Mtu ambaye hali chakula kila siku na kwa wakati atakuwa na afya dhaifu, magonjwa ya kila namna yatamshambulia na kumtesa. Vivyo hivyo mtu asipo soma Neno na Kufanya maombi kila siku huyu atapata utapiamlo wa kiroho, hivyo atasukumwa sukumwa na kuangushwa na dhambi kwa urahisi. Ukitaka kumshinda shetani jitahidi uwe msomaji wa Neno na uwe mwombaji kila siku aloo! Ibilisi atakaa mbali na wewe, dhamiria; ipo nguvu ya kukuwezesha kuwa mwombaji na msomaji wa Neno.

Comments