Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Tuesday, March 31, 2015

UKOMBOZI NA UPONYAJI Ni Kwa Ajili yako; YESU Anakupenda, MUNGU Anakupenda, ROHO MTAKATIFU Anakupenda.

IBADANI JUMAPILI EFATHA MWENGE

SHUHUDA

SARA KISINGI: Namshukuru Mungu amenifanyia mambo makuu mawili, nilikuwa sijaokoka nikaja Efatha, nilikuwa nina uvimbe tumboni na nilitakiwa kufanyiwa operation, lakini Askofu wangu akasema hautafanyiwa operation Mungu ni Mwaminifu, nilipofika Kibaha nyumbani, niliendelea kuumwa sana nikapelekwa Amana Hospitali ikashindikana na nilipelekwa Muhimbili lakini baada ya kufika daktari akasema njoo tukupime, baada ya kupimwa akasema kuna jiwe kubwa sana, na akaingiza mkono akalivuta likatoka na akawaita watu waje kunipiga picha kwani mimi ni mtoto wa ajabu nimezaa jiwe, lakini nikamwambia mimi sio mtoto wa ajabu mimi ni mtoto wa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Baada ya hapo nikaruhusiwa kwenda nyumbani.
Pia nilikuwa na kesi ya kusingiziwa, nilipotoka nyumbani kuelekea Polisi nikatamka neno nikasema Mungu mimi hii kesi sio ya kweli naomba unisaidie naingia Polisi naamini nipo na Wewe.
Mungu wa Efatha alivyo wa Ajabu, kesi ilienda hadi mahakamani lakini mawakili walianza kugombana wao kwa wao, nikaambiwa niondoke kwani kulionekana hakuna kesi walikuwa wamenisingizia kesi ya uongo. Nikaruhusiwa nikaondoka. Namshukuru Mungu wa Baba yangu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira kwa matendo makuu Aliyonitendea.

Anastella Mchomvu: Ninamshukuru sana Mungu wa Efatha kwa ajili ya matendo makuu aliyonitendea. Wakati nakwenda Kusanyiko Kuu Kibaha Mwaka jana nilikuwa natafuta mashamba na nilikuwa natamani mashamba makubwa na nilipofika Kusanyiko Mtumishi wa Kenya akawa anafundisha somo la "Mimi ni mtu Mkubwa sana", Usiku ule nilifanya maombi na nikajibiwa usiku ule ule, nikapigiwa simu kuwa kuna mashamba Morogoro, na baada ya kutoka Kusanyiko mimi na Mume wangu tulienda Turiani Morogoro tukapewa mashamba makubwa kwa bei ya ajabu, na nilipata hekari 200 kwa ajili ya kulima, pia tumenunua hekari 10 kwa ajiri ya Efatha, na nimekuja na hati ya mauziano ya hekari 10 kwa ajili ya Efatha.
Pia Bagamoyo nimepata hekari 100, pia napenda kumshukuru Mungu kwa kunipatia Nyumba kwani jana tarehe 28/03/2015 nimefanya ibada ya kuweka wakfu nyumba yetu, Mungu wa Efatha amenifanyia maajabu.
Pia tulikuwa tumetoka kuwaona wazazi, tulipofika Tabata tulipata ajali iliyosababisha magari 4 kugongana lakini kwenye gari yetu hatukuumia, kwani nilimwambia Mungu hili gari nililiweka wakfu kwa ajili ya kazi yako.
Pia napenda kumshukuru Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Watumishi wote walio kuwa wananiombea.
 Hongereni wote mliompokea Bwana Yesu leo, kwa nguvu yake awawezeshe wote kuishi maisha ya ushindi INAWEZEKANA kuishi maisha Matakatifu hapa Duniani. Kuanzia leo kushindwa siyo sehemu ya maisha yenu Ibilisi ameshindwa kabisa.

