Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Sunday, December 21, 2014

WAMEKUBALI KUWA WANA WA MUNGU NAYE YESU AMEWAPUMZISH. Hongereni kwa kuokoka Roho Mtakatifu awaongoze katika njia zenu zote, Amen                                                    

SOMO: KAZI ZA YESU.


Yohana 5:17-18 "Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,"
Hoja kubwa ya wayahudi kumkarikia Yesu ni juu ya SABATO, na hadi leo hii kuna ubishani mkubwa juu ya siku ya sabato.
Sabato maana yake ni puumziko, siyo siku, uwe na siku ya kupumzika uiheshimu. Mungu alifanya kazi siku sita ya saba akapumzika hapa haoneshi siku bali alifanya kazi siku sita Mungu akaona kazi ni njema, akapumzika. wewe unapumzika vipi kama hujamaliza kazi? wanadamu wengi leo wanapumzika bila kumaliza kazi
Mwanzo 2:1-2 "Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. "
Mungu alipoona amekamilisha kazi alifurahia akapumzika kwa maana nyingine isingekamilika asinge pumzika, usipumzike kwa sababu ya siku bali kwa sababu umekamilisha.
Mathayo:12 :1-8 “Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Chombo sio kikubwa kama mtumiaji wa chombo, siku siyo muhimu kama wewe. Anamaanisha nini anaposema mwana wa adamu anaondoka katika uungu anahusisha ubinadamu wetu. Sabato imewekwa kwa ajili ya mwanadamu, mapumziko hayahusu siku tu bali mapumziko ya kweli kutoka katika vifungo mbalimbali
Mathayo 11;28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”
Mimi ndiye Bwana wa sabato “mimi bwana wa mapumziko” yeye ndiye atupaye pumziko, hazungumzii siku. Siku, miaka na nyakati zipo kwetu ili ujue yakupasayo kutenda kwamba ni wakati wa kusoma, kuoa.Siku haipumzishi bali mtu anapumzika na anayempumzisha mtu ni Bwana wa napumziko Yesu pekee, hakuna msaada katika siku.
Yohana 5:39 "Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia."
Wewe nabaki kuchunguza chunguza maandiko katika biblia ukizani huko kuna mzima, chunguza sana Yesu asomewi Yesu anaaminiwa, kuna watu wanaisomea biblia miaka mingi hadi vipara lakini hawana Roho Mtakatifu na hawawezi kuombea wagonjwa.
Usifungwe na siku maana kwa Mungu wetu kila siku ni siku ya Mungu, wewe ndiye unayechagua lini nipumzike. Kumbuka pumziko la kweli lipo kwa Bwana Yesu. Yesu alipomaliza kazi aliacha maagizo kwa watumishi aliowaweka ila wafanye na wawaelekeze watu wafanye kile Yesu amekusudia wafanye ikiwa ni pamoja na kuwapumzisha wenye mateso na vifungo mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ma mateso mbalimbali.
Leo hii tunashuhudia watu wakipata mapumziko katika ndoa zao, afya zao, uchumi wao, Walio katika kristo ni marufuku kupita katika mateso, maana unaye apumzishaye. Hakuna maisha ya raha na amani kama ya WOKOVU.

Shuhuda

EFATHA MASS CHOIR WAKITOA SHUKURANI KWA MUNGU WAO Tunamshukuru Mungu kwa kutuokoa kutoka dhambini tulipokuwa akatuheshimisha kwa kuona tunafaa kuwa vyombo vya sifa ni kwa neema tu.SHUHUDA IBADA ZA LEO


