Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Friday, June 26, 2015

NENO

Rumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Kusudi la Mungu kukuokoa ni ufanye KAZI pamoja naye ili akupe Mema ya Nchi, kwa muda mwingi sana umefanya kazi zako wewe mwenyewe, wakati mwingine umefanya kazi za shetani. Kwa ujumla Mungu amekusudia MEMA kwa kila ALIYEOKOKA na Mema haya yanapatika kwa KUFANYA KAZI. Bila kufanya kazi na Mungu huwezi kula Mema ya Nchi, yaani Utajiri aliouweka Mungu hapa duniani


Thursday, June 18, 2015

MATUKIO MBALIMBALI KITUONI EDEN (Dodoma) 17/June/2015 mchana.

Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, anafika na kukiweka wakfu Kituo cha Efatha Ministry Eden (Dodoma)

 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akifungua Jengo la Kituo cha Efatha Ministry Eden.

 Watumishi wa Efatha Ministry Eden wanampa Zawadi Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, pamoja na Watumishi wengine.


 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira anawabariki Mchungaji na mama Mchungaji Eliya Shoo wa kituo cha Efatha Ministry Eden.


MATUKIO MBALIMBALI KITUONI IHUMWA (Dodoma) 17/June/2015

Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Akiweka wakfu na Kulifungua Kanisa la Kituo kipya cha Efatha Ministry Ihumwa (Dodoma) leo

 Mchungaji (Mch Bigilimana) wa Kituo Kipya cha Efatha Ministry Ihumwa, Dodoma. Baada ya Kituo kuwekwa Wakfu na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira

 Mtume na Nabii akitoa neno la Ubaba kwa wana Efatha kituoni Ihumwa Dodom

Monday, June 8, 2015

MATUKIO KATIKA PICHA JUMAPILI (7/June/2015)

MATUKIO KATIKA PICHA JUMAPILI (7/June/2015) KUHUSU KUPITA MAJUMBANI, MAHOSPITALINI, MAGEREZANI N.K. KUWAOMBEA WAGONJWA NA WENYE SHIDA MBALI MBALI EFATHA MINISTRY ULIMWENGUNI KOTE kama Agizo la Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa Wana Efatha wote Ulimwenguni kote.Wednesday, June 3, 2015

IBADA YA KUPAKWA MAFUTA kwa wana Efatha wote, Kituoni Mwenge Dar es Salaam , Tanzania.

Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mke wake Mama Eliakunda Mwingira, katika Ibada inayoendelea hapa Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam-Tanzania


Kanisani Efatha Mwenge Watumishi wakiwa wamekaa katika viwanja nje ya Kanisa wakiwa na shauku ya kuyaona maajabu ya Mungu siku ya leo, ukumbi wa ndani umejaa


 Watoto wa Sunday school walipokea upako huu pia. / The anointing was also done to the Sunday school children.