Wednesday, March 25, 2015

IBADANI JUMAPILI TAREHE 22/03/2015

Mchungaji Mary Abel wa Eneo la Utukufu aliyeongoza Ibada ya Neno katika Ibada ya Kwanza..
 Efatha Mass wakimuimbia Mungu wetu, hakika wameimba kwa uzuri wa aina yake Mungu azidi kuwapaka mafuta kwa ajili ya utumishi wao. Amen
 Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira naye yupo katika Ibada hii ya kwanza ni Baraka ya pekee kuwa na Baba yetu. Amen
 Pichani: Mchungaji Thadeo Msuya akihubiri kwenye Ibada ya pili, Efatha Mwenge Dar es salaam.
 Watumishi wa Mungu kwa utulivu wakifuatilia Ibada ya Neno iliyoongozwa na Mchungaji Msuya.
 USHUHUDA
Hery Jackson, namshukuru Mungu kwa kunipa kibali fanya kazi yake Precious Center Kibaha, baada ya kufanya kazi kwa uaminifu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alinikabidhi kwa mtu mmoja akamwambia nenda na huyu kijana ukamfundishe kazi mpaka kitu kitokee, kweli baada ya hapo niliendelea na huyo mtu niliepewa akawa ananifundisha kazi ya uhandisi wa majengo na barabara na kweli kimetokea kitu kama baba alivyosema. Sasa nafanya kazi katika makapuni mbalimbali kama Mhandisi namshukuru Mungu kwa maana kwa elimu niliyonayo nisingeweza kufanya kazi kama hii ila ni kwa neema tu. Pili namshukuru Mtume na Nabii na mchungaji wangu Aimana Dominick kwahiyo nimekuja kushuhudia haya Mungu aliyonifanyia ili kuujenga ufalme wake, Amen.

Wednesday, March 18, 2015

WAMAMA AMBAO MMEBARIKIWA HII YA KWENU KUTOKA KWA MAMA YETU.

Wa mama ambao mmebarikiwa, mna maduka Kariakoo, mna Maduka Mwanza, Mna maduka sehemu mbalimbali, mnaenda Dubai, mnaenda China, mmeanza kukosa Uaminifu, hebu ACHENI, hiyo ni dhambi. Hiyo Baraka isikufanye usimuheshimu Mumeo, usimfanye Mumeo housegirl, kama ulikuwa unamuwekea Mumeo Maji endelea kumuwekea, Hela siyo Mume wako, Hiyo ni Maua, najua kuwa MUNGU aliyekupa hizo hela Anakuangalia; Kubali KUBADILIKA, Kubali KUJIREKEBISHA, Acha hiyo Dhambi.

WENYE SAFARI YA MBINGUNI HII INAWAHUSU

Ni lazima Waji Examine, Je pale Nyumbani wanajua Umeokoka? Mkeo anajua Umeokoka? Mumeo anajua Umeokoka? Watoto, Jirani, Wafanyakazi wenzio, Chuoni, Shuleni Wanajua Wewe Umeokoka?
Matunda yako ndiyo YATAKAYOSEMA kuwa Wewe Umeokoka, Je hiyo ndivyo ilivyo? Matunda yako yanaonyesha Wewe Umeokoka? Mumeo, Mkeo, Watoto, Jirani na Wote Wanakiri kuwa Wewe Umeokoka? Au unamdhalilisha KRISTO?
Jichunguze.

IBADANI TAREHE 16/03/2015 EFATHA MWENGE

SHUHUDA

Naitwa Anastazia mmasa namshukuru Mungu kwa yale aliyonitendea nikiwa nina hii mimba ya mtoto huyu nilikuwa nikijisaindia haja ndogo na utumbo mrefu ulikuwaa unatoka nikawa na maumivu makali sana na nilpoenda hospitali mnazi mmoja daktari aliniambia niende muhimbili na lipofika nikakuta kuna foleni sana niliamua kurudi mnazi mmoja wakaniambia nikanunue dawa na nilipoanza kutumia zile dawa nikawa napata maumivu sana na zilikuwa zimebakia dawa za siku tatu nikamwambia yesu naomba unihurumie mimi mtumishi wako . Siku za kujifungua zilipofika mama Chitete akaniambia unamwamini Mungu wa Efatha kuwa anaweza ? nikamwambia Amen na muda wa kujifingua ulipofika niliingia leba ya Efatha na mpaka jioni nikawa sijajifungua nikapelekwa mhimbili baada ya muda mfupi nilijifungua salama nikiwa pale hospitali dada mmoja alikuwa anatakiwa afanyiwe upasuaji lakinialiponiona nimejifungua kwa muda mfupi baada ya kufika hospitalini akasema mimi nataka nijifungu kama huyu dada na kweli ikawa kama alivyosema