Mch Merania Irengo wa Eneo la Amani
Anamshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kutenda kazi karibu na mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Pia namshukuru Mungu kwa sababu kuna siku mtu mtumishi wa Mungu alisema kila mtu ambaye watoto wao wako nchi za nje warudi nyumbani ili watumikie taifa lao, nikaingia katika maombi Mungu ni mwema mwaka jana mwanangu aliye zamia marekani alirudi nyumbani na mwingine wa kike amerudi, mmoja aliyeolewa Uganda naye karibini atakuja nyumbani na mumewe, kwa kweli namshukuru Mungu
Kwenye kusanyiko la mwaka huu 2014 Mtumishi wa Mungu alisema kuna watu wanaenda kupokea zawadi, nakumbuka tarehe 14 mwezi huu wa kumi na mbili mshirika wangu mama mmoja akanipigia simu kuuliza kama nipo nyumbani nika mwambia nipo baada ya dakika 45 alikuja akanipa gari funguo kadi ya gari na kila kitu akaniambia amenipa gari ili inisaidie katika majukumu yangu ya kichungaji. Hatimaye na mimi namiliki gari kweli Mungu amenishangaza, namshukuru sana Mungu. Nataka ujue changamoto hazina mchungaji kila mtu anachangamoto anazopita nazo lakini kama unaye Mungu atafanya njia kwa ajili yako. Pili neno kutoka kwa mtumishi wa Mungu lina nguvu ya kusababisha jambo litokee. Amen

Saturday, December 13, 2014

Kumpokea Yesu!

Baadhi ya waliotoka Kumpokea Yesu katika Maisha yao, Mungu wetu ni Mzuri...Ushuhuda!

Alex
1.       Amepata Shahada ya Kwanza ya Uandishi wa Habari…na anaweza kujiunga na masters moja kwa moja

Pia ana mshukuru mungu kwa Kumaliza madarasa ya Kukulia wokovu.anamfurahia Mungu wake Amen!

Kamata Neno la Madhabahuni utakuwa Heri mwana wa Mungu!Njiambatanishe na Yesu.

Ukijiambatanisha na Yesu magonjwa yanakuwa mbali nawe, kila aina ya TABU inakaa mbali nawe.
Kama uko katika Huduma furani mahali unapoabudu, jiambatanishe na madhabahu ya mahali hapo,usiangalie kushoto wala kulia, usiwe na mawenge,Tulia mahali ulipo, uwe na Adabu na sehemu unapoabudu, na kuhakikishia utamwona Mungu.

Njoo Ibadani ukutane na Jibu lako.

Tengeneza Hoja mbele Za Bwana, hakika utakutana na majibu ya Maisha yako.
Roho yako iambatane na Roho ya Yesu, ndio maana tukimwita Yesu anaonekana.kwa sababu tumeunganishwa naye katika Roho.
Mfano.
Elisha tunaona ameunganishwa na Elijah, Alitazama juu akauliza Mungu wa Elijah yuko wapi.na alipoiweka ile jozi yake kukawa Njia.
Tujiambatanishe na wapakwa mafuta wa Mungu.wale Mungu aliowaamini. akawapa nguvu kwa ajili ya utukufu wa jina lake.
Mfano Mwingine 1samweli 18:
Daudi na Yonadhani, Roho wa Yonathani akaambatana na ya Daudi.Neno na Mchungaji Aimana!

Mchungaji Aimana:
Tuendelee Na Tadhimini.
Umetembea Na Huduma ya Efatha kwa muda gani.. Harafu umemuona Mungu Kwa Kiasi Gani.
Usemezane na Moyo iabiye Nafsi yako.na hakika huhitaji kuwekewa Mkono na Mtu.
Unaweza ukatembea na Huduma Furani lakini usikutane na yesu.
Tupate live audio streaming www.mixlr.com/efatha

Don George Amemuona Bwana Kwa namna ya kipekee!

