Kila eneo katika maisha ya mwanadamu linahitaji aina fulani ya tabia na taratibu zinazowezesha kumpatia Ushindi. Tabia ni roho kamili inayoweza kumsababishia mtu kufanikiwa au kushindwa katika maisha ya Kiroho na ya Kimwili. Ili ufanikiwe ni muhimu kujenga TABIA SAHIHI na KUZINGATIA TARATIBU zinazotakiwa. Mfano kuna tabia na utaratibu wa kufanya biashara, kufanya kazi ofisini, kuishi katika ndoa, kutenda kazi ya MUNGU, kuwa WACHA-MUNGU na kadhalika. Ili mtu aweze kupata Baraka alizokusudiwa na MUNGU inambidi kujenga TABIA NZURI kwa JUHUDI ZOTE huku akitenda MATENDO yenye KUMPENDEZA MUNGU na Wanadamu. (a) TABIA NI NINI Tabia ni maumbile yaliyo katika viumbe hai ambayo yanaviwezesha kukabiliana na mazingira yanayovizunguka. Maumbile hayo yanajidhihirisha zaidi ndani ya mwanadamu na wanyama katika matendo na mienendo yao. Mwili wa kiumbe hicho ndio unaoonyesha tabia hizi. Wanyama wana tabia za maumbile ya kinyama na wanadamu wana tabia za maumbile ya kibinadamu. Mfano: Simba ana tabia ya kunyemelea mawindo yake, Fisi ana tabia ya kula mizoga, Kuku ana tabia ya kupiga kele akishataga na Mbwa ana tabia ya kubweka akiona kitu ambacho hajazoea. Tabia ni roho kamili inayoweza kumsababisha mtu kufanikiwa au kushindwa katika maisha ya kiroho na ya kimwili pia. Hivyo ni muhimu sana kuona kuwa tabia nzuri ya mtu inajengeka mapema utotoni ili maisha yake ya baadae yasije kuwa mabaya. :Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Itaendelea kesho mwana wa MUNGU, USIKOSE na USIPITWE)

Comments