SHUHUDA: Walikaa MIAKA 15 bila kupata Mtoto -Shuhuda hii ilikuwa jana USIKU. Mwana wa MUNGU Mama huyu ni Mwenyeji wa kutoka Botswana, Mume wake ni Daktari Bingwa huko Botswana, na wote ni wa kutoka Botswana. Walikaa MIAKA 15 bila kupata Mtoto, WALIZUNGUKA Hospitali mbalimbali KUBWA na NDOGO lakini hawakufanikiwa kupata Mtoto (ingawa pia Mume wake alikuwa Daktari Bingwa), Wakaenda katika sehemu mbalimbali za MAOMBI huko kwao Botswana na sehemu zingine, lakini hawakufanikiwa. Siku moja walikutana na Mtu mmoja huko Botswana, akawaambia kuwa “MUENDE TANZANIA na Mkamuone Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Nanyi mtapokea Baraka Zawadi ya Mtoto”. Wakatii wakaja Tanzania, wakamtafuta Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, wakaambiwa yuko Kibaha Precious Centre, basi wakajieleza kuwa wao wametoka Botswana na Wameelekezwa waje kumuona Mtumishi wa MUNGU. Mtumishi wa MUNGU akaambiwa kuwa kuna Wageni toka Botswana wanataka Kukuona, Mtumishi wa MUNGUAkasema “Wana Appointment na Mimi? Hakuna” Lakini Akaagiza Waruhusu waje. Wakaja Kibaha, wakakutana na Mtumishi wa MUNGU, Wageni hawa wakamwambia Mtumishi wa MUNGU, kuwa “Baba sisi tuna shida ya kupata Mtoto, Tumekaa Miaka kumi na tano (15), tunaomba UTUOMBEE”. Hawa Wageni baada ya kumwambia Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii, wakawa wanasubiri KUOMBEWA, …(HAIKUWA HIVYO: Badala ya KUOMBEWA Mtumishi wa MUNGU Akawaambia kuwa NENDENI kwenu Botswana Mkarekebishe Mambo yenu yaani MKAPATANE Na WALE MLIOWAKOSEA (kwa Upande wa Mume) na MKE akaende kufuta Maneno aliyokuwa ameyatamka akiwa Mdogo kwa Wazazi wake “Kuwa YEYE Hatakuja KUOLEWA na wala HATAKUJA KUZAA Mtoto” Hawa WAGENI Wakashangaa Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira AMEJUAJE Hayo yote? Wakamuuliza “UMEJUAJE?” Mtumishi wa MUNGU Akaawambia kuwa MKISHAFANYA HAYO, MRUDI TENA HUKU TANZANIA. Wageni hawa Wakarudi kwao Botswana bila KUOMBEWA CHOCHOTE, Wakaenda na WAKAFANYA Kama Mtumishi wa MUNGU ALIVYOWAAGIZA KUFANYA. Baadae Mwaka jana 2013 Mwezi wa Tatu (March) wakarudi tena Tanzania kuja kumuona Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Baada ya kufika, Baba Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii AKAONA NI KWELI WAMEFANYA KAMA ALIVYOWAAGIZA KUFANYA. Basi AKAWAAMBIA “ Mwaka huu (2013) MWEZI WA SABA MAMA Huyu ATAPATA UJAUZITO, … . (Hakuwaombea bali ALITAMKA NENO KWAO) OOOOoooh Haleluya “MUNGU Hasemi UONGO Kamwe”, NENO la Mtumishi wake KWELI LILIKUJA KUTIMIA, MUNGU wetu MKUU BABA Yetu YU HAI, YEYE Ni MWANZO na MWISHO, ALFA na OMEGA katika YESU KRISTO BWANA wetu ndani ya ROHO MTAKATIFU. Kweli huyu Mama ilipofika Mwezi wa Saba (Mwaka jana 2013) alishika Mimba, Alipata UJAUZITO kama Mtumishi wa MUNGU Alivyowaambia. Na leo ndio WAKEKUJA katika KUSANYIKO KUU HILI LA BWANA 2014, Kuja KUMSHUKURU MUNGU BABA Yetu kwa UPENDO MKUU MUNGU Aliyompa YEYE katika NDOA YAKE. LEO Ana Mtoto huyo Pichani unayemuona (anaitwa Timotheo) BAADA YA MIAKA KUMI NA TANO BILA MTOTO. HUYO ndiye MUNGU tunaye MUABUDU na KUMFUATA, HUYO ndiye YESU KRISTO BWANA wetu TUNAYEMUAMINI katika UWEPO wa ROHO MTAKATIFU Wetu. MUNGU BABA YETU Anasema “Yeremia 32:27 Tazama mimi ni BWANA MUNGU wa wote wenye mwili; Je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?”


Comments