Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Monday, February 23, 2015

SHUHUDA Jumapili tarehe 22/2/2015

Nilikuwa na Kibao cha Marufuku kwamba Siwezi kufaulu, lakini baada ya Kuomba na Kuvunja Kibao hicho, Nimefaulu na Nimepata DIVISION ONE.
Ester David Msimbi: Napenda kumshukuru MUNGU, katika kusoma kwangu nimekuwa nikifanya vizuri lakini nilikuwa sishiki Nafasi ya Kwanza, nilikuwa namaliza Kisutu Sekondari, wakati huo nilikuwa na mambo yangu mengi ya uongozi, nilikuwa sifanyi vizuri, nilipokuwa nafanya Mitihani nilikuwa sipati zile Division zinazo takiwa. Lakini baada ya Mafundisho ya Mchungaji wangu Mama Mdadila aliposema kuna “KIBAO cha Marufuku” kimeandikwa mbele yangu kwamba Sitafaulu, akasema “TUKIVUNJE” kile kibao, na baada ya Kuomba na Kuvunja kile kibao MUNGU Aliniona na Kunisaidia, nimepata Division ONE.
Na kuna maneno magumu kutoka kwa baba yangu mzazi alinitamkia, ya kwamba nitafeli nitapata ziro - ziro lakini MUNGU alijiinua kwangu na kunipa Kibali kwa Mwaka huu wa (Mtembeo Wa MUNGU Kwa Wale Alio Waridhia) nimepata Divison One. Lakini hii yote ni kwa sababu nilikuwa najitahidi sana katika masomo yangu lakini pamoja na hayo kuna kitu kilikuwa kinanizuia kufikia Division one, kila ninapo jitahidi nafasi yangu ilikuwa inachukuliwa na mwingine lakini MUNGU wa Efatha kutokana na maombi ya Mama Mchungaji Mdadila nimefaulu, namshukuru MUNGU sana Amina


YESU YU HAI, NI YULE YULE.....
SHUHUDA: Wana wa MUNGU wakishukuru MUNGU wetu MKUU kupata Mtoto baada ya Kukaa miaka 5.
Wana wa MUNGU pichani, waliamua kuja mbele ya Wana wa MUNGU, kuja Kumshukuru MUNGU MKUU kwa Matendo Makuu waliyotendewa, walikaa miaka 5 bila kupata Mtoto, walitiwa Nguvu na Mwana Efatha aliyekuwa anakaa nao jirani, aliwaambia "Msikate tamaa, MUNGU wetu ANAWEZA, YESU WETU YU HAI, YESU NI YULE YULE, YU HAI, ATAWAPA ITAJI LENU LA MOYO", Walizidi kuendelea Kuomba Kila siku,.. SIFA NA UTUKUFU NA UKUU ni kwa MUNGU WETU BABA YETU MKUU, AMETENDA, Hakuna JAMBO GUMU KWAKE, YEYE NI MUNGU si Binadamu, ANAWEZA, YU HAI, HAKUNA LINALOMSHINDA, Hata wewe hapo TAZAMIA KICHEKO CHAKO Sasa, POKEAAAAAA....

Monday, February 16, 2015

IBADANI JUMAPILI TAREHE 15/2/2015

USHUHUDA
Glory Samweli natokea Eneo la Sayuni napenda kumshukuru Mungu kwa ajili ya Baba Josephat pamoja na Maaskofu wangu wote, napenda kumshukuru Mungu amenipa Ndoa katika familia yetu tulikuwa hatuolewi ila kwa sasa ni mimi ambaye ni wa kwanza kuolewa na kuwa ndoa katika familia yetu. Nilijifunza, Baba Mtume na Nabii alisema JIFUNZE kupata maisha ya Ushuhuda, sasa nimeolewa na Ndoa yangu imefanyika mwaka jana tarehe 23/8/2014.
Ilikuwa sikumoja Baba alituambia tucheze ngoma za asili nilikuwa nina maisha magumu lakini nilikuwa nacheza huku nikimwambia Mungu nataka nikuone, na kweli Mungu aliniridhia Baba alinipa shilingi 10,000 nikaanzishe biashara, ila nilivyofika nyumbani nikamwambia Roho Mtakatifu hii hela haitoshi nataka unipe nyingi zaidi ya hii. nikaja kutoa fungu la kumi na sadaka. Siku ya pili ilipofika akaja mtu akasema nataka tufanye biashara, akanipa hela akaniambia chukua hii hela utanirudishia kidogo kidogo. Namshukuru Mungu sasa nina cafe yangu (mgahawa) na unajulikana sana ipo maeneo ya Masaki, namshukuru Mungu sasa nina jina kubwa.
 Naitwa Lucy Mtege wa Ubungo Maziwa, namshukuru Mungu kwa binti yangu kujifungu salama , jumaplili nilikuja na binti yangu alikuwa anasumbuliwa na pepo la ngono baada ya maombi binti yangu alitoka kwenye kiti akakaa chini akawa anajisikia vibaya na wahudumu walikuja kumchukua wakambeba na walimtoa nje na kumwingiza katika chumba kimoja na ndani ya kile chumba kulikuwepo na madaktari walimwombea na kupona mguu wake aliokuwa analalamika mama mguu unauma, lakini baada ya muda kuombewa maombi akawa mzima, na hakusikia tena yale maumivu ya mguu, na baada yakuachilia mguu mwanangu akaanza kusikia uchungu na kusaidiwa na madaktari akajifungua salama hapahapa kanisani mtoto wa kike anaitwa Eliakunda .