Don George 
Zaburi 20:7 Nimekuja nchini mwaka 1991 nilikutana na Mtumishi wa Mungu Mtume na nabii Elias Mwingira mwaka 2001
Nilikuwa katika misukosuko mingi sana lakini baada ya kukutana na Apostle nimefunguliwa mambo mengi na pia Mama Apostle alikuwa akinisaidia mambo Mengi.
Nikaoka, Nikaoa Huku Efatha.
2012 niliombewa Mke wangu alikuwa anatakiwa kujifungua tarehe 9 November,Ilipita wiki mbili hajajifungua na Njia Ilijifunga, aliambiwa ajifungue kwa Operation lakini baada ya kumpigia APOSTLE alitamka neno hatojifungua kwa operation atajifungua salama.
Siku ya operation Mtoto alitokea wodini na madokta walishangaa haijawahi kutokea katika Hospitali hiyo Mzazi kujifungulia wodini.wakamuliiza wewe ni mhindi je Umeokoka? akasema ndio nimeokoka.Mke wangu akajifungua mtoto wa kiume. Namshukuru kwa Maombi yake Apostle na Mungu wangu sana.Amen.


Jumapili Tarehe 14 December! Ni neema Ya kipekee kuwa Mbele za Bwana, Karibu mwana Mungu! Wewe Uliye mbali tupate live kwenye www.mixlr.com/efatha.

Saturday, December 6, 2014

Neno La leo na Mchungaji Aimana.

NENO LA JUMAPILI NA MTUMISHI WA MUNGU AIMANA DOMINIC

Mwanzo 4:7a. kama ukitenda vyema hutapata kibari? angalia ushuhuda wa huyu dada kwamba aliona hana haja ya kusema  atafauru lakini alijifuta mwenyewe. mangapi yametamkwa kwenye madhabahu ya Mungu lakini kwako hayajatimia kwa sababu tunashindwa kujitakia mema? Kama yale yaliyo tamkwa kwangu na tungeyatakia mema yale tungekua mbali. Nipo hapa kukukumbusha achana na zile nyaraka ambazo zimeandikwa na wanadamu angalia nyaraka za kwenye Bibilia.

Tukiamua kubadilika tukabeba nyaraka za madhabahuni tutakua na ushuhuda kabla mwaka haujaisha. Nenda katafute Yule mtu mwenye dhambi anaye jiuza anaye piga miziki disko mlete kwa Yesu wapo tayari wanatusubiri tuwaendee. 


Umepakwa mafuta ya Roho Mtakatifu je unayatendea mema yale mafuta? kwenye kamati haupo ivi hayo mafuta yako unayatendea mema. Sababisha mchungaji wako wa kituo afurahi angalia unaweza kufanya nini hemani mwa bwana fanya usababishe Yesu afurahi. 

Unatupata live kwenye www.mixlr.com/efatha audio live streaming...!!


Je ulionao karibu wanafurahi kwa sababu yako?

Mungu anafurahi kwa sababu yako, kazi ulioitiwa kuifanya unaifanya kwa uaminifu.
Ebu tufanyike furaha kwa viongozi wetu na Mungu wetu.Neno na Mchungaji Aimana:TAFAKARI uone ni nini iyo haujafanya Kafanye vizuri.

Mwanzo 4:7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko inakuotea malangoni, nayo inakutamani wewe walakini yakupasa ushinde.
Tutamani sana kutenda mema,Kukaa katika kumtumainia Mungu tutapata kuwa na shuhuda.
Ukiamua kubadilika inawezekana kabisa, ukitamani lile linalokusumbua liondoka litaondoka tu, pale ikiamua kusima na Mungu ambaye ni msaada wetu.Sifa kwa Bwana.wetu Mungu baba...Yote alimaliza pale msalabani.
SHUHUDA:

Dorcas Jackson
Kutoka Eneo la Upendo.
Ushuhuda

Dorcas Jakson kutoka upendo napendA kumshukuru Mungu ilikuwa mwaka 2008 nimemaliza form four sikupata credit moja na nilikata tama katika ule mwaka nilipokuwa kwenye ibada jumapili moja mtumishi wa mungu alitangaza kwamba kuna binti anataka kufika chuo kikuu baada ya mwaka ule nilipata niliendelea na advance level na nilipata division one katika wasichana wote tulikuwa wawili tu tilofaulu. ulipofika mwaka wa pili ilikuwa na changamoto kubwa nilipokuwa najiandaa field ilikuwa mwezi wa 9 nilipata changamoto sana kwani kila Mwalimu alikuwa ananitaka nilipata bahati ya mtumishi wa mungu akasema nitakuwa wakwanza na ninaomba kwaajiri yake akasema bwana yesu ninaomba nimwongoze kwa mwanafunzi huyu na baada ya maombi hayo Mtumishi wa Mungu mimi nilikuwa nakubarika na katika watu

