Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Sunday, December 21, 2014

WAMEKUBALI KUWA WANA WA MUNGU NAYE YESU AMEWAPUMZISH. Hongereni kwa kuokoka Roho Mtakatifu awaongoze katika njia zenu zote, Amen



                                                    

SOMO: KAZI ZA YESU.


Yohana 5:17-18 "Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,"
Hoja kubwa ya wayahudi kumkarikia Yesu ni juu ya SABATO, na hadi leo hii kuna ubishani mkubwa juu ya siku ya sabato.
Sabato maana yake ni puumziko, siyo siku, uwe na siku ya kupumzika uiheshimu. Mungu alifanya kazi siku sita ya saba akapumzika hapa haoneshi siku bali alifanya kazi siku sita Mungu akaona kazi ni njema, akapumzika. wewe unapumzika vipi kama hujamaliza kazi? wanadamu wengi leo wanapumzika bila kumaliza kazi
Mwanzo 2:1-2 "Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. "
Mungu alipoona amekamilisha kazi alifurahia akapumzika kwa maana nyingine isingekamilika asinge pumzika, usipumzike kwa sababu ya siku bali kwa sababu umekamilisha.
Mathayo:12 :1-8 “Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Chombo sio kikubwa kama mtumiaji wa chombo, siku siyo muhimu kama wewe. Anamaanisha nini anaposema mwana wa adamu anaondoka katika uungu anahusisha ubinadamu wetu. Sabato imewekwa kwa ajili ya mwanadamu, mapumziko hayahusu siku tu bali mapumziko ya kweli kutoka katika vifungo mbalimbali
Mathayo 11;28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”
Mimi ndiye Bwana wa sabato “mimi bwana wa mapumziko” yeye ndiye atupaye pumziko, hazungumzii siku. Siku, miaka na nyakati zipo kwetu ili ujue yakupasayo kutenda kwamba ni wakati wa kusoma, kuoa.Siku haipumzishi bali mtu anapumzika na anayempumzisha mtu ni Bwana wa napumziko Yesu pekee, hakuna msaada katika siku.
Yohana 5:39 "Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia."
Wewe nabaki kuchunguza chunguza maandiko katika biblia ukizani huko kuna mzima, chunguza sana Yesu asomewi Yesu anaaminiwa, kuna watu wanaisomea biblia miaka mingi hadi vipara lakini hawana Roho Mtakatifu na hawawezi kuombea wagonjwa.
Usifungwe na siku maana kwa Mungu wetu kila siku ni siku ya Mungu, wewe ndiye unayechagua lini nipumzike. Kumbuka pumziko la kweli lipo kwa Bwana Yesu. Yesu alipomaliza kazi aliacha maagizo kwa watumishi aliowaweka ila wafanye na wawaelekeze watu wafanye kile Yesu amekusudia wafanye ikiwa ni pamoja na kuwapumzisha wenye mateso na vifungo mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ma mateso mbalimbali.
Leo hii tunashuhudia watu wakipata mapumziko katika ndoa zao, afya zao, uchumi wao, Walio katika kristo ni marufuku kupita katika mateso, maana unaye apumzishaye. Hakuna maisha ya raha na amani kama ya WOKOVU.

Shuhuda

EFATHA MASS CHOIR WAKITOA SHUKURANI KWA MUNGU WAO Tunamshukuru Mungu kwa kutuokoa kutoka dhambini tulipokuwa akatuheshimisha kwa kuona tunafaa kuwa vyombo vya sifa ni kwa neema tu.



SHUHUDA IBADA ZA LEO


Mch Merania Irengo wa Eneo la Amani
Anamshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kutenda kazi karibu na mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Pia namshukuru Mungu kwa sababu kuna siku mtu mtumishi wa Mungu alisema kila mtu ambaye watoto wao wako nchi za nje warudi nyumbani ili watumikie taifa lao, nikaingia katika maombi Mungu ni mwema mwaka jana mwanangu aliye zamia marekani alirudi nyumbani na mwingine wa kike amerudi, mmoja aliyeolewa Uganda naye karibini atakuja nyumbani na mumewe, kwa kweli namshukuru Mungu
Kwenye kusanyiko la mwaka huu 2014 Mtumishi wa Mungu alisema kuna watu wanaenda kupokea zawadi, nakumbuka tarehe 14 mwezi huu wa kumi na mbili mshirika wangu mama mmoja akanipigia simu kuuliza kama nipo nyumbani nika mwambia nipo baada ya dakika 45 alikuja akanipa gari funguo kadi ya gari na kila kitu akaniambia amenipa gari ili inisaidie katika majukumu yangu ya kichungaji. Hatimaye na mimi namiliki gari kweli Mungu amenishangaza, namshukuru sana Mungu. Nataka ujue changamoto hazina mchungaji kila mtu anachangamoto anazopita nazo lakini kama unaye Mungu atafanya njia kwa ajili yako. Pili neno kutoka kwa mtumishi wa Mungu lina nguvu ya kusababisha jambo litokee. Amen