Namshukuru Mungu ameniokoa na ajali.
Adam Adam, Namshukuru Mungu nilikuwa naendesha gari aina ya noah nilikuwa naenda Mbeya, nilipofika Iringa lile eneo ambalo gari ya Manjinjah na lori lilipata ajali mimi niliingia kwenye lile shimo lililowaua wenzangu na baada ya hapo gari yangu matairi ya nyuma yalipasuka yote gari likapinduka mara nne lakini sikupata majeraha ya aina yeyote na nilitoka mzima nikiwa na akili zangu zote na kuanza kuwasaidia wenzangu waliokuwa wameumia. Tulikuwa saba kwenye gari mmoja alifariki na wengine walikuwa wamevunjika miguu, viuno na viungo mbalimbali.Neno la madhabahuni linatulinda kwasababu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema hatutakufa kwa ajali, kweli nimeamini Mungu anatembea na wale wampendao. Wana Efatha hatutakufa kwa ajali sawasawa na Neno la Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira.

Shuuda za watumishi wa Mungu waliotumwa Tabora.
Mama mmoja alikuwa kichaa akasema yeye anatokea Msumbiji na anaabudu Sabato hawezi kuoka, wakati tunamuongoza sala ya toba akawa anasinzia, alikuwa na irizi kiunoni imefungwa akasema msiifungue, baada ya maombi kukolea akaifungua ile irizi yeye mwenyewe, baada ya kuombewa kumbe ile nyumba wanashiriki mambo ya kichawi na huyu ni mtu wa Uganda akatoa pembe akatupa nje ile irizi na pembe za uchawi na baadaye akaombewa, na tukaichukua ile irizi na vitu vya uchawi tukavichoma moto, ameokoka na anasoma madarasa Efatha.
Kijana mwingine alisema hawezi kuokoka ana dini yake, baada ya kuongozwa sala ya toba akaanza kusema ana mila na desturi zao, baada ya kuombewa akaanza kusema alikuwa anaumwa, kuna siku alikuwa anakunywa maji inzi aliingia kwenye koo aka kaa hapo mpaka sasa anamiaka 7 bila kutoka hapo kwenye koo, akawa anashindwa kula vizuri na kunywa maji.Pia mke wake hazai wala hawana mtoto,baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu wa Efatha inzi akatoka katika koo lake, amesimama katika wokovu na anasoma madarasa na mke wake,hivi sasa mke wake ni mjamzito.Anamshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyo mtendea.
Dada mmoja anaitwa Asha alikuwa mchawi na baada ya watumishi wa Mungu kumuombea walimchukua na kuishi nae,lakini akajaribu kuwawangia watumishi wa Mungu usiku waka mkamata, alipoendelea kuombewa alikataa kuacha uchawi, Watumishi wa Mungu walimrudisha kwao na kumuonya kama hataki kuacha uchawi atakufa, baada ya siku chache akafa kutokana na nguvu ya Mungu. Kama ilivyo andikwa usimwache mchawi aishi.
 Pichani: Mch. Thadeo Msuya aliyesimama katika Ibada ya Neno Ibada ya pili.
 Katika Picha: Ibada za watoto ambapo watoto hufundishwa kulingana na umri wao, wana waalimu maalum walioandaliwa ili kuwalea na kuwafundisha watoto. Ni vizuri kuwalea watoto katika Mungu ili wawe na msingi mzuri wa Imani. Unapokuja Ibadani na mwanao usihofu wakati wewe ukiwa kanisani, mwanao atakuwa kwenye ibada zao maalum. Karibu sana na Mungu akubariki


 Pichani: Kanisa likiwa katika maombi Ibadani. Live Ibada ya kwanza
 Pichani: Wana wa Mungu wakiwa katika Ibada ya maombi Ibada ya kwanza Efatha mwenge Dar es salaam Tazania

Tuesday, March 10, 2015

Tuesday, March 3, 2015

EFATHA MATUKIO NA HABARI MIKOANI NA NJE YA NCHI: Leo tuko Mkoa wa Efatha Ministry- Zanzibar.

