Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Friday, October 9, 2015

Chaille Mcneese kutokea Marekani akiwa amesimama baada ya kupokea uponyaji wake Mungu wa Efatha ni muweza wa Yote Amina!!

Breaking News

Haleluuyaah! Mungu wetu anazidi kutenda miujiza watu wanapokea uponyaji wao waliokuwa hawawezi kutembea sasa wanaanza kuinuka. Asante Mungu wetu, Asante Yesu Kristo, Asante Roho Mtakatifu kwa uaminifu wako na upendo wako kwetu. Anza kushukuru Mwana wa Mungu popote ulipo sasa kwa matendo makuu ya BWANA wetu Yesu Kristo. Amini ushapokea uponyaji wako sasa.

SOMO: NGUVU YA UWEPO WA MUNGU MCHUNGAJI MICHAEL OLAWARE Ili uweze kusonga mbele unahitaji uwepo wa Mungu Kutoka 33:12 "Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako." Musa alikuwa mtu mwenye busara, Musa alikuwa na hekima na wewe ukajifunze kutoka kwa Musa, Musa akamwambia Mungu nionyeshe njia si vile ninavyotaka mimi bali vile unavyotaka wewe. Huduma ya Efatha Mungu anakwenda kutupeleka mbele na kutufanya watu wakuu na anavyotupeleka mbele atafanya njia yake. Maombi yako siku zote omba Mungu akuonyeshe njia yako. Penye uwepo wa Mungu panakuwa na mahusiano kati ya mtu na Mungu. Ukiwa na uwepo wa Mungu unakuwa na Roho saba za Mungu, zitakazo kupa mafanikio katika maisha yako. 1wakorinto 9:24"Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate." Kila unachokifanya katika maisha hakikisha unakifanya ili kufanikiwa, iwe ni kwenye ndoa, biashara, huduma, usifanye ili kushindwa bali fanya ili uweze kushinda. Jifunze kujidhibiti mwili wako kwasababu mwili wako ni wathamani na ni hekalu la Roho Mtakatifu usiweke madawa ya kulevya, pombe kwenye mwili wako pia jifunze kutembea kwenye kusudi, Kutembea kwenye mapenzi ya Mungu , kila kitu kinakusudi hapa chini ya jua lazima ujue kusudi lako uwe na malengo na ujijue kwa nini upo hapa, kwa nini upo Efatha, usiishi maisha ya mwingine. Mungu ni mwenye makusudi dumu kwenye makusudi yake. Kwenye biashara zako unahitaji njia ya Bwana. Haijalishi umefankiwa kiasi gani unahitaji uwepo wa Mungu, usithubutu kufanya kitu chochote nje ya uwepo wa Mungu. Zaburi 114:1-5 "Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?" Kama bahari ilivyo kimbia na wana wa Israel wakapita vivyo hivyo kila mazingira magumu yatakavyo kimbia katika maisha yako. Kila kizuizi kitapisha njia chenyewe kwasababu umebeba uwepo wa Bwana na nguvu za shetani ziitaachia. BARAKA ZA UWEPO WA BWANA • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapewa pumziko, • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapata kibali, • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapata ushindi, • Uwepo wa Mungu utakupa ulinzi , • Uwepo wa Mungu unakupa uongozi na mwelekeo • Uwepo wa Bwana unakupa mahitaji. • Ukiwa na uwepo wa Bwana Mungu atakupa afya VITU VITATU VILIVYOSABABISHA MUSA AFURAHIE UWEPO WA BWANA 1. Aliweka usikivu wake wote kwa Mungu ,Mungu anapokuita anataka uwe naye tu, hataki uwe na mengine. Kutoka 3:2 "Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.." 2. Musa alitoa kila alichonacho kwa Mungu kutoka 4:19 "Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa." 3. Musa alikuwa ana tegemewa na alikuwa msikizi, unahitaji kutegemewa na unahuitaji kuwa na uwepo wa Bwana ili uweze kuingia katika nchi ya ahadi.

http://mixlr.com/efatha-ministry/

Kipindi cha maombi ya kipekee, kumbuka leo Mungu anaenda kukutana na matatizo ya kila mmoja wetu, iwe ni magonjwa leo historia za watu zinabadilishwa mahali hapa na popote pale mnapoungana nasi na njia yeyote tegemea, uponyaji wako leo, leo. (Live kusanyiko kuu Precious center kibaha)


Tuesday, October 6, 2015

Its another Day of Rejoicing and praising before the Lord comes lets worship the lord he si worthy of Praise.

