Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Thursday, February 20, 2014

DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia jana...Ubarikiwe) ''Tambua kinachokukandamiza! Wahubiri wengine watasema Kwa kuwa imeandikwa, “Hulituma Neno liwaponye, sasa nawaletea Neno la MUNGU, Amesema tena YEYE mwenyewe alichukua madhaifu na masikitiko yetu yote, …” Kwa kupigwa kwake sisi tumepona kwa hiyo pokea uponyaji! Siyo mgonjwa wala hana pepo! Miradi yake haiendelei, au watoto wanafeli shuleni, au ana matatizo katika ndoa hivyo tafuta kwa nini hayo yametokea, tafuta kiini cha tatizo! Mfano. Kuna mtu mmoja aliona maisha yake yameharibika na anakaribia kufa; alikwenda hospitali nyingi lakini hakupona, mwishoe hata hospitali wakakataa kumpokea maana hakutibika. Akaomba sana kwa MUNGU, MUNGU Akamwambia “Siwezi kukuponya mpaka uende kwa Mtumishi wangu uliyemtukana”. Alipokuja kwangu maana alikuwa ametamka maneno magumu sana juu yangu, akatubu kwa machozi; nikasikia HURUMA YA BWANA ndani yangu nikatamka Neno “Laana yako na ikuondoke”! Alikuja kwangu akiwa ameshikiliwa hawezi kutembea, baada ya laana yake kuondoka akatembea mwenyewe na UHAI ukamrudia! Ni vizuri kuelewa kinachokutesa, kumbuka “Watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa” lakini kinachosababisha wakose maarifa ni kwa sababu hawajatambua UKWELI wa tatizo lake. “Utagundua SIRI na hiyo SIRI ndiyo UKWELI wenyewe na huo UKWELI Utakuweka HURU”. Omba! BWANA YESU niingize kwenye chumba cha Uchunguzi (xray); ROHO MTAKATIFU nisogeze kwenye Uchunguzi sasa nipime ee MUNGU Wangu.''

Naibariki Alhamisi Yangu!


Monday, February 17, 2014

DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia jana... darasa ni zuri, JIFUNZE UPATE KUJUA NINI KINAKUSHIKIRIA, NINI KINAKUTESA Ili Uweze KUKISHINDA KATIKA MAISHA YAKO) ''Zaburi 107:17 “Wapumbavu kwa sababu ya ukosaji wao na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa”. Yawezekana unapitia mateso au maumivu ambayo yametokana na maovu yaliyofanyika huko nyuma labda wazazi wako kukosea au wewe mwenyewe kutokutii mambo ambayo MUNGU Amekuagiza. Kwa sababu hiyo unateseka; asili ya makosa siyo shetani. Tuangalie kwa ukaribu watu hawa: - Daudi alipakwa Mafuta lakini alipita njia za kufuatilia mpaka alipofika mahali pa kutukuka. Yusufu naye alipakwa Mafuta na MUNGU na akatamkiwa kabisa atakuwa nani, lakini akapita mapito magumu kabla ya ndoto yake au maono yake kutimia. Jitahidi kufuatilia UKWELI ili uwekwe HURU; wapumbavu kwa sababu ya upumbavu wao hujitesa, Nafsi zao huchukia kila aina ya Chakula. Wameyakaribia malango ya kuzimu. Maanake kila unachokifanya kinakufa na wewe unaona maumivu ya kifo, lakini Biblia inasema, “Wakamlilia BWANA na dhiki zao, naye Akawaponya na tabu zao zote”'' (Itaendelea kesho, Usipitwe Mwana wa MUNGU, ndio muda wako huu wa KUWEKWA HURU).

Naibariki Jumanne Yangu!


Sunday, February 9, 2014

DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea pale lilipoishia wiki iliyopita... KIRI katika UFAHAMU WAKO). MUNGU Akamwambia Nabii amimine mafuta kwa Daudi; familia nzima na jamii yote ikajua huyu ndiye Mfalme. Baada ya sherehehe hawakumtambua tena; akarudi machungani; waliona kama MUNGU Amekosea kwa Daudi kupakwa mafuta. Wengi wetu tumepakwa Mafuta na BWANA kuwa Matajiri wakubwa, Wafanyibiashara wakubwa, Viongozi wakubwa lakini bado mmekaa chini, maana hakuna anayekutambua, lakini saa inakuja ya KUTAMBULIKA KWAKO, sema HALELUYA. Siku moja Daudi akatumwa na babaye awapelekee chakula ndugu zake wakiwa vitani; alipofika kule akakuta wamekumbwa na tatizo linalosumbua Taifa zima. Akajitokeza kupambana na Goliathi na akamshinda! Sasa utamshinda adui yako na Yule anayetesa familia yako na ukoo wako kwa jina la YESU. Sema HALELUYA.

Naibariki Jumatatu yangu!


Haleluya,... YESU wetu ni MZURI, MUNGU wetu ni MZURI, ROHO MTAKATIFU Ni Mzuri, Ibada zimekwisha na Uwepo wa MUNGU wetu MKUU tumeuona, ROHO MTAKATIFU Akitawala, MUNGU MKUU BABA Yetu akimtumia vizuri Mtumishi wake Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira kutupatia Chakula kizuri cha Kiroho,... Oooh Haleluya: "Jinsi gani ya kuishi na kupata KIBALI?... Kuna Protocol/Njia/ Principal/Kanuni/Utaratibu wa Kupata KIBALI. Mfano Treni ina njia yake, bila hiyo reli treni haiwezi kwenda,... kaa kwenye reli, kaa kwenye NJIA husika ili uweze kupata hiko KIBALI, bila kukaa kwenye hiyo Reli au ukikaa nje ya Reli, huwezi kupata KIBALI..."


Thursday, February 6, 2014

Sunday, February 2, 2014

Naibariki Jumatatu Yangu!


YESU Ni MTAMU Jamani kuliko Chakula... Hawa Vijana Pichani nao walipata Neema ya UKOMBOZI, wao walikuwa na HOFU YA KUOA, Wanaogopa KABISA KUOA, Lakini jana Ibadani YESU ALIWAWEKA HURU... JE WEWE Hutaki kuwa HURU kwa hilo linalokutesa?, YESU YUPO ANAKUSUBIRI TU, ila Angalia Muda unakwenda Unyakuo unakaribia.


Dhambi si mpaka utende, Mawazo tu yanaweza kukufanya utende dhambi...: Apostle & Apostle Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Haleluya,... YESU ni MZURI, MUNGU Wetu ni Mzuri, ... Tunamshukuru ROHO MTAKATIFU kwa kutuweka katika Uwepo wa Utukufu wa BWANA MUNGU Wetu leo katika Ibada, Ibada ilikuwa nzuri, BWANA Aliongea nasi vema, Tulikula na Kunywa Chakula kizuri cha Kiroho kutoka Madhabahuni kupitia Mtumishi wake Mkalimani wetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira,... Oooh KIBALI ... ''Unataka kuwa Mtu wa KIBALI, basi kuwa Mtu MKWELI''


Wageni kutoka sehemu mbalimbali walikuja Kumsikiliza na Kumuabudu na Kumsifu na Kumtukuza MUNGU Wa EFATHA. Je Wewe unasubiri nini?