Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Wednesday, June 25, 2014

SOMO: KUSIKIA NA KUONA (Linaendelea tulipoishia) IBADA: Jumapili 22/June/2014 Mikutano ya YESU mingi ilifanyika juu ya Milima na kando ya Bahari. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, Mathayo 13:3-8 “Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua na kwa kuwa hazikuwa na mizizi zikanyauka, Nyingine zikaanguka penye miiba, ile miiba ikazisonga, nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini”. Sasa hizi karibu na njia ndege wakazila, hapa hasara, Ya pili zikaanguka kwenye miamba hizi sio hasara tu ziliota, lakini kutokana na udongo kukosa kina na kuwa hazina mizizi zikanyauka, Mbegu ya tatu zikaanguka kwenye miiba, ile miiba ikamea na kuzisonga, kundi la nne zikaanguka kwenye udongo mzuri zikazaa moja mia, moja sitini na moja thelathini, mwenye sikio na asikie. Katika mahubiri ya YESU ambaye ni MHUBIRI MKUU, ni mahali hapa ndipo ameweka mkazo katika KUSIKIA na KUONA, maeneo mengine amekazia IMANI. Kuna Waliojaliwa na Wasiojaliwa, kwa hiyo Kusikia na Kuona kunahitaji KIBALI cha MUNGU, hii pia inanipa Mimi msukumo ya kusema uwe na KIBALI, haiwezekani Mlokole mwenye Kibali cha MUNGU amekaa Miaka mitano bado amechoka, haiwezekani kwa kuwa MUNGU Ninayemtumikia ni MUNGU wa Neema, AINUAYE, ANAYEHUISHA, “Inakuwaje miaka hiyo yote haupigi hatua?” Hapana lazima kuna tatizo, ndipo Mhubiri Kiongozi YESU amewajalia ninyi kuzijua SIRI.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Photo: SOMO: KUSIKIA NA KUONA (Linaendelea tulipoishia)
IBADA: Jumapili 22/June/2014

Mikutano ya YESU mingi ilifanyika juu ya Milima na kando ya Bahari. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, Mathayo 13:3-8 “Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua na kwa kuwa hazikuwa na mizizi zikanyauka, Nyingine zikaanguka penye miiba,  ile miiba ikazisonga, nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini”. Sasa hizi karibu na njia ndege wakazila, hapa hasara, Ya pili zikaanguka kwenye miamba  hizi sio hasara tu ziliota, lakini kutokana na  udongo kukosa kina na kuwa hazina mizizi zikanyauka, Mbegu ya tatu zikaanguka kwenye miiba, ile miiba ikamea na kuzisonga,  kundi la nne zikaanguka kwenye udongo mzuri zikazaa moja mia, moja sitini na moja thelathini, mwenye sikio na asikie. Katika mahubiri ya YESU ambaye ni MHUBIRI MKUU, ni mahali hapa ndipo ameweka mkazo katika KUSIKIA na KUONA, maeneo mengine amekazia IMANI. Kuna Waliojaliwa na Wasiojaliwa, kwa hiyo Kusikia na Kuona kunahitaji KIBALI cha MUNGU, hii pia inanipa Mimi msukumo ya kusema uwe na KIBALI, haiwezekani Mlokole mwenye Kibali cha MUNGU amekaa Miaka mitano bado amechoka, haiwezekani kwa kuwa MUNGU Ninayemtumikia ni MUNGU wa Neema, AINUAYE, ANAYEHUISHA, “Inakuwaje  miaka hiyo yote  haupigi hatua?” Hapana lazima kuna tatizo, ndipo Mhubiri Kiongozi YESU amewajalia ninyi kuzijua SIRI.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Naibariki Alhamisi Yangu!

Tuesday, June 24, 2014

EFATHA MINISTRY - Kenya: Mchungaji Kiongozi wa Efatha Ministry Kenya Mch. Betson Kikoti pichani akiongoza Ibada leo jioni (tarehe 24/6/2014) katika Kanisa la Mjini Nairobi City Centre (Efatha Ministry Nairobi City Centre)... Je na wewe Uliweza kuhudhuria Ibada ya Zone? BWANA Awe nanyi wana wa MUNGU wana Efatha Kenya, na MUNGU wetu MKUU, MUNGU wa Efatha akawalinde na kuwa pamoja nanyi. (10 photos)
Naibariki Jumatano Yangu!