Roho ya maarifa haitakaa imtumie mtu mwoga, mvivu na anayependa kulala ovyo, inawatumia ambao wako tayari.Amua kudhubutu hii Roho itakutumia, usiendelee kukaa ulipo, usikubali kufia ulipo nenda kafie mbele kwa mbele, kufa huku unajaribu, kufa huku unadhubutu. Je ukotayari kufa wakati unadhubutu? Mungu hachukii kushindwa anachukia kukata tamaa. Ukishindwa jaribu tena na tena mpaka ushinde.

Kusikia ni muhimu kuliko unavyofikiri ndio maana imeandikwa kama mkisikia na kutii mtakula mema ya nchi.Watu wengi wanatamani kuona miujiza lakini mimi natamani mtu angesikia. Kusikia kunaenda na kupumua maana vyote vinaenda na hewa. Kuona kunaenda na kushika au kugusa. Ukisikia utakuwa watofauti kuliko wenzako, kusikia ndiko kunatofautisha mtu na mtu.

Pichani; Waimbaji wakimwimbia Mungu katika Madhabahu ya Efatha 'Precious center Kibaha', hakika Mungu wetu ni wa Upendo usio na kikomo, aijaza mioyo ya watu wake furaha
Pichani; Mtumishi wa Mungu Mchungaji Michael Olaware kutoka Uingereza akitoa Neno la Mungu katika Kusanyiko kuu ndani ya mji wa Bwana Precious center Kibaha. Jinsi upendo wa Mungu usivyokuwa na ukomo kwa Mwanadam. Hupaswi kukata tamaa, wala kukwazika kisa umetengwa, wala kujihisi upweke na kujiona mwenye dhambi sana ikakufanya kushindwa kumwabudu Yeye. Mungu wetu upendo wake ni endelevu, mwendee kwa maombi huku ukiuachilia Moyo wako kwake maana upendo wake hauna kipimo naye atahuisha nafsi yako

SHUHUDA:Naitwa Ester Emmanuel: Napenda kushukuru Mungu kupitia mchungaji Michael kutoka njee ya nchi, alihubiri akasema kuna mtu anaitwa Ester ana neno aliambiwa na Mungu na asipolifanyia kazi litageuka na kumfanya awe kinyago, nanilimuona Raisi Nyerere akiididimiza chini kuzimu na mimi nikaamrishwa kutamka maneno nikaamuru na pia nikawa nina kutana na Raisi Mwinyi nayeye pia hivyo hivyo na pia nikamkuta pia anadidimiza nchi na mwishowa siku nikamkuta mtu mwishoni akanyanyua ngumi kwa ushuhujaa mkubwa natukawa tumeshinda

SHUHUDA: Kwajina naitwa Hilda Jeremia :Namshukuru Mungu kwasababu niliungua na mafuta nilidondokewa na dumu la mafuta liter 20, nilikuwanaumwa sana kidonda kilikuwa kikubwasana naniliandikiwa kulazwa lakini nilimpigia mama Mchungaji nikamwelezea akaniuliza kuwa mimi nasemaje kuhusu hilo nikamwambia sitalazwa kwakuwa baba Mtume na Nabii alisema hakuna kiongozi kulazwa na mimi ni kalishika neno la Baba nanilipona ndaniya mwezi mmoja

10 things to help you thrive:- 1. Be connected to God. John15. Without God you cannot do anything. For a man to prosper he has to be connected to His source of power. 2. Become planted in the house of God. Those planted in the house of the Lord will flourish. To get profit off the Lords house, you must be planted in the house of the Lord. “Be rooted”. 3. Expose yourself to the right environment. Be careful where you expose yourself. If you have a friend who does not add value to your life, leave him/ her and move on. 4. Discover your true worth. Nobody will tell you what you are worth. The only person with the right to tell what you’re worth is your manufacturer. The word of God is your manual. 5. Nurture your heart and order your words. You must protect your heart. If there is anything that you need to protect more than anything; it’s your heart. 6. Put your light on a candlestick. Isaiah 60 (Arise and shine) Let your life shine 7. Unleash your potential. Everybody has something to offer. God breathed in mans nostrils; and in that breath there is potential that is not discovered. You have the responsibility to stir up your potential. You have what it takes for your prosperity. You have something inside worth discovering. 8. Renew your mind Rom 12. 9. Be filled with the Holy Spirit Pastor Michael UK


Pastor Michael UK: When God calls you, Make sure you say “Yes”, for you do not know who you are saving. You might say “no” and then cause a whole nation to perish.

Friday, October 2, 2015

Monday, September 14, 2015

KUSANYIKO, KUSANYIKO, KUSANYIKO 2015

KUSANYIKO KUU LA BWANA MUNGU WETU MKUU katika Mtembeo wa MUNGU kwa Hao Aliowaridhia USIWE MMOJAWAPO WA KUKOSA,.........Usikose Mwana wa MUNGU, hiki ni Kibali chako cha UPENDO wa MUNGU Kwako, waalike na Wazazi wako, Ndugu zako, Rafiki zako, Jirani zako, Jamaa zako, nao waje Wapokee UPENDO WA MUNGU, Ubarikiwe, YESU Anakupenda.

IBADANI JUMAPILI 14/09/2015

TESTIMONY

Hilary Olomi from Keko Dar es salaam
God has done great things in my life. One day I started coughing and soon I lost consciences and people from my work place were immediately called and I was rushed to Regency Hospital and I was taken to ICU and I was insulted with tubes of oxygen, afterwards when my Pastor heard about it they came to the room and prayed for me took out the tubes and I was able to breathe without the tubes, I thank God for what He did because by now I could be dead I thank God that am still alive.

 SHUHUDA:
Naitwa Stella Bernard, Namshukuru Mungu kwa Matendo yake ya Ajabu kwangu, siku mmoja nilisikia Sauti ikiniita kuja Efatha nilitii ile Sauti nikaja hapa Efatha 2011, nilikuwa nina watoto wawili wa kike sikuwa na mtoto wa kiume nilimwomba Mungu anipe mtoto wa kiume na nilipata mtoto wa kiume. Pia tulikuwa kwenye darasa la Ustawi Mtume na Nabii Josephat Mwingira alikuja na pipi akasema kuna mtu hajawahi kufurahi katika ndoa yake na akila hii pipi ndoa yake itakuwa tamu kama hii pipi, nilisimama nikachukua ile pipi mpaka sasa nina FURAHA, pia Baba akanipa ile pipi na pia nilimwomba Mungu anipe shamba nimepata na pia biashara yangu inaendelea vizuri ninamshukuru MUNGU.

Friday, August 21, 2015

NENO

Efeso 1:3 "Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zote za kiroho mbinguni."
Ukitaka vitu vya ROHONI lazima uwe Mtu wa Ibada, BARAKA zetu zipo katika Roho.

Thursday, July 30, 2015

IMANI


 UNAPOAMINI Yale YASIYOONEKANA Unathibitisha kwamba:-
- MUNGU ni KWELI.
- MUNGU ni HAKIKA.
- MUNGU Yu HAI.

Friday, July 17, 2015

ZIARA YA KITUME NA KINABII YA MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA - Efatha Ministry Kenya.

Ni Wana wa MUNGU wa Efatha Ministry Kenya- Nairobi City Centre Church wakiwa tayari kwa Furaha na Shangwe kwa ajili ya Kumpokea Baba yao wa Kiroho Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, akiwasili Kanisa la Efatha Ministry Kenya- Nairobi City Centre, Wana wa MUNGU wa Efatha Ministry Nairobi City Centre wakimpokea.Mtumishi wa MUNGU Mchungaji Kiongozi Efatha Ministry Tanga (Kulia) Mch. Consolata Kitundu akiwa pamoja na Mume wake, Wakisalimia Wana wa MUNGU wa Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam-Tanzania, Jumapili iliyopita (12/July/2015) Ibadani, Alikuja pamoja na Waimbaji wa Mass Choir Efatha Ministry Tanga.

Wabarikiwe, walihudumu vema

 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwa katika Nyumba ya BWANA Efatha Ministry Kenya- Nairobi City Centre Church.


Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Akiweka WAKFU Nyumba ya BWANA MUNGU Wetu MKUU Efatha Ministry Kenya- Taveta

 Efatha Ministry Kenya- Taveta