Saturday, December 13, 2014

Kumpokea Yesu!

Baadhi ya waliotoka Kumpokea Yesu katika Maisha yao, Mungu wetu ni Mzuri...







Ushuhuda!

Alex
1.       Amepata Shahada ya Kwanza ya Uandishi wa Habari…na anaweza kujiunga na masters moja kwa moja

Pia ana mshukuru mungu kwa Kumaliza madarasa ya Kukulia wokovu.anamfurahia Mungu wake Amen!

Kamata Neno la Madhabahuni utakuwa Heri mwana wa Mungu!



Njiambatanishe na Yesu.

Ukijiambatanisha na Yesu magonjwa yanakuwa mbali nawe, kila aina ya TABU inakaa mbali nawe.
Kama uko katika Huduma furani mahali unapoabudu, jiambatanishe na madhabahu ya mahali hapo,usiangalie kushoto wala kulia, usiwe na mawenge,Tulia mahali ulipo, uwe na Adabu na sehemu unapoabudu, na kuhakikishia utamwona Mungu.

Njoo Ibadani ukutane na Jibu lako.

Tengeneza Hoja mbele Za Bwana, hakika utakutana na majibu ya Maisha yako.
Roho yako iambatane na Roho ya Yesu, ndio maana tukimwita Yesu anaonekana.kwa sababu tumeunganishwa naye katika Roho.
Mfano.
Elisha tunaona ameunganishwa na Elijah, Alitazama juu akauliza Mungu wa Elijah yuko wapi.na alipoiweka ile jozi yake kukawa Njia.
Tujiambatanishe na wapakwa mafuta wa Mungu.wale Mungu aliowaamini. akawapa nguvu kwa ajili ya utukufu wa jina lake.
Mfano Mwingine 1samweli 18:
Daudi na Yonadhani, Roho wa Yonathani akaambatana na ya Daudi.



Neno na Mchungaji Aimana!

Mchungaji Aimana:
Tuendelee Na Tadhimini.
Umetembea Na Huduma ya Efatha kwa muda gani.. Harafu umemuona Mungu Kwa Kiasi Gani.
Usemezane na Moyo iabiye Nafsi yako.na hakika huhitaji kuwekewa Mkono na Mtu.
Unaweza ukatembea na Huduma Furani lakini usikutane na yesu.
Tupate live audio streaming www.mixlr.com/efatha

Don George Amemuona Bwana Kwa namna ya kipekee!

Don George 
Zaburi 20:7 Nimekuja nchini mwaka 1991 nilikutana na Mtumishi wa Mungu Mtume na nabii Elias Mwingira mwaka 2001
Nilikuwa katika misukosuko mingi sana lakini baada ya kukutana na Apostle nimefunguliwa mambo mengi na pia Mama Apostle alikuwa akinisaidia mambo Mengi.
Nikaoka, Nikaoa Huku Efatha.
2012 niliombewa Mke wangu alikuwa anatakiwa kujifungua tarehe 9 November,Ilipita wiki mbili hajajifungua na Njia Ilijifunga, aliambiwa ajifungue kwa Operation lakini baada ya kumpigia APOSTLE alitamka neno hatojifungua kwa operation atajifungua salama.
Siku ya operation Mtoto alitokea wodini na madokta walishangaa haijawahi kutokea katika Hospitali hiyo Mzazi kujifungulia wodini.wakamuliiza wewe ni mhindi je Umeokoka? akasema ndio nimeokoka.Mke wangu akajifungua mtoto wa kiume. Namshukuru kwa Maombi yake Apostle na Mungu wangu sana.Amen.