Photo: Naibariki Jumatano yangu...

IMANI

Imani chanzo chake ni kusikia, kusikia nini? Kusikia HABARI NJEMA. Sasa si kila Muhubiri amebeba Habari Njema, narudia, YESU alisema Neno la ajabu sana, alisema, “Mtawatambua kwa matendo yao”. Si kila Muhubiri amebeba Habari Njema, Si kila ...Muhubiri ana Habari njema, TAFADHALI uliweke hilo.
Paulo kwa kusisitiza hilo anasema, “Wengine wanahubiri wakilenga kuongeza maumivu katika Utumishi wangu lakini hata hivyo Injili inahubiriwa”. Kwa hiyo watakuwepo wahubiri ambao kazi yao si kujenga Imani.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Monday, June 23, 2014

A person wasting time is one without wisdom, for wisdom helps you to utilize your time. Time always reduces, and this either makes you attain wealth or poverty.: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Toa kwanza habari mbaya kichwani pako, ndipo HABARI NJEMA zinaweza kupata nafasi, Toa kwanza Habari mbaya ulizonazo ndipo Habari Njema zinaweza kupata nafasi.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Naibariki Jumanne Yangu!

IBADA: Jumapili 22/June/2014

SOMO: KUSIKIA NA KUONA

Mithali 22:12 [sikio lisikialo na jicho lionalo…] Anaposema “Sikio lisikialo na jicho lionalo” maana yake lipo sikio lisilosikia na jicho lisiloona, anasema BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili yaani sikio na jicho, ukiona na kusikia maana yake una KIBALI cha MUNGU, ndiyo maana katika kitabu changu nimeandika “Mtembeo wa Mungu kwa hao aliowalidhia”, katika maisha ya mwanadamu ukipungukiwa haya mambo mawili ya msingi ni hatari sana, ni heri mwanadamu asiongee na akaona lakini haiwezekani asikie na aone halafu asiongee, ukiona mtu hawezi kuongea tatizo lipo katika sikio na macho, ukiona anashindwa kutembea, tatizo lipo katika macho. Siri ya Uumbaji ipo katika KUONA na KUSIKIA, ili kitu kitokee lazima USIKIE, ndio maana katika Uumbaji wake MUNGU, ALITAMKA na vikatokea, Alipomaliza kuumba akavileta kwa Adamu ili avipe majina sawasawa na Adamu alivyoona na kuviita majina ndiyo ilivyo hata leo, hapa MUNGU alitaka kuona kuwa huyu mtu kama AMEONA na KUELEWA, kwa hiyo Kuona na Kutamka vinaenda pamoja, Kuona na Kusikia vinasababisha UONGEE. Katika kuishi kwako kama huoni na husikii, na kwambia utakufa mapema, maana utasindikiza wenzio mwisho utakata tamaa na kufa mapema. Ukiwa Afrika unaweza kuishi vizuri na ukiwa Marekani unaweza kuishi vizuri, kinachosababisha ni kusikia na kuona, ukienda Marekani kama HUONI hutapata kitu, Ukiwa mpumbavu hata uende wapi bado utakuwa mpumbavu, tatizo lipo katika Kusikia na Kuona. : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Tutaendelea kuwaletea Somo hili, Omba ROHO MTAKATIFU MUNGU Akufunulie ili Uweze KUSIKIA na KUONA kutoka katika Somo hili, Ubarikiwe.)


Monday, June 16, 2014

SOMO LA JUMAPILI Jana (15/6/2014):

MAAMUZI yanayoleta Mabadiliko na Uponyaji; hapa tunahitaji kumsikiliza ROHO wa Shauri: Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira.

Inawezekana mambo yanaokuzunguka yamekufanya ufike mahali pa kukata tamaa, umeenda huku na huko kutafuta msaada lakini hujafanikiwa, na wengine wamekung’ong’a, lakini leo YESU anakualika umpe mzigo wako ili AKUPUMZISHE, inawezekana umemuomba mtu akuombee lakini mtu huyo naye hana majibu, anakuombea kwa MUNGU lakini shida yako jinsi anavyoijua si kama unavyoijua wewe mwenyewe, usitumie njia ndefu nenda mwenyewe kwa MUNGU jieleze, maana anasema katika Neno lake “Njooni ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo nitawapumzisha”. Ukimuendea WEWE mwenyewe, Mtumishi wake atapewa AGIZO la Kukusaidia. Kile kilio chako mbele za MUNGU kwa Uaminifu, utaona Mtumishi anataka kufunga ibada atasema kuna mtu hapa ana shida hii na hii, ni kwa sababu ya kilio chako kwa MUNGU wako, kilio chako mbele za MUNGU kinasababisha MUNGU anainua Mtu mwingine kwa ajiri yako, anaamrishwa nenda kamsaidie mtu fulani. Ili Mtumishi aweze kukusaidia ni lazima MUNGU asikie kilio chako....(Somo hili litaendelea, ni Zuri sana Mwana wa MUNGU, tutakuwa tunakupatia sehemu kwa sehemu, ili uweze kula chakula hiki vizuri zaidi, Ubarikiwe)
 
 

Thursday, June 12, 2014

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."

ROHO ya Maarifa inakupa uwezo wa kubuni, kuumba na kupambanua roho, kwa sababu MUNGU wetu ni Mumbaji. Kazi ya ROHO wa Maarifa ni kukuwezesha ili ufikie mahali pa kukusudia neno, nalo lithibitike kwako, Anakusaidia wewe uweze kuwaza jambo ambalo litakuwa la faida kwako, Anakusukumia WAZO, MAONO, MAFUNUO, yote yanafunuliwa na huyu ROHO wa Maarifa, kazi yake kufunua mambo ya siri yaliyofichika, ROHO wa Maarifa anapatikana kwa wachache mpaka uweze kumsikiliza ROHO wa Shauri. ROHO wa Maarifa anaweza kukuongoza mpaka ukafika mahali pa kujua mambo makubwa. Ukitamka neno litathibitika hivyo ndiyo maana zinatangulia ROHO hizi zingine kufanya kazi na wewe, kisha hizi za hatari zinakuwa za mwisho (ROHO wa Shauri, Uweza, Maarifa, Kumcha BWANA) : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Naibariki Ijumaa Yangu!

Tuesday, June 10, 2014

PRAYERS FOR THE 3 MAJOR PARTS - Your prayers must have answers. - Your prayers must be victorious. (These prayers must make you a victor forever and you can also pray for victory in another area Psalm 65:2-4.) - Prayers that make you have the ability to receive. A prayer is the communication between you and heaven, Hebrews 4:16 (Therefore let us approach the throne of grace with boldness, so that we may receive mercy and find grace to help us at the proper time.) Prayers must give you answers, victory and ability to receive. You get courage when you forgive others. When you continue to pray, your foes are taken away from you and good people are brought close to you. When an intercessor prays, his/ her evils are removed by way of prayer. When you welcome them they become close to you. James 4:12. When you pray, things move. In prayers GOD has given us something to recognize HIM. Matthew 6:9. Through this prayer GOD shows us: -We have a FATHER in heaven Who when we talk to, our prayers are answered. -PRAISE HIS NAME: Train yourself day by day, to praise HIM for it is by this you get a chance to get close to HIM Psalm 16:11 -ABOUT A KING: You have to recognize HIS kingdom as the greatest among other kingdoms. It is by this your prayers shall have answers. -ABOUT HIS LOVE: When you worship you have to understand what GOD wants with you. 1John 5:14-15 :Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Naibariki Jumatano Yangu!

Photo: Naibariki Jumatano yangu...

Naibariki Jumanne Yangu!

Monday, June 9, 2014

IBADA YA JUMAPILI 8/6/2014

Haleluya,... Pichani; Ibada ya Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania

 Kwaya za Mass Choir pamoja na Chipukizi, zikimwinua BWANA MUNGU wetu MKUU

 Pichani: Ukombozi na Uponyaji Ibadani leo

Wana wa MUNGU katika Kituo Kipya cha Efatha Ministry Mkwajuni-Chunya, wakiwa katika Furaha na Amani tele baada ya kumalizika Ibada ya leo Jumapili, kituoni hapo.

Hakika tutafika Duniani kote, kufanya Kazi na Kutangaza Habari Njema za BWANA... wetu YESU KRISTO na kuliandaa Kanisa tayari kwa Unyakuo.