Pichani: Viongozi wa Mkoa Efatha Ministry- Zanzibar wakiongozwa na Mch. Kiongozi, wakiwa katika Ukaguzi wa Kupata eneo la Kupanua Kituo kimojawapo cha Mkoa huko Zanzibar.

 Pichani: Mchungaji Kiongozi wa Mkoa wa Efatha Ministry -Zanzibar, Mch. Henry akiwa katika Mojawapo ya Safari za Kiutumishi kutembelea Vituo huko Mkoani Zanzibar.

 Pichani: Watumishi (Wachungaji) wa Mkoa Efatha Ministry -Zanzibar wakiwa katika Safari ya kwenda eneo la Kituo mojawapo la Efatha Ministry huko Zanzibar (Mbuji) ambapo pia kuna Prayer Mountain ya Mkoa Efatha Ministry- Zanzibar.
 Pichani: Wana wa MUNGU wa Efatha Ministry Mkoa wa Zanzibar, wakiwa katika mojawapo za Kazi za Kiroho huko Zanzibar.


PIchani: Ibada mojawapo za Uponyaji na Ukombozi huko Zanzibar.
(Wewe uliyepo Unguja au Pemba, na ungependa kujumuika kwa pamoja na Wana Wa MUNGU wenzio huko Unguja au Pemba, au unahitaji Msaada wa Kiroho ukiwa huko Pemba au Unguja, basi unaweza kupiga simu hii: 0652338343 au tuandikie e-mail kupitia ict@efathaministry.org au efathaict@gmail.com) Ubarikiwe.

 Pichani: Mojawapo ya Mikesha ambayo huwa inafanyika huko Zanzibar.

EFATHA MATUKIO NA HABARI

Pichani: Mh. Nape akiingia ukumbini Kibaha Precious Centre kuzungumza na Wachungaji wa Efatha.KUTOKA IBADANI 1/3/2015

MTUMISHI SUZY MSOFE
SOMO:WANA WA MUNGU WANATAKIWA WAWAJE
Mathayo 5:8 " Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
"
SIFA ZA WANA WA MUNGU
1. Matendo yako yataonekana kwa maana kila utakalolifanya wataliona ni jema.
2. Maneno yako yatakuwa matamu na yakumpa Mungu utukufu.
3. Moyo wako ukiwa safi unakuwa na tabia njema na kuwapendeza hata wanadamu.
4. Wanamtafuta Mungu kwa bidii na wanaongozwa na Mungu na wanakuwa na muda kwa ajili ya Mungu
5. Wanakuwa na njaa na kiu ya neno la Mungu.
6. Wanatamani wengine waingie kwa Yesu ili waone uzuri wa Mungu.
7. Wana wa Mungu wakiudhiwa hawakasiriki, kwa sababu wao wanamtanzama Mungu anasema nini.

Pichani: Efatha mass choir wakimwimbia na kumtukuza Mungu wetu mkuu katika Ibada ya kwanza. Mungu wetu anatamani tumuabudu katika Roho na kweli.

 
Eneo maalum la maombi kwa waliofungwa na vifungo mbalimbali vya kipepo, wakiombewa na kufunguliwa, kwa Jina la Yesu.

 MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA Akisalimia kanisa katika Ibada ya kwanza.

 Pichani: Mojawapo ya Ibada ya watoto (sunday school) hapa Efatha Mwenge Dar es salaam. Watoto huwa na Ibada zao maalum na waalimu wao maalum kuwafundisha, kuwalea na kuwaombea watoto. Ni ibada nzuri sana kwa watoto,walikuwa na mitihani ya kile wanachofundishwa. Mlee mtoto katika njia inayofaa naye hataicha katika maisha yake yote.