wanaotakiwa kupeleka repoti nilikua peke yangu na kuna wanafunzi wako wengi lakini mimi niliona ni kibari kwa mungu alinitetea lakini Yule mwalimu aliendelea kuniambia maneno ya ajabu lakini ninamshukuru Mungu kwani  na katika ile ripoti nilipewa A. 

VIJANA VIJANA.....MNAKUMBUSHWA KAMBI YA VIJANA TAREHE 18 MWEZI HUU KIJANA KARIBU SANA UKAPOKEE MBARAKA WAKO.


TUPO LIVE SASA tupate katika mtandao wetu, www.mixlr.com/efatha ubarikiwe

Saturday, November 29, 2014

Ibada ya asubuhi ya kwanza inayo aanza saa moja kamili hakikisha unakuwepo jumapili ijayo.Kuna ya Pili saa NNE na ya tatu saa SABA karibu sana.

IBADA YA TAREHE 30/11/2014
NENO LA JUMAPILI NA MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

MKESHA MKESHA MKESHA

UTAKUWEPO SEHEMU YA KUKATA MANENO.

YOHANA 5:1 – 18 
1.      Imani ya Kuona na
2.       Imani kuto kuona

Jinsi Yesu alivyo kuwa anafanya maajabu yake YOHANA 5:1-8 Imani lazima ikupeleke mahali lazima ikufikishe kwenye hitma ya kile unacho kitarajia. Yerusalemu hapo kunakitendea kazi, bilika liko pale Yerusalemu lilikuwa na matawi 5 na ndani ya hayo matawi kulikuwepo na jamii kubwa ya wagonjwa na hao wagonjwa wamegawanyika katika matatizo yao, VIPOFU, VIWETE, WALIO POOZA, ni watu wenye safari ya kiimani. Imani lazima ingojewe mtu mwenye imani anasubira. Mwenye imani hatafuti muujiza anatafuta neno likolee.

Ufunuo 22:17 na Roho na Bibi harusi na aseme njoo. YOHANA 7:37 BIRIKA LINA MATAWI 5 zaburi 40:1:5 atakuponya na mambo mabaya yote.
1.      Kuponya wenye shinda
2.      Kudhibitisha watu na imani zao angalia sana mtu asije kuchukua cha kwako. Ng’angania.  Kwani aliye kuwa wa kwanza kuingia katika bilika ndie anaponywa.


Fanya vile anavyotaka Mungu ufanye usitake wewe, tamani kuwa wa kwanza na umuweke Mungu wa kwanza na usiache mtu akutangulie. Acha kuzurula tulia kwa Mungu wako Yesu ni kitugani alikiona kwa Yule mtu kiwete? Aliangalia imani aliyo Yule mtu na nia aliyo anyo kila wakati akitaka kuingia mwenzie anaingia ndani ya miaka 38 hatoka hakukata tamaa iko siku muujiza utatimia.

Jesus Only Jesus

He did not look at the answer of the paralyzed he said stand up and walk.
He understood the faith in that man, the problem was who will Immerse him into the pool.
And there he was he instructed him to walk. Because he was there and the man had faith if the get into the pool is healed which was the logic.Jesus took the anxiety out of the man by Instructing upon a task of taking a step of waking up and walking.this was soooo great.wow!!

Tamani nafasi ya kwanza, muweke Mungu wa kwanza.


Being before the lord is joy:

Being before the lord is joy:
Efatha Members rejoices, happy before the lord...its amazing very amazing..be one of them who are entitled to the Kingdom of God

This one now explains that he has been there for 38 years.

