hospitali ya Mwananyamala walinipiga picha ya X-ray wakasema kidole kimevunjika, nikiwa hapo nikasikia sauti ikiniambia nenda kwa Mchungaji wako nilipofika kwa Mchungaji nikakuta kuna ibada ya Cell nami nikaungana nao na baadaye nikamweleza naye akaniambia neno moja unakubali kumtumikia Mungu nikajibu ndio, akaniombea na muda huo mkono ulikuwa umevimba lakini baada ya maombi nikaona maumivu yale makali yameondoka. Kesho yake nikarudi Hospitali na Daktari aliponiangalia mkono na ilepicha ya X- ray niliyopiga ile siku ya ajali ambayo ilikuwa inaonyesha nimevunjika cha kushangaza Daktari alisema sijavunjika wala sina kidonda, tayari YESU alikuwa ameniponya na sasa mkono ni mzima kabisa namtukuza Mungu kwa kuniponya. Siri moja inatupasa kufanya kazi ya Bwana kwa bidii nasi tutakuwa salama.

Image

Jina langu ni NEEMA KALUGULA naishi Holland nina kila sababu ya kumshukuru Mungu, mwaka 2005 nilimtolea Mungu kiwanja cha kujenga kanisa. Mume wangu akataka kuniacha kabisa. Mungu akaniambia usijali watoto wako watasoma Ulaya. Nikapata kazi mahakama ya kimataifa na watoto wangu wamesoma Ulaya na mmoja ameanza kazi. Namshukuru Mungu alichokisema kimetimia. Pia mwanangu alipata ugonjwa wa kuanguka na kuzimia nikatuma maombi PRAYER HOUSE, EFATHA MINISTRYMWENGE wakamuombea na sasa mtoto wangu ni mzima na anaendelea na kazi. Ni mengi amenitendea. NAMSHUKURU BABA MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA NA Wana maombi wa PRAYER HOUSE. MUNGU AWABARIKI SANA NI MIMI NEEMA KALUGULA. Kutoka HOLLAND.

Image

USHUHUDA Naitwa MACKDONALD MAANYA: Natoka eneo la Shalom zone ya Ebenezer, napenda kumshukuru MUNGU kwa yale aliyonitendea, ni mengi sana lakini kubwa kabisa napenda kumtukuza MUNGU kuhusu Ndoa yangu yametokea mambo Mengi na vikwazo vingi lakini nilisimama kwamba jambo hili lazima liwezekane na hatimaye tulifunga Ndoa Takatifu katika Madhabahu ya Efatha na pia Mungu ametujalia mapacha SHONE na SAMWEL. Namshukuru MUNGU kwani Mke wangu ananifanya Nang’ara, ukiona mimi Nang’ara basi ni Mke wangu. Wewe ambaye hujaoa ndoa sio yako ni ya MUNGU wala usione kuwa kufunga Ndoa ni ngumu.

Image

MCHUNGAJI THADAYO MBAZI MSUYA. a10Uzima ni roho wa Mungu kupitia Yesu kristo yohana 1;3-5 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. “ – Ndani ya neno ndimo ulipo uzima – Neno ni pumzi na neno ni roho, – Utajuaje huyu mtu anauzima 1. UPENDO ; kuna NENO ndani yake ili Mungu ajitwalie UTUKUFU na huo uzima uwe ni NURU ambao hawajaokoka lazima uwalete kwa Yesu, hata ukisema kwa lugha ya manabii kama huna upendo ni kazi bure. Kama ukiwa na chuki huwezi kusoma biblia na wala kitabu chochote cha Efatha . Yesu alijitoa ili mimi na wewe tuwe na upendo wa kweli. Mlete mtu kwa Yesu ili upendo wake ukamilike. 2. Unaposikia Neno la Mungu unapaswa kumsoma kwani yeye anapatikana kwenye Neno usiwe mvivu wa kusoma biblia huwezi kuwa na upendo lakini, ukiwa msomaji wa biblia utakuwa na sifa ya kuitwa mfalme na utakua na neema ya kumpenda mwenzako. Tunaye baba anayefichua ya sirini upendo wa Bwana lazima ujue Neno kwanza. 3. Kama huna upendo ndani ya Efatha wewe ni maiti. Unaheri wewe uliye okoka ili uende ukawapatie wengine Neema hiyo ifanyie kazi mtumishi wa Mungu. 4. Ili uweze kumpenda Yesu lazima usome neno asubuhi mchana na jioni, 5. kaa karibu na mtu anaye mpenda Mungu kaa vizuri kwa sababu upo sehemu salama. Mimi ni nani embu kubali kukaa ndani ya Efatha Tulia mbele za Bwana upate upendo wa kweli. Amina

