Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Wednesday, April 29, 2015

EFATHA MINISTRY KILIMANJARO:IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26 APRIL 2015

Uwepo wa UPENDO MKUU WA MUNGU WETU MKUU MWENYE UPENDO KWETU Wanaye, NGUVU YAKE Ikitawala.
(Kwa Wewe ambaye unahitaji Msaada wa Kiroho na upo Moshi au popote pale Kilimanjaro, unaweza piga Simu hii:0655788707)


Tuesday, April 21, 2015

USHUHUDA

Mariam Mwambuta: Kutoka Morogoro nilikuwa naumwa sana natetemeka, nikapata ganzi mwili mzima nikalazwa Hospitali nikiwa nimefumba macho Hospitali nikamwona Mtume na Nabii Josephati Elias Mwingira ametokea mbele yangu akanishika kifuani na mgongoni mwangu sikusikia alicho sema lakini nilisikia sauti ikiniambia umepona. Nilipofika nyumbani nilipata ganzi tena mwili mzima nikazidiwa zaidi, nilikuwa siwezi majirani zangu wakanitoa nje nilikuwa naita Yesu Yesu, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akanitokea tena akaniambia usiogope, baada ya muda kupita nikaona watu wananisukumia kwenye kaburi, mara Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akaja tena akasema nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote za yule adui hakuna kitakacho nishinda , akaja akanichukua na kunivuta mkono wake wa kulia, mwili wangu ulikuwa una dalili zote za kuparalaizi nikaamua kuja Dar es salaam, ndipo nilikutana na Mtumishi wa Mungu Mchungaji Daudi Urio wa Efatha Mwenge akanileta kanisani Efatha, nilipofika kanisani nikakutana na somo katika kitabu cha Yohana 6:1..,linasema mkutano mkuu ulimfuta Yesu kwasababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alikuwa anafundisha somo hilo akasema aliye kuja anaumwa akifika kitandani atapata uponyaji wake, niliamini na kweli nilipo rudi nyumbani nikasema ninalala ili nipate uponyaji nilipo amka nikajikuta nimepona hakuna tena ile hali ya kuparalaizi. Namshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyo nitendea.

Thursday, April 16, 2015

ZONE

Eneo la Tumaini - Kanda ya Mlalakuwa Kituo cha Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania.


Wednesday, April 8, 2015

KAMBI YA VIONGOZI


Mtu ambaye hali chakula kila siku na kwa wakati atakuwa na afya dhaifu, magonjwa ya kila namna yatamshambulia na kumtesa. Vivyo hivyo mtu asipo soma Neno na Kufanya maombi kila siku huyu atapata utapiamlo wa kiroho, hivyo atasukumwa sukumwa na kuangushwa na dhambi kwa urahisi. Ukitaka kumshinda shetani jitahidi uwe msomaji wa Neno na uwe mwombaji kila siku aloo! Ibilisi atakaa mbali na wewe, dhamiria; ipo nguvu ya kukuwezesha kuwa mwombaji na msomaji wa Neno.