Jumapili Tarehe 14 December! Ni neema Ya kipekee kuwa Mbele za Bwana, Karibu mwana Mungu! Wewe Uliye mbali tupate live kwenye www.mixlr.com/efatha.

Saturday, December 6, 2014

Neno La leo na Mchungaji Aimana.

NENO LA JUMAPILI NA MTUMISHI WA MUNGU AIMANA DOMINIC

Mwanzo 4:7a. kama ukitenda vyema hutapata kibari? angalia ushuhuda wa huyu dada kwamba aliona hana haja ya kusema  atafauru lakini alijifuta mwenyewe. mangapi yametamkwa kwenye madhabahu ya Mungu lakini kwako hayajatimia kwa sababu tunashindwa kujitakia mema? Kama yale yaliyo tamkwa kwangu na tungeyatakia mema yale tungekua mbali. Nipo hapa kukukumbusha achana na zile nyaraka ambazo zimeandikwa na wanadamu angalia nyaraka za kwenye Bibilia.

Tukiamua kubadilika tukabeba nyaraka za madhabahuni tutakua na ushuhuda kabla mwaka haujaisha. Nenda katafute Yule mtu mwenye dhambi anaye jiuza anaye piga miziki disko mlete kwa Yesu wapo tayari wanatusubiri tuwaendee. 


Umepakwa mafuta ya Roho Mtakatifu je unayatendea mema yale mafuta? kwenye kamati haupo ivi hayo mafuta yako unayatendea mema. Sababisha mchungaji wako wa kituo afurahi angalia unaweza kufanya nini hemani mwa bwana fanya usababishe Yesu afurahi. 

Unatupata live kwenye www.mixlr.com/efatha audio live streaming...!!


Je ulionao karibu wanafurahi kwa sababu yako?

Mungu anafurahi kwa sababu yako, kazi ulioitiwa kuifanya unaifanya kwa uaminifu.
Ebu tufanyike furaha kwa viongozi wetu na Mungu wetu.



Neno na Mchungaji Aimana:TAFAKARI uone ni nini iyo haujafanya Kafanye vizuri.

Mwanzo 4:7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko inakuotea malangoni, nayo inakutamani wewe walakini yakupasa ushinde.
Tutamani sana kutenda mema,Kukaa katika kumtumainia Mungu tutapata kuwa na shuhuda.
Ukiamua kubadilika inawezekana kabisa, ukitamani lile linalokusumbua liondoka litaondoka tu, pale ikiamua kusima na Mungu ambaye ni msaada wetu.



Sifa kwa Bwana.wetu Mungu baba...Yote alimaliza pale msalabani.




SHUHUDA:

Dorcas Jackson
Kutoka Eneo la Upendo.
Ushuhuda

Dorcas Jakson kutoka upendo napendA kumshukuru Mungu ilikuwa mwaka 2008 nimemaliza form four sikupata credit moja na nilikata tama katika ule mwaka nilipokuwa kwenye ibada jumapili moja mtumishi wa mungu alitangaza kwamba kuna binti anataka kufika chuo kikuu baada ya mwaka ule nilipata niliendelea na advance level na nilipata division one katika wasichana wote tulikuwa wawili tu tilofaulu. ulipofika mwaka wa pili ilikuwa na changamoto kubwa nilipokuwa najiandaa field ilikuwa mwezi wa 9 nilipata changamoto sana kwani kila Mwalimu alikuwa ananitaka nilipata bahati ya mtumishi wa mungu akasema nitakuwa wakwanza na ninaomba kwaajiri yake akasema bwana yesu ninaomba nimwongoze kwa mwanafunzi huyu na baada ya maombi hayo Mtumishi wa Mungu mimi nilikuwa nakubarika na katika watu

wanaotakiwa kupeleka repoti nilikua peke yangu na kuna wanafunzi wako wengi lakini mimi niliona ni kibari kwa mungu alinitetea lakini Yule mwalimu aliendelea kuniambia maneno ya ajabu lakini ninamshukuru Mungu kwani  na katika ile ripoti nilipewa A. 

VIJANA VIJANA.....MNAKUMBUSHWA KAMBI YA VIJANA TAREHE 18 MWEZI HUU KIJANA KARIBU SANA UKAPOKEE MBARAKA WAKO.


TUPO LIVE SASA tupate katika mtandao wetu, www.mixlr.com/efatha ubarikiwe