EFATHA "Funguka''; UPONYAJI na UKOMBOZI, Haleluya Tutaifanya Kazi ya BWANA wetu YESU KRISTO kila mahali, Tunampenda YESU wetu, Tunampenda MUNGU wetu na BABA yetu, tuko tayari.
  


Monday, June 2, 2014

Naibariki Jumanne Yangu!

Zawadi ya watoto.

Haleluya...Tumepata Zawadi ya Watoto wawili kwa Siku ya leo hii Jumamosi, siku yetu ya Mwisho ya Mwezi wa Maombi na Kufunga, Watoto hawa wote wamezaliwa Madhabahuni hapa Kanisani Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania. Tunamshukuru MUNGU wetu MKUU, YEYE BABA YETU ANATUPENDA SANA kwa YESU KRISTO BWANA.


Wana wa MUNGU wakishukuru Madhabahuni kwa KIBALI, na wengine wakishuka chini kwa ajili ya kuomba KIBALI.
Wana wa MUNGU wakiwa mbele za BWANA MUNGU wetu MKUU


Sunday, June 1, 2014

aleluya, kwa kweli tunamshukuru MUNGU wetu MKUU BABA yetu katika YESU KRISTO BWANA wetu na katika Uwepo wa ROHO MTAKATIFU kwa Neema, Rehema,Baraka na UPENDO MKUU aliotupatia katika Mwezi wetu wa Kufunga na Kuomba, Mwezi wa Tano (May/2014) uliopita, kweli tuliona MAMBO MAKUU, Tuliona KIBALI, Oooh MUNGU Anatupenda WANAWE, Nasi tutazidi KUMPENDA na KUMPENDA na KUMPENDA na tutampinga na kumkataa shetani ibilisi mlaaniwa. Sasa Wana wa MUNGU kazi ni mbele kwa mbele " KUMPINGA shetani na KUMKATAA, kwani tunayo NGUVU na MAMLAKA ya Kukanyaga nyoka na ng'e na kushinda nguvu zote za yule adui; na wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kutudhuru" Usicheze naye, usicheke naye, atakuabisha, atakurudisha nyuma, atakupotezea muda, atakufanya uchelewe kupokea Matazimio yako; Kuwa na HASIRA YA MUNGU, kuwa na WIVU WA MUNGU, Usirudi Nyuma tena Mwana wa MUNGU. Na wewe ambaye bado hujampokea YESU, njoo sasa achana na Maisha ya Mateso, ya kuburudhwa na shetani, anakufanya Uteseke, uhangaike, usiwe na Amani na Furaha katika maisha yako, matatizo mateso hayaondoki kwako, magonjwa, misiba... AMUA SASA, Umpokee YESU, Njoo kwa YESU sasa. Mbarikiwe.

SHUHUDA: Haristidesi John Kiria anatokea eneo la Tumaini, aliamua kuja na kusimama mbele ya Wana wa MUNGU kuja kutoa Shukrani kwa MUNGU wetu MKUU kwa Baraka na Neema alimzojalia kupata WOKOVU kuja Efatha. Anasema "Siku moja nilikuwa nyumbani naangalia Television channel ya Efatha -TRENET, mara nikamuona Baba Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii anahubiri, kwa kweli nilipenda Mahubiri yake, yaani yalikuwa tofauti kabisa kabisa na Watumishi wengine, yalikuwa na Ujasiri na Nguvu na Imani na Upendo, NIKAMPENDA sana Baba Mtume na Nabii, nikatamani kuja Efatha kwani niliona kuna kitu cha Tofauti mahali hapa, basi sikuchukua muda mrefu nikaja Efatha ilikuwa Mwaka jana. Sasa baada ya kufika hapa nikapata Chakula kizuri cha Kiroho, mojawapo kilikuwa ni kuhusu MALIMBUKO, Ujue sisi Wachaga kule kwetu, Watoto wakizaliwa tu huwa tunawakabidhi kwenye mizimu, kuna madhabahu kule ambapo huwa unachukua Mbuzi na kumchinja, halafu ile damu unaimwaga kwenye, halafu nywele za mtoto unazifukia kwenye migomba; Lakini baada ya kupata UFAHAMU nikasema mimi Mwanangu sitamtoa kwenye mizimu, bali nitamtolea MUNGU, kwa hiyo nimekuja leo KUMTOLEA MUNGU MALIMBUKO".Naibariki Jumatatu Yangu!

Photo: Naibariki Jumatatu yangu...