And we see Jesus asking him what do you want to be done to you now.SEE "this i want somebody to take me into the pool because for when i begun to go, others deep before me".And Mighty Jesus emphasis to him stand up take your beddings and walk.amazing faith that is.and he does exactly as he is told by Jesus.
and he is healed.

Kuwa na Subira; always be patient...e.g.

My Help and My Deliverer
1 I waited patiently for the Lord;
he inclined to me and heard my cry.
2 He drew me up from the pit of destruction,
out of the miry bog,
and set my feet upon a rock,
 making my steps secure.
3 He put a new song in my mouth,
a song of praise to our God.
Many will see and fear,
and put their trust in the Lord.
4 Blessed is the man who makes
the Lord his trust,
who does not turn to the proud,
to those who go astray after a lie!
5 You have multiplied, O Lord my God,
your wondrous deeds and your thoughts toward us;
none can compare with you!
I will proclaim and tell of them,
yet they are more than can be told.

In the book Of John why we are seeing a bowel/pool of water.
And we see people waiting for it to stir up for them to deep themselves into it.
This shows how they had the sense of patience of waiting for water to stir up, and the logic is that the first to enter the pool gets healed.
So God requires our attention to our areas of work as far as the kingdom of God is concerned.
And verily i say unto you today you shall receive your miracle.
Amen

Kuhusu Imani! Ufunuo 22:17

Mtu yeyote mwenye Imani lazima awe na subira, ukiwa huna subira utakuwa mtu wa kuanza upya kila wakati.
Mwenye Imani hatafuti Muujiza, anasubiri Neno la Mungu likolee Vizuri.

Revelation:22:17
The Spirit and the Bride say, "Come." And let the one who hears say, "Come." And let the one who is thirsty come; let the one who desires take the water of life without price.

Neno limeanza Na Apostle Elias Mwingira..John 5:1-18

Imani isiyo kufikisha mahali imekufa..Lazima Imani iwe na Hitma..Ikufikishe sehemu..Yesu yuko mahali Panaitwa Yerusalem.Kuna vitendea KAZI...ili kazi  iambatane na kile unachokitaka.Yesu alikuwa katika sehemu yake ya Kazi..na mahali pale kulikuweko na jamii ya wahitaji/wagonjwa na walikuwa katika vikundi.k.m vipofu, viwete, waliopooza,
Kwa ivo walikuwa na Imani kwamba Yesu anaweza kuwaponya.

Nguvu ya Mungu Kazini!

Yesu anapita akiwahudumia watu wake asubuhi ya leo.Watu wanafunguliwa Mutumainie Mungu upokee muujiza wako leo anaweza yeye aliyetukuka mbinguni na Duniani.

Mtume Na nabii Josephat Elias Mwingira

Sifa kwa Bwana wetu....wewe ni baba Amen...aya twenda Pamoja na wanaEfatha Mwenge Tanzania!!

Sifa kwa Bwana Yesu

We ni baba hakuna Mungu kama wewe, wewe ni baba Hakuna Mungu kama wewe...utukuzwe baba, muumba wa miisho yote ya Dunia, Mwanzo tena Mwisho, Jabali letu, mwamba wenye imara, Pembe ya wokovu wetu. tunakuimbia.haleluyah ,Mungu wetu Mzuri saaana. Mzuri wewe kwetu. Baba yetu hakuna kama wewe. ulituumba sisi sifa na utukufu ni kwako.AaaaaaMen!

Ibada ya kwanza inaendelea ni muda wa matoleo...futatana nasi katika www.mixlr.com/efatha ubarikiwe sana mwana Mungu

Saturday, November 15, 2014

KUKAA NDANI YA YESU

Ukikaa ndani ya Yesu kunamambo makubwa yanatokea kwako, ndio maana alitoka mbinguni akaja kukaa ndani yangu. Yesu Kristo alikuwa mbegu kwaajiri yangu kwahiyo anataka mimi na wewe tumzalie matunda. Bwana anataka na mimi na wewe tuzae watu wengi tukaandaye kanisa kwaajiri ya unyakuo.