Image

EFATHA MINISTRY MASS CHOIR, wakimtumikia MUNGU katika Ibada ya pili hapa Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania

Image

Mchungaji David Mwakisole: SOMO: ASILI YA BARAKA ZETU NI KATIKA KRISTO YESU: BWANA YESU ni RAFIKI yetu. Mfano:- Ukiwa na rafiki yako unakuwa unampenda na unatamani kumfurahisha mara zote, hivyo kama unatambua kuwa BWANA YESU ni RAFIKI yako unatakiwa UMFURAHISHE, Je utamfurahishaje? • Kwa kutenda sawasawa na maagizo yake kutoka kwa Watumishi wa Mungu, ukiwa unatamani kufanya mambo mazuri kwa ajili yake ndipo anafurahi na kama kunakitu kinakuzuilia ili usifanye vizuri anakiondoa na kukuacha ukiwa huru. • Tamani kufanya mambo mazuri kwa ajili YAKE ili YEYE akufurahie na kufungua yale yaliyofungwa katika maisha yako. Ukikosa kuzingatia kinachotoka katika MADHABAHU ya Mungu dunia itakupelekesha, unapofika hemani mwa BWANA (Kanisani) unatakiwa kutafakari yanayotoka katika MADHABAHU, usiwaze tofauti na NENO linalotoka katika MADHABAHU ya BWANA maana hautapokea chochote na mwisho wa siku utatoka kama ulivyoingia.

Image

Mchungaji David Mwakisole: SOMO: ASILI YA BARAKA ZETU NI KATIKA KRISTO YESU: Ili tuweze kuvuta BARAKA za MUNGU kwetu ni lazima tuwe na kitu cha kumpa MUNGU, tusiende mbele zake mikono mitupu, toa nguvu zako na mali zako, baraka haziji mpaka UMEFANYA KWA BIDII ndipo wale malaika waliotumwa kwako wanapopata nguvu ya kuvuka vizuizi na kukuletea BARAKA zako. Unapokuwa na AMANI ya YESU ndipo unaweza kuzalisha vitu vingi katika maisha yako. Ili shetani akuweze kitu cha kwanza anakuondolea AMANI kwa kukukumbusha yaliyopita. Ni kweli ulikuwa mwizi, mzinzi, mlevi lakini mara baada ya kuokoka YESU alisamehe yote sasa shetani asikukumbushe ya nyuma.

Mchungaji David Mwakisole: SOMO: ASILI YA BARAKA ZETU NI KATIKA KRISTO YESU: Mithali 8:17 " 7 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona". Bidiii ni KUWAZA, KUTAFAKARI NA KUKIRI. Anasema wampendao na kumtafuta kwa bidii watamuona, sio wale wanaosema WANAMPENDA tu ndio watakao muona ni lazima UMTAFUTE KWA BIDII. Ili mwanadamu aonekane anampenda MUNGU kuna kitu cha ziada anatakiwa akifanye, ukisha mpenda MUNGU tafuta cha kujionyesha mbele zake kwa kumtumikia kwa kutoa muda wako kwenda kuwaambia wengine habari za YESU na hapo atajua unampenda, Ili tuonekane tunampenda MUNGU lazima tushiriki yale yanayohusu UFALME WAKE hapa Duniani kama vile kupeleka injili popote Duniani kwa kujenga Makanisa na mengineyo,

Image

Mchungaji David Mwakisole: SOMO: ASILI YA BARAKA ZETU NI KATIKA KRISTO YESU: Waefeso 1:3 " Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; " Baraka maana yake ni nini? Baraka sio fedha tu bali mtu akikwambia umebarikiwa inamaana kuanzia mwilini mpaka Rohoni uwe umebarikiwa. Kubarikiwa ni kuwa na AMANI ya kweli ndani ya moyo wako, unapokuwa na AMANI ndipo unaruhusu mema yanakujia, unapokuwa na UCHUNGU unamfukuza YESU ndani yako. Amani ni ya muhimu sana kwako ndio maana YESU alipokuja akawakuta wanafunzi wake wamejifungia kwa hofu aliwaambia AMANI IWE KWENU, hakuwaambia mimi ndiye YESU, ukiwa na AMANI ndipo YESU anasema na wewe kwa karibu sana. Kwa nini tunatakiwa kuwa na AMANI kwanza? Kukosekana kwa AMANI ndani ya moyo wa mtu ndicho chanzo cha mabaya mengi,

Image

Waimbaji wa Efatha Ministry Mass Choir wakimsifu Mungu. Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam.

Image

Karibuni wote katika ibada za Jumapili ya tarehe 27/11/2016 hapa Efatha Ministry Mwenge Tanzania, ibada ya kwanza inaendelea pia mnaweza kusikiliza ibada za siku ya leo kupitia www.mixlr.com/efatha-ministry . TRENET TV - YouTube Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube. YOUTUBE.COM

SHUHUDA: Naitwa Melania Shao napenda kumshukuru Mungu kwa mambo makubwa aliyonitendea. Niliokoka mwaka 2010 lakini niliingia Efatha mwaka 2011 na mwaka 2012 nilipewa nafasi ya kuwa kiongozi. Nikiwa mjamzito nilijifungua mwanangu akiwa mzima lakini baada ya miaka 3 alibadilika akawa anavimba hadi kushindwa kulana akawa hakuwi, nikampeleka hospitali na baada ya kupimwa na wataalam wakagundua haumwi chochote. Siku moja nilimleta mtu Kanisani kuombewa, Mchungaji Mdadila alipomaliza kumuombea huyo mtu akamuona mwanangu akiwa anacheza akaniuliza yule ni mtoto wa nani? nikamwambia ni wa kwangu akaniambia mbona simuoni mtoto? Nilikuwa napenda sana kumuweka urembo kichwani na kumsuka dreds Mchungaji akamnyoa nywele na kumuombea na mwanangu alipokea uponyaji na alianza kukua kama watoto wengine kwa sababu alipokuwa na miaka 5 alionekana kama mwenye miaka 3. Namshukuru sana Mungu kwa kuweza kumponya mwanangu na sasa ana miaka 10 na amerefuka. Mwaka 2013 nilibeba mimba ya mwanangu wa pili na mimba ikawa ni ya miezi 12 nikaambiwa natakiwa nifanyiwe upasuaji kwa sababu ilikuwa kila nikipimwa inaonekana kuwa mtoto amesimama na alikuwa hageuki. Mimi nilikataa kwa kuwa Baba yetu Mtume na Nabii anatufundisha kuwa watoto wetu wasitokee dirishani bali pale alipo ingilia ndipo atokee. Siku moja kukawa na ibada ya shukurani kanisani na niliombewa niliporudi nyumbani nikaenda hospitali kupima ikawa mtoto wangu amegeuka na wiki iliyofuata nikajifungua salama. Baada ya hapo mwanangu tena akawa hakui na haongei akawa mwembamba sana nikaambiwa nimpeleke India lakini nikawa nahudhuria kwenye maombi na sasa amepona na alianza kuongea akiwa na miaka 3 na sasa ana miaka 5. Namshukuru sana Mungu kwa aliyo nitendea kwani kama siyo yeye wanangu wote wangekuwa hawakui. Mtu wa Mungu usikate tamaa katika jambo unalo pitia amini ipo siku yako kwa Mungu, Mungu anaweza na atakushindia. Unachotakiwa ni wewe kutii na kufanya kile unacho elekezwa na Watumishi wa Mungu Mfano:- kuwaleta watu kwa Yesu yamkini ndiyo ikawa siku yako ya wewe kupokea uponyaji wako.

Image

English Version:TESTIMONY!! My name is Theresia Athanas, from Kilimanjaro KDC, I want to thank the Lord for the great thing that He has done in my life, this week I was called by my daughter who living in Dare s salaam when I was in Moshi, she called in and said that she had been told she had to undergo a cesarean because her child had not turned in the right direction. So I came with her to church here at Efatha Ministry Mwenge Dar and we were able to meet with Pastor Mwakisole who prayed over her and then he said we should go home and wait until she is due and that she will deliver safely. I took his word with faith knowing that it will work, at around 1 o’clock at night she starts experience pain, we rushed her to hospital where the doctors said we had to wait for till morning so that she may undergo operation at the same time she was vomiting and complaining of a lot of pain. I called Pastor Mwakisole again and he prayed for her and he said it will be well. I went outside and feel into an outburst of tears and thanked the lord , when I went back in I found that he has already given birth naturally but her child came out legs first, Pastor Mwakasole called again to know how she was and was happy to know it was all well. I really thank the Lord for delivering my daughter from the hands of death.

Image

USHUHUDA!! USHUHUDA! NAITWA THERESIA ATHANAS MOSHI Natokea Kilimanjaro KDC, wiki iliyopita nilipigiwa simu na mwanangu anayeishi Dar kuwa amepitiliza siku zake za kujifungua na kwamba ameambiwa ajiandae kwa upasuaji (Operation) kwa ajili ya kujifungua maana mtoto alikuwa hajageuka. Nikamwambia asiende kwanza hospitali anisubiri nakuja, nilipofika nikaja moja kwa moja kanisani hapa Efatha Ministry Mwenge nikaonana na Mchungaji Mwakisole, nikamweleza mwanangu ameambiwa atajifungua kwa upasuaji, Mchungaji akaomba akasema atajifungua salama kwa njia ya kawaida, ila msimpeleke hospitali hadi uchungu utakapoanza. Uchungu ulipoanza tukampeleka hospitali, manesi waligomba kwa nini tumemchelewesha, maana alitakiwa kuwahi kwa ajili ya upasuaji, mimi nikamwambia mwanangu hatajifungua kwa upasuaji. Wakasema haiwezekani maana mtoto hajageuka na mtoto akiwa katika hali hii huwa tunafanya operation ili kuokoa maisha ya mama na mtoto hivyo ni lazima apasuliwe. Nikampigia Mch. Mwakisole nikamweleza, akasema niweke simu kwenye tumbo aongee na mtoto, nikaweka akaomba. Baada ya hapo hali ya mwanangu ikawa mbaya akaanza kutapika hadi, kuishiwa nguvu. Akakimbizwa chumba cha upasuaji, mimi nikatoka nje nikimshukuru Mungu. Katika hali isiyo ya kawaida mtoto akaanza kutoka haraka kwa miguu akamalizia na kichwa, hadi manesi wakashangaa na wao walikiri kuwa ni Mungu aliyefanya. Wakaniambia usiache kumshukuru Mungu kwa jambo hili. Ndio maana nipo mahali hapa kumshukuru Mungu maana alisema kupitia Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira kuwa sio sawa kujifungua kwa operation, bali mtoto anatakiwa kutoka kupitia njia aliyoingilia. Namshukuru pia Mchungaji mwakisole kwa kuwa pamoja nami, Mungu ambariki sana. MUNGU HASHINDWI

Image

PICHANI: Waimbaji wa Efatha Ministry Chipkizi wakimtumikia Mungu katika Ibada ya pili inayoendelea hapa Efatha Ministry Mwenge Dar

Image

MCHUNGAJI DAVID MWAKISOLE: SOMO: SIRI YA BARAKA ZA MUNGU WAPI ZILIPO: Kumbukumbu la torati 28:1 "takuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani" . Baraka sio kuwa na fedha peke yake kwani unaweza kuwa na fedha na bado ukawa umelaaniwa, baraka ni kuwa karibu na MUNGU ili uweze kupokea vya kwake. Asili ya baraka zote ni YESU na ili tuweze kuzipata hizo baraka ni lazima tuachane na mambo yote yanayo haribu uhusiano wetu na YESU na kutuweka mbali na MUNGU. Inawezekana ni dhambi ya uvivu, uvivu katika mambo ya MUNGU ni kikwazo kikubwa cha kupokea baraka zetu toka kwa MUNGU.

MCHUNGAJI DAVID MWAKISOLE: SOMO: SIRI YA BARAKA ZETU WAPI ZILIPO: Baraka maana yake ni kinyume cha laana, ukiambiwa umebarikiwa maana yake hujalaaniwa na ukiambiwa umelaaniwa maana yake kwako hakuna baraka. Laana imekuja baada ya mtu kumkosea MUNGU, mtu akikwambia umelaaniwa maana yake uko mbali na MUNGU na akikwambia umebarikiwa maana yake uko karibu na MUNGU. Asili ya baraka zote ni MUNGU mwenyewe, hutaweza kuziona baraka mpaka umepatana na MUNGU na ukifarakana naye tu utaanza kuona laana zikikufuata na kila unachokifanya kinaharibika.

Image

Karibuni wote katika ibada za Jumapili hapa Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania, ibada ya kwanza inaendelea pia mnaweza kusikiliza ibada za siku ya leo Live kupitia Online Radio www.mixlr.com/efatha-ministry .

Tne Leaders Service is in session at Efatha Ministry Eldoret. In whichever position you have been given to serve; serve it well, for the Glory of GOD. Pastor Godson Mmari. EFATHA MINISTRY's photo.

Image

Waimbaji wa Efatha Ministry mass choir wakisifu Mungu katika ibada ya kwanza leo Jumapili Efatha Ministry Mwenge,

Image

Karibuni wote katika ibada ya kwanza hapa Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania. Popote ulipo unaweza kusikiliza ibada za siku ya leo LIVE kupitia www.mixlr.com/efatha-ministry

Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Akiwabariki watoto wa Kituo cha Mlimani Eldoret (Kenya)

Image

Somo: MLANGO: MCHUNGAJI Angelina Mdadila: Wagalatia 4:1"Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote". Sisi tuliookoka ni warithi pamoja na BWANA na hatutakiwi kuishi tena kama watumwa bali kama warithi. Katika maisha ya mtu yeyoye ipo milango miwili, mkubwa na mdogo, katika mlango mkubwa vinapita vitu vikubwa na vingi na katika mlango mdogo vinapita vitu vichache na vidogo. Mlango mkubwa unaruhusu vitu vikubwa na vikuu kukujia, pia ukipita katika mlango huu mkubwa unakutana na watu wakuu. Ukipita katika mlango mdogo unakutana na watu wa chini na utakutana na mambo madogo.

Image

Somo: MLANGO:

Image
Mchungaji Angelina Mdadila: Hatari ya mlango mkubwa unapofunguliwa vinaingia vitu vingi hata vibaya na inawezekana usiweze kuvijua japokuwa kusudi la mlango mkubwa sio hilo. Mlango mkubwa unatakiwa kuwa na tahadhari kubwa kwani unapitisha vitu vingi. Katika mlango mdogo vinapita vitu vichache na mtu mmoja mmoja na sio rahisi kupitisha vitu vibaya. 1Wakorintho 16:9 "Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao". Mlango mkubwa umefunguliwa na Mungu katika maisha yako lakini anasema yuko azuiaye. Mlango mkubwa umekusudiwa ili kuingiza mema na mazuri katika maisha yako lakini yuko azuiaye. Wakati huu wateule wa baraka za Mungu wamefunguliwa mlango mkubwa lakini yule azuiaye amewafanya kuwa wadogo, wakienda sokoni wanakuta nyanya nzuri na mbaya(masaro) wakiangali zile nzuri wanajiona wadogo kuliko nyanya na wananunua masaro ambayo yanatakiwa kuliwa na wanyama au kuku.

Mchungaji David Mwakisole:

Image
Mathayo 5:21-37 " Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.  Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.    Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,    iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.  Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.    Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.    Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;    lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.    Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitu

Mtume na Nabii J. E.Mwingira

Image
Ukimpendeza MUNGU hata ukimkosea Anakuhurumia, hata kama Uliaibika vya Kutosha leo MUNGU Anakwenda kutoa Aibu yako na Anakwenda KUKUFUNIKA na UTAKATIFU Wake, ya Kale yamepita na tazama yamekuwa MAPYA. Sema huu ni MWANZO wa Safari yangu ya UMILELE, MUNGU aliyeanza KAZI na Mimi ATAIMALIZA Hataishia Njiani.

USHUHUDA

Image
Naitwa Khadija Makani, napenda kumshukuru MUNGU kwa MATENDO yake ya Ajabu aliyonitendea. Nina miaka sita nilikuwa natoa funza katika sehemu zangu za siri, nilihangaika sana kutafuta UPONYAJI lakini sikupona hadi ndugu zangu wakanisusa wakasema huyu mtu kufa hafi wala haponi wakaacha kunihudumia. Nikawa nimekaa ndani tu nateseka ila kuna Mama mmoja akanipeleka Hospitali lakini ugonjwa haukuonekana, ndipo nilipoletwa Efatha Nikaombewa na baada ya Maombi nilipoenda Hosp italini ndipo ugonjwa Ukaonekana. Nikagundulika nina uvimbe tumboni nikafanyiwa upasuaji Nikakatwa utumbo nikawekewa wa plastiki, ndipo nikagundulika na Kansa tena nikawa naendelea na Matibabu huku nakuja kwenye Maombi. Nilipoenda Kupima tena wakaniambia kuwa NIMEPONA na hata dozi ya dawa sijamaliza, NAMSHUKURU sana MUNGU kwa MATENDO YAKE aliyonitendea sitarudi nyuma bali NITAMTUMIKIA huyu MUNGU wa Mbinguni, Namrudishia SIFA na UTUKUFU, YEYE MUWEZA wa Yote. JE? Wewe una tatizo gani??? Uwe na AMANI, YESU anaponya..

USHUHUDA.

Image
Kwa jina Naitwa Elizaberth Mwenda: Napenda kumshukuru MUNGU kwa MATENDO Makuu aliyonitendea kwa kuniinua kwenye Elimu yangu kwani nilikuwa mtu wa nchini sana kielemu na sasa kwa upande wa academic NAONGOZA. Pia namshukuru MUNGU kwa kupitia kinywa cha Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira tulipokuwa Kusanyiko Kibaha aliposema tusikubali kuongozwa na viongozi wasiofaa tuache kulalamika tugombee hizo nafasi, nikalishika hilo neno na kuchukua hatua kwani nami nilikuwa naonewa sana na viongozi shuleni nikaamua kugombea uongozi na sasa ni Kiongozi.  UKIMUAMINI MUNGU na UKIWAAMINI WATUMISHI WAKE, Utafanikiwa... Usikate tamaaa kwa MUNGU kuna MAJIBU ya tatizo lako.

USHUHUDA :

Image
Naitwa IRENE: Namshukuru sana MUNGU kwa kunipa KIBALI cha kufika katika Madhabahu yake, namshukuru kwa ajili ya Elimu yangu na Maisha yangu kwa ujumla. Nimehangaika sana katika elimu yangu nikiwa nasomea cheti cha Udaktari kwa muda wa miaka 4. Nilikuwa nakaa nyumbani muda mwingine kwa kukosa ada, siku nyingine nashinda njaa hata siku mbili sijala, lakini namshukuru sana MUNGU kwa kunitia Nguvu mpaka nimemaliza na juzi nimemaliza kufanya mtihani namshukuru sana MUNG U japokuwa nilikuwa naumwa mara kwa mara lakini nilikuwa naongoza katika mitihani yangu.  Wakati sijaokoka nilikuwa nina tabia mbaya nilikuwa na kiburi na nina Nunanuna tu, namshukuru sana MUNGU baada ya KUOKOKA sasa hivi tabia yangu IMEBADILIKA sana, nilikuwa hata nikiambiwa nioge aliyeniambia nakasirikia tu, ilifika mahali hata shuleni nilitengwa na kila mtu, NAMSHUKURU sana MUNGU sasa nina Marafiki na nimekuwa mtoto mzuri shuleni na hata nyumbani. MUNGU azidi kuibariki Huduma ya Efatha pamoja na Mtumishi wake Mtume

NJOO KWA YESU, ABADILI MAISHA YAKO.

Image
MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA. MUNGU ninaye mtumikia ni MUNGU abadilishaye mambo. HAIWEZEKANI narudia HAIWEZEKANI umpokee YESU moyoni mwako kwa kumaanisha alafu hakuna mabadiliko yeyote kwako. Hutawaambia watu kuwa ninaye YESU, bali wao watakuuliza nini kimekutoke mwenzetu? wengine watakiri waziwazi au mioyoni mwao kuwa hakika unaye MUNGU. Kuzaliwa kwa Bwana YESU, kulikuwa kwa aina yake, kulitanguliwa na wajumbe kadhaa,  Mathayo 1:18-23 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa

NENO JUMAPILI TAR. 16-10-2016 : UTAKATIFU NDIO KUMCHA BWANA

Image
MCH: DAVID MWAKISOLE Mathayo 5:21-34 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.   Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.   Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,   iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.   Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;   lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.   Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima

IPOKEE “NGUVU YA MUNGU “ I – MTUME NA NABII: JOSEPHAT E. MWINGIRA

Image
   KUSUDI LA KUUMBWA MWANADAMU Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi na hiyo nchi ilikuwa ukiwa na utupu, kwa sababu mvua ilikuwa haijanyeshea na mwanadamu hajaumbwa ili kuhudumia.  Mwanzo 1:1–2 “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu nan chi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza liikua juu ya uso  wa vilindi vya maju; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maju”.   Mungu aliumba mtu, kwa kufinyanga udongo na kupulizia pumzi yake akawa nafsi hai. Asili ya mwili wa mtu huyu ni udongo na asili ya pumzi iliyo ndani yake inayobeba uhai ni Mungu. Pumzi hiyo huingia na kutokea puani. Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. Asili ya makao yake huyu mtu ni bustanini.   Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”.  Mungu aliumba mwanaume na mwanamke kwa kusudi malum na aliwaita jina la ADAMU.   Mwanzo 5:1 – 2 “Hiki ndicho kitabu cha vizaz

AINA TATU YA JAMII ZA WANADAMU HAPA DUNIANI

Image
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira UZAO WA KISHENZI Uzao wa kishenzi hauna habari ya nini kinachoendelea  mahali walipo. Ukiwatembelea nyumbani kwao, hawawezi kukukarisha,  na wakati unaaga kuondoka, ndipo wanauliza unaondoka ? wanajibaraguza kukutafutia kiti. Uzao wa kishenzi daima wanawaza watapata nini kwenye kila jambo na kazi yao ni kuchafua, kuiba, kuharibu na mambo yote mabaya. Hawaoni aibu kufanya mambo ya kishenzi, hata wakipata mapato hutumia yote, hawana mpango wa kuwekeza. Wanaishi kwa gharama kubwa na hutumia nguvu nyingi kujilinda. Hawaoni shida kula fungu la kumi, Hata kama wameokoka. Mtu wenye tabia za uzao wa kishenzi ni vigumu kuingia mbinguni. Ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya watumishi wa madhabahu kusema kuwa fungu la kumi ni lao wenyewe. Kula fungu la kumi inamaana unajifanya kuwa Mungu mwenyewe. Hawa watumishi wana mbingu gani ya kufungulia watu madirisha? Waowenyewe wanatakiwa kutoa fungu la kumila mapato yao lakini nao hawatoi . Malaki 3

SOMO: MASKINI WA ROHO

Image
MCHUNGAJI VICTOR GASPA Mathayo 5:3, 8 “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. ...8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.” Maskini wa Roho ni nani? Ni Yule ambaye anatamani kumuona Mungu akigusa maisha yake na anatamani afanye jambo ili Mungu atukuzwe. Huwezi kumuabudu Mungu kama wewe si maskini wa roho.  Zaburi 42:1-3 “Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako". Maskini wa roho ni yule mwenye kiu na shauku ya kumuona Mungu katika maisha yake, maskini wa roho siyo yule anayezunguka huku na kule kwenye kila semina anayosikia, huyu ni mzururaji na siyo maskini.   Maskini wa roho ni yule anaye mng’oja Bwana, hatakama leo hajamtendea anaamini ipo siku atamtendea, ni mtu ambaye anajua

DHAMBI

Image
MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA: Mungu wetu anatupenda sisi tulio wake, mwanadamu aliumbwa katika ukamilifu lakini baada ya dhambi alipoteza kila kitu.  Dhambi ni nini? Ni ile hali ya kuanguka katika sheria na mpango wa Mungu, dhambi ikiingia kwa mtu anapoteza muelekeo na anakuwa kituko na magomvi katika ndoa yanaingia. Dhambi ni mdudu mbaya sana, inaleta chuki, inaondoa upendo inakufanya unakuwa hovyo, inakushusha uthamani wako. Mungu anakupenda na anakuwazia mambo mazuri. Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Mungu alimpenda Musa kwa sababu ya mambo yake aliyokuwa akifanya na ndio maana akasema sijawahi kumuona mtu mpole kama Musa. Upole ni ile hali yako ya kufanya mambo pasipo kukurupuka, upole haimaanishi kutembea kwa unyonge kama mgonjwa bali ni kuwa makini katika mambo unayo yafanya. Acha haja zako zijulikane na Mungu na siyo wanadamu, siyo katika kila jambo unalopitia unatangaza mpaka mtaa wa tatu.

USHUHUDA:

Image
Naitwa SAIMONI METELE: Namshukuru sana Mungu ameniponya kwani nilikuwa naumwa presha na kisukari tangu mwaka 2006. Nilihangaika sana ili nipone lakini sikupona, mwaka 2014 siku ya jumapili nilizidiwa nikapelekwa Muhimbili na nikalazwa. Ilipofika jumatatu saa tano nikazidiwa presha ilifika 250, nikasikia ubaridi kutoka miguuni mpaka kichwani kisha nikazimia. Nikakaa kama masaa sita nikapata fahamu kidogo kisha nikazimia tena, nikapelekwa chumba cha wagonjwa mahututi nikakaa siku tisa . Nilipozinduka nikawa nimepooza upande mmoja. Nikakaa Muhimbili kama mwezi mmoja tena na nilipokuja kupimwa Daktari akaniambia figo yangu imefeli, baada ya muda nikarudi nyumbani Manzese nikaenda Kanisa moja la palepale Manzese lakini sikupona. Mtoto wa dada yangu akaniambia Baba kuna Kanisa moja la Efatha liko Mwenge ukienda utapona. Nikaenda Efatha Mwenge na nikaombewa baada ya wiki moja nikapona. Namshukuru sana Mungu na Watumishi wake walio niombea. Nilikuwa nimekata tamaa natamani kumeza dawa ili

SOMO: ROHO WA IBADA (ROHO WA KUMCHA BWANA)

Image
MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA Ni namna unavyo fikiri na kuwaza ufanye nini ili Baba yako wa Mbinguni apendezwe na wewe. Kuabudu sio kunena kwa lugha peke yake, wala sio kupiga kelele tu bali ni namna unavyotenda. Kuabudu ni ile hali ya kupondeka moyo na unakuwa kama mtu asiyekuwa chochote mbele za Mungu, unapoenda kwenye uwepo wa Mungu unajiona kuwa wewe mwenyewe si chochote fahamu zako zinakuwa hazifanyi kazi bali akili  ya Mungu. Unapofika hatua hiyo chochote unachokifanya ni kwaajili ya Mungu na huwezi kumzuia Mungu chochote na upo tayari kufa kwa ajili ya Bwana. Kuabudu sio namna unavyosema kwa kinywa chako tu bali ni jinsi unavyojisikia vizuri ukiwa kwenye uwepo wa Mungu. Kuabudu ni kule kumpenda Mungu kwa moyo wako wote..