 TANGULIZA MAMBO MUHIMU KWANZA?
Jambo moja muhimu wewe unatakiwa uwe wa muhimu ufanye mambo ya muhimu, hakuna mtu anayefanya mambo ya ovyo ovyo alafu akawa mtu muhimu, fanya mambo ya muhimu ili uwe mtu muhimu. Unaweza ukaona mke wako, gari, kazi, nyumba na watoto ni wa muhimu kumbe sivyo kuna jambo ambalo unatakiwa kulifanya muhimu ndipo vitu vyote vitaonekana muhimu mfanye Mungu wa muhimu kwanza ndivyo vitu vyote kwako vitaonekana vya muhimu. Utafuteni kwanza ufalme wake na vingine vyote mtazidishiwa.
 Efatha mass choir wakimsifu na kumwabudu Mungu Ibadani, nifuraha na amani kumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. Karibu uungane nasi kila Jumapili

Wednesday, February 11, 2015

IBADA KUU JUMAPILI TAREHE 8/2/2015

SHUHUDA
ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUFAULU MASOMO
Naitwa Cosmas Peter, wa eneo la Shalom,
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza chuo kikuu na kufaulu mitihani ya CPA, leo niko mbele yenu namshukuru Mungu, mwaka 2009, nilimaliza chuo kikuu huria, nilifanya mitihani yangu ya CPA lakini sikufanya vizuri masaomo yote. Baada ya hapo nilianza masomo ya kukulia wokovu, ubatizo wa maji mengi na Roho Mtakatifu. siku moja Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema , ukitaka kutoka mahali ulipo dhamiria moyoni mwako, baada ya hapo niliondoka na kutoa pesa zilizokuwa kwenye akanti yangu ya benki na kutoa madhabahuni. Baada ya kutoa hizo pesa zote miezi mitatu baadaye nilipata pesa nyingine kwaajili ya ada ya chuo, ndipo 2014 nilianza tena chuo na kufanya mitihani yangu ya CPA na kufanya vizuri masomo yote, kwahiyo ndani ya mwaka mmoja nikafanikiwa kumaliza masomo ya CPA. Hivyo namshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea. Kwa hiyo nawasihi wana wa Mungu washike neno linalotoka madhabahuni na kulitendea kazi ndipo watakapoona matokeo yake.
  JOHN MASENGA (APATA UPONYAJI DHIDI YA UGONJWA WA TEZI DUME)
Leo ninatoa ushuhuda wangu nilikuwa nasumbuliwa na tezidume ambalo lilikuwa linanisumbua kwa mda mrefu madaktari walisema nifanyiwe upasuji lakini mimi na mke wangu tukasema daktari ni MUNGU hivyo tukaingia kwenye maombi, nilivyoenda kupima Daktari aliniambia sina tena tatizo hilo, yaani ni alinikuta ni Mzima kabisa hivyo namshukuru MUNGU.
 Efatha mass choir wakimsifu na kumwabudu Mungu wetu Ibadani leo.
Mch. David Mwakisole Mchungaji kiongozi Mwenge akifundisha Neno Ibada ya pili Somo lenye Kichwa :
MLANGO UMEFUNGULIWA MBELE YAKO NA WAPO MAADUI WANAOKUZUIA KUINGIA. 1Kor 16:5-9

Wednesday, February 4, 2015

JAMII


IBADA KUU JUMAPILI TAREHE 1/2/2015 EFATHA MWENGE

Kiongozi ibada ya sifa mass choir, Anna akiongoza mass choir kumwabudu Mungu wetu Ibadani.


Mch. Betson Kikoti, Mchungaji kiongozi Efatha Ministry Kenya, alihudumu Ibada ya kwanza, hakika Mungu wetu ni Mwema.
Mch Mese Komba wa Efatha Mbauda Arusha, akihudumu katika Ibada ya Pili Efatha Mwenge Dar es salaam

  Mimi ni Mtume Ruffas Christeen kutoka Pakistani
Nilikuwa katika kufunga na kuomba kwa siku 40 kwa ajili ya kutaka kumtafuta Baba wa kiroho ndipo Mungu akanionesha Mtume wake, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ambaye niliona habari zake kupitia mtandao wa Internet, Mungu akanimbia nije Tanzania ndipo nitakapomuona yeye (Mungu) kupitia Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, sasa ninafuraha kuwa nimempata Baba ambaye ni Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, na mimi sasa ni sehemu ya Huduma ya Efatha kule Pakistan
 Mtume Ruffas Christee kutoka Pakistan akisalimia kanisa hapa Efatha Mwenge, ni mtumishi aliyeona neema ya kipekee iliyopo kwa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na amekuja ili awe chini ya Huduma ya Efatha
 Pichani: Apostle Ruffas Christee na team yake wakiwa katika Ibada ya maombi, kanisani Efatha Mwenge. Jumapili hii tumekuwa na Ibada maalumu ya maombi.