Yohana 15:1-20 Yesu ananena na wanafunzi wake, anawaasa wanafunzi wake anawapa maagizo anasema mimi ndimi mzabibi na uzima, na kila tawi linalozaa ndani yake huzaa, lisiro zaa hukatwa. Kama wewe haupo ndani ya Yesu ni vigumu sana kuzaa matunda. Mwanzo 23:26 Yesu anasema hatutauwa tasa wala matubo yetu hayata haribika. Ili uzae ndani ya Yesu kuna kuzaa matunda, Yesu alikuwa mzabibu mwema na amenipanda ndani ya mzabibu mwema. U

Ukiona tabia yako hajawa njema basi Yesu hayupo ndani yako, kama Yesu alikuwa mtii lazima uwe mtii kiburi kinatoka wapi?. Hakuna kitu kibaya wewe umeokoka harafu siku unaenda mbinguni Mungu anasema sikujui kitu kibaya sana.

Yesu alikuja kuufanya ulimwengu umgeukie Mungu kutokana na wanadamu wamegeuka na kutenda dhambi. Umeletwa ili umzalie Mungu matuda,Yesu alipoenda kwenye ule mtini alipouangalia anataka matunda kwake alikosa aliulaani ule mti. Angalia usilaaniwe, tusababishe maongezeko katika ufalme wa Mungu, kunafaida katika kuzaa matunda. Kuzaa sio kazi, kazi nikutunza na kunyonyesha.

KUNA FAIDA TUNAPOZAA MATUNDA TENA YALE YANAO DUMU.
1.     Ukikaa ndani ya Yesu anakutendea mema
2.     Pendo la kristo linahamia kwako ukishika amri zake. Yesu akasema pendaneni, Ila sisi wapendwa hatupendani wala hatusalimiani. Je tutafika mbinguni? Usikubali kukwazika wala kuwa mrokole jina tu. Upendo huhimili yote
3.     Faida nyingine tunakuwa  rafiki wa Yesu. Fungu la 10 ni ulinzi wa kutosha
4.     Faida nyingine anakutoa kunako utumwa na anakufunulia siri zake. Ibrahimu alikuwa rafiki wa Mungu.

5.     Huwezi kuyafanya ya dunia ukiwa na urafiki na Mungu kwani  ukipendwa na Dunia ujue hujakaa ndani ya Mungu. Ulimwengu  ulimchukia Yesu lazima dunia ikuchukie ni lazima ujue wewe ni rafiki wa Mungu. Using’anganie dini. Kila mtu ataitwa kivyake umeletwa huku duniani kwa kusudi fanya mapenzi ya Mungu. Kazi ya dini inakuweka kwenye kibano ili usiweze kumjua baba yako halisi ndio baba wako wa siri, dini ni mlezi,kaa ndani ya Yesu tembea na Yule aliekuita. Mwili ulionao hauna dhamani siku Mungu akiutoa kwenye huo mwili wanakimbiza kuzika.  Fanya kazi ya kuamrisha mwili sio mwili ukuamrishe wewe. Kaa ndani ya Yesu ili ubaki kwenye mti ili uweze kupaliliwa na Mungu kama mti mzabibu. 

Tuachane na mwili, tuache kuufurahisha mwili, mwili ni wa udongoni tu, Roho ndio ya Mbinguni, Tutamani mapenzi ya Mungu, Tufanye kazi pamoja na Kristo.Neno la Leo Kukaa Ndani ya Yesu.

FUNGU LA KUMI NI ULINZI...TOA KWA UAMINIFU NAYE ATAMKEMEA YULE ALAYE NA YULE AHARIBUYE.


Faida za kukaa ndani ya Yesu;

Unapokaa ndani yake Kristo Lile pendo la kristo linahamishiwa kwako.unakuwa na ule upendo wa Kristo.
1.Tutashika amri zake Yesu
2.Tukikaa ndani ya Yesu atatundea mema
3.Hatutasengenyana, tutasaidiana, tutakuwa na Umoja
4.Yesu atatuombea kwa Baba wetu wa Mbinguni.

Neno Linaendelea tupate mtandaoni live audio streaming...www.mixrl.com/efatha

Hakikisha unalea Kondoo wako mpaka asimame,ukileta mtu kwa Yesu Mlee Mpaka nae afike mahali Tumzalie Mungu matunda. ndio maana tuliokolewa.Amen

USHUHUDA

     Neema bakiri eneo la tukufu  Mungu amenitendea mambo makuu sana jambo la kwanza niliokoka 2010 lakini sikuweza kusoma madarasa nilikuwa sijapata nafasi na nimesoma madarasa nimebatizwa na mafuta nimepakwa jana tarehe 15/11/2014, pia nilikuwa  nahamu ya kumjua Mungu nilikuwa natamani sana lakini sikuweza kupata nafasi, ya kwenda zone lakini nilipo muomba Mungu kwamba nataka niende zone akanijibu, ninamshukuru sana kwamba ninaenda zone na mchungaji wangu na askofu wangu ananisimamia. Jambo la tatu Mtume na Nabii alitupa unabii mwingi sana tulipokuwa kusanyiko akasema watu wote watapewa zawadi mtaenda kupata kazi na mtaenda kupata nanilipokea zawadi ya kwenda Arusha, na wakati najiandaa na safari ya  kurudi nilipata ajari ya Piki piki nilipata kugongana na gari nilijua labda nimeumia bega niliambiwa niende hospitali lakini nilikataa kwani ningeenda hosptali nisinge fika jana kwenye mafuta alisema nilipokuwa kwenye gari bega lilikuwa linauma sana na baadaye nilitembea na kitabu cha mtembeo wa Mungu kwa hao alio waridhia nikakiweka kwenye bega langu nikaomba nikapokea uponyaji, namshukuru sana Mungu.

NENO LA MUNGU NA MCHUNGAJI VICT TEMU KUKAA NDANI YA YESU:

Ukikaa ndani ya Yesu kuna mambo makubwa yanatokea kwako, ndio maana alitoka mbinguni akaja kukaa ndani yangu. Yesu Kristo alikuwa mbegu kwa ajiri yangu kwa hiyo anataka mimi na wewe tumzalie matunda. Bwana anataka na mimi na wewe tuzalete watu wengi tukaandaye kanisa kwa ajiri ya unyakuo.

Yohana 15:1-20 Yesu ananena na wanafunzi wake, anawaasa wanafunzi wake anawapa maagizo anasema mimi ndimi mzabibi na uzima, na kila tawi linalozaa ndani yake huzaa, lisilo zaa hukatwa. Kama wewe haupo ndani ya Yesu ni vigumu sana kuzaa matunda. Mwanzo 23:26 Yesu anasema hatutauwa tasa wala matumbo yetu hayata haribika. Ili uzae ndani ya Yesu kuna kuzaa matunda, Yesu alikuwa mzabibu mwema na amenipanda ndani ya mzabibu mwema.

Ukiona tabia yako haiendani na taratibu za yesu, basi Yesu hayupo ndani yako, kama Yesu alikuwa mtii lazima uwe mtii kiburi kinatoka wapi?. Hakuna kitu kibaya wewe umeokoka harafu siku unaenda mbinguni Mungu anasema sikujui ni kitu kibaya sana.Ibada Ya Kwanza..Neno La Mungu:kukaa Ndani ya Yesu Na Mtumishi wa Mungu Vicky Temu.KUKAA NDANI YA KRISTO YESU...TUPATE LIVE www.mixlr.com/efatha

Ibada ya kwanza inaendelea, tupate live kwenye tovuti yetu,facebook..kuna kitu Nyumbani mwa Bwana.