ROHO WA BWANA JUU YANGU

Image
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA: Ukitembea na Roho wa Bwana utajua majira yako na atakufanya kuwa mtenda kazi na mwana wa Mungu. Roho wa Bwana juu yako ni kukuonyesha na kukufanya uwajibike na kufanya kazi ya Mungu kwa bidii. Ukishaanza kuonyesha unafanya kazi ya Mungu kwa bidii bila mtu kukusukuma Mungu anakuthibitisha. Mungu akikuamini anaweka hazina yake kwako, ni vizuri sana ukafanya kazi ya Bwana bila kushurutishwa. Mungu akikuamini hutakaa ukose kitu, unakuw a mgawaji, hautakuwa na uhitaji wa kitu chochote k amachakula, nguo na vitu vyote unavyovitamani havitakuwa tatizo kwako. Kuwa mwaminifu mahali popote ulipo, kwa kupitia kile kidogo unachokipata, ndivyo utamfanya Mungu akuamini kukupa Baraka zake maana anajua utaweza kuzitunza. Luka 10:19 “ Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”

SOMO: KARAMA;

Image
MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA: Shetani akitaka kukujaribu anakuletea kitu ambacho kinafanana sana na kitu unachokipenda. Ili Mungu akutumie atakupitisha katika kila jaribu ili aone kuwa je unampenda?. Ili uweze kusonga mbele ni lazima ushinde hiyo mitihani na ukishindwa utarudia tena na tena.Aliyemuweka gerezani Yusuphu sio mke wa Potifa bali ni Mungu mwenyewe kwa kuwa alikuwa anakusudi naye, akaleta mkuu wa waoshaji na mkuu wa waokaji w akiwa wameota ndoto, Mungu alifanya hivyo kwa makusudi. Wale watu wakaja kwa Yusuphu na akawatafsiria ndoto zao, na huo ndio ukawa mlango wa Yusuphu wa kutokea, Yusuphu hakuangalia kuwa yeye ni mfungwa bali aliwasaidia. Ili Mungu akutumie ni lazima ufike eneo la ukomavu hatakama unashida kubwa kuliko za wengine unazisahau na kuwasaidia wengine. Tatizo la kila mtu ni suluhisho la tatizo la mwingine.

SOMO: KARAMA;

Image
MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA: Unaposhiriki mateso pamoja na Kristo, utukufu wa Mungu na Roho wake unakaa pamoja nawe.  Mungu anataka umtolee kile ambacho unakipenda ndipo atajua kuwa unampenda, Ibrahim alipoambiwa amtoe Isaka hakuwa na maswali mengi kwa kuwa alikuwa anampenda Mungu. Ibrahim ndani ya moyo wake alikuwa tayari amemtolea Mungu Isaka kama zawadi alipotaka kumchinja ndipo malaika wakaleta kondoo. Ndipo Mungu akasema sasa nimejua kuwa unanipenda. Ili Mungu ajue kuwa unampenda ataona sadaka zako unazomtolea. Katika mlima ambao Ibrahim alitaka kumtolea Mungu Isaka awe kama dhabihu ya kuteketezwa, ndio mlima uleule ambao Bwana Yesu alisulubiwa, Mungu alipoona Ibrahim alikuwa tayari kumtolea mwanawe wa pekee ndio Mungu akamtoa mwanawe mpendwa Yesu Kristo awe dhabihu kwa ajili ya ulimwengu. Ili Mungu ajue kuwa unampenda toa dhabihu ambayo itamgusa. Hakuna kitakachotokea kwenye maisha yako mpaka umechukua hatua, Mungu hawezi kufanya kitu chochote k
Image
MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA: Matendo 17:26-28 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone.....” Mwanzo 39:1-5 “Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. Bwana akawa p amoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake........” Adui zako watasababisha mteremko wa maisha yako, wa Ishmael walimtoa Yusuphu katika shimo na wakamuuza kwa Potifa ili kutimiza hatima ya Yusuphu. Maombi yangu kwako ni kwamba Mungu akupeleke mahali sahihi na kwa muda sahihi siku zote za maisha yako.

BAADHI YA PICHA SIKU YA TATU YA KUSANYIKO KUU LINALOENDELEA HAPA PRECIOUS CENTER KIBAHA TANZANIA

Image