Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Monday, October 28, 2013

MUNGU WETU NI MZURI

Haleluya,... MUNGU wetu ni MZURI Sana, daima Anatuwazia MEMA, Anatupenda sana, Bwana wetu YESU KRISTO ni MZURI sana, YEYE HATUACHI KAMWE, daima yuko UPANDE Wetu, daima yuko NASI Watakatifu wake. ROHO MTAKATIFU ni MZURI, YEYE ni MSAIDIZI wetu, Daima HUTUONGOZA, HUTUKUMBUSHA YOTE, HUTUFUNDISHA YOTE, HUTUEPUSHA na Mabaya na Hatari zote, HUTUOMBEA KUSIKOTAMKWA, Daima HUKAA NDANI YETU, Sisi ni HEKALU LAKE.

Jana Jumapili Wana wa MUNGU Wana Efatha, Watanzania WENZANGU, Tunamshukuru MUNGU wetu kupitia ROHO WAKE; Tulipokea chakula kizuri sana cha KIROHO Kupitia Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira, MUNGU anatamani watakatifu wote WATOKE katika Kusetwa na yule ibilisi muovu shetani. ROHO WA BWANA Alimtumia Vizuri Mtumishi wake Mama Eliakunda KUTUPATIA UFAHAMU JUU YA MAISHA YETU YA KIROHO.

NYUMBANI MWA BWANA

 Tunamuabudu BWANA wa mabwana, MFALME wa wafalme,... YEYE ALIYEMUWEZA WAYOTE.
 " NENO, MAFUNDISHO, MAHUBIRI YA JUMAPILI Tarehe 27/October/2013 toka MADHABAHU YA KITUME na KINABII Mwenge Dar Es Salaam, EFATHA MINISTRY." - Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira.

“MOYO WANGU UMEJAA SHUKRANI”
- Jifunze KUSHUKURU, utapata kuweza kuona mambo mapya katika maisha yako.
Isaya 12:1-6 “Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeuka mbali, Nawe unanifariji moyo. Tazama, MUNGU ndiye wokovu wangu, Nitatumaini wala sitaogopa: Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni Jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa. Litajeni jina lake kuwa limetukuka……..”

Unaposhikilia jambo lako katika Ulimwengu wa roho, LITATOKEA. Unatakiwa UAMINI kwa NGUVU, Vita vyetu ni katika Ulimwengu wa roho, shetani hana jipya, ana COPY tu, ORIGINAL ilishachanwa, Copy amebaki nayo ili aone jinsi UNAVYOSHINDA.

Mpe YESU moyo wako, Anza KUFURAHI na YESU.

Kuanzia leo ebu anza KUJIFUNZA kutamka NENO Unalolitaka, anza KUSHUKURU, anza Kujifunza KUSHUKURU.

Anza KUJITAMKIA MAZURI, Unapotamka MAZURI yatasogea.

Unataka mke Mzuri; TAMKA Mke mzuri, Unataka Mume Mzuri; TAMKA Mume mzuri, Unataka Mtoto mzuri; TAMKA Mtoto mzuri, Unataka Jambo Zuri; TAMKA Jambo zuri, TAMKA VIZURI sasa.

Tangaza MAKUU ambayo MUNGU AMEKUTENDEA, Ukiyatangaza YANASOGEA.

Zaburi 37: 1-11 “Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili. Maana kama majani watakatika mara, kama miche mibichi watanyauka. Umtumaini BWANA ukatende mema,………….”

Angalia kile ambacho MUNGU AMEKUAHIDIA wewe, USIWAANGALIE wale watenda mabaya wafanikiwavyo, maana hao moto wameandaliwa tayari, hao ni wa moto tu.

Wewe ndiwe FURAHA ya MUNGU, MUNGU Alikuumba kwa mfano wake ili Afurahi, KINACHOMUUDHI MUNGU ni DHAMBI.

MUNGU Wetu Anatuwazia mema, Mawazo yake ni ya AMANI Kwetu.

Ushamwambia BWANA haja ya MOYO, sasa Mpe NAFASI Afanye.

BEBA Sifa za BWANA ndani ya Moyo WAKO.

Iko RAHA katika Kumtegemea BWANA, Ipo FURAHA katika KUMTEGEMEA BWANA.

Zaburi 37:1-11

- Utatafuta ugonjwa wako, hutauona tena, wale waliokuwa wanakushambulia hutawaona tena, Tatizo lako hutaliona tena.
- Toa MATAKATAKA yote ndani ya Moyo wako, Toa UCHUNGU wote ndani ya Moyo wako, maana huo MOYO utapelekea mwili wako kwenye MAANGAMIZI.
- Moyo wako UTAKAA na BWANA, Umeamua KUTEMBEA na BWANA.
- Kaa na BWANA, ili UFURAHIE VYA KIFALME.

BWANA Anawacheka maadui zako, maana YEYE ndiye Mpiganaji vita.

Ukipata AMANI, Umepata AFYA Njema, Unapokosa AMANI Unakuwaje?. Tafuta AMANI ya KRISTO, kuna watu wanafanya maamuzi mabaya kwa sababu WAMEKOSA Amani, walikuwa wana hasira.

Hasira HASARA, Wewe kwa Mtu Uliyeokoka usiwe na Hasira, Ukiwa na Hasira MWITE BWANA YESU Akupe AMANI.

Usikubali KUSHINDWA, Taka MASHAURI YA ROHO MTAKATIFU, Mwenye Hekima ya MUNGU hafanyi mambo kwa Hasira.

ANZA Mazoezi ya KUSHANGILIA, Anza mazoezi ya KUMTUKUZA BWANA.

KITU MUHIMU: LINDA MOYO WAKO, Maana Moyo wako Ukiwa na Amani UTAPATA YOTE.

Mpe Moyo wako YESU, SI Binadamu, Binadamu Watu WATAUTOBOATOBOA.

Unamuweka MTU Moyoni, UNAMBEBA Mtu Mwenye Kilo kama 85 MOYONI, huoni Unajiangamiza?

FURAHA YAKO si MUME, Si WATOTO, si MKE, si NYUMBA NZURI,…. BALI NI YESU. Maana Watoto Wataolewa au Wataoa, Mume anaweza kuwa Safari au kuwa MBALI nawe, LAKINI YESU HAWEZI Kukuacha.

MUNGU HATAKI Kuona KITU Kinaingilia kati yako na YEYE, kama Mume ndio Anakufanya uwe mbali na YEYE MUNGU, unaweza kushangaa Mume wako ANAONDOLEWA, Kitu CHOCHOTE kile KISICHUKUE nafasi ya MUNGU.

Kuna watu ndoa zao ZIMEKUFA kwa sababu Waume zao walichukua Nafasi YA MUNGU.

Na MUNGU NI MWENYE WIVU Sana (Imeandikwa: MIMI NI MUNGU MWENYE WIVU), Akiona UNAMSAHAU kwa sababu ya KAZI, au BIASHARA, au MUME, au MKE, au WATOTO, au SHAMBA, N.K, MUNGU ANAWEZA Kuviondoa hivyo vyote ili AWE KARIBU NA WEWE.

WOKOVU ni Nuru, ni Taa; kwa hiyo Watu WAIFUATE TU.
Zaburi 119: 105
Zaburi 119: 36

Ukiwa na BWANA (WOKOVU) Utapata AKILI NZURI na KIBALI.
Mithali 6: 16-18 “Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;


Wednesday, October 23, 2013

WORDS OF WISDOM AND FULL OF KNOWLEDGE

(Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira)

“EVIL DOERS”

After all these the bible tells us:-
Psalm 27:1(The LORD is my light and my salvation; whom shall I fear? The LORD is the strength of my life; of whom shall I be afraid?)

It is good when you UNDERSTAND the moment evil strikes at you, the best time for you to PRAY, the time to DESIRE ASSISTANCE, and the time to require fellow BRETHREN or ELDERS.

Psalm 27:2 (When the wicked, even mine enemies and my foes, came upon me to eat up my flesh, they stumbled and fell). When Evil is directed at you, its main aim is to DEVOUR you. It is good if you UNDERSTAND what you have PASSED through, EVIL comes from people whose HEARTS are filled with HATE and when they speak the UTTER SWEETNESS. When they speak, you may think you are UNITED, but SPIRITUALLY they are FULL of EVIL. The evil are they that seek to devour your flesh. They are those who are subtle, hypocrites, witches etc.

He is talking about the oppressors and enemies. These EVIL DOERS are your enemies and your oppressors. All those that are against you aim to DESTROY you. He/ they might have prepared themselves to destroy your MARRIAGE, OFFSPRING, BUSINESS, DEVELOPMENT, and HEALTH and also to destroy your HONOUR.

Many in the community are DESTINED to great things, but they have no direction due to the evil who are ALL AROUND them; their oppressors LOOK UPON them, and they have surrounded them without their knowledge.

When they SPEAK, you will think they have good intensions but in their hearts they THINK evil. This is not only towards you, but also all those that pass their way. Evil is not in words but a habit that is in-built in one’s HEART. You can’t TRAIN in evil, you are BORN with it. Evil is a habit you’re BORN WITH, as the bible says: “LORD JESUS said to the Jews, you are born of your father the devil, for in the beginning they were ALL EVIL.” since the beginning Satan was a LIAR, KILLER, EVIL, and anyone who is full of EVIL works to destroy.

Then GOD said, “Behold the day I will send MY NEW SPIRIT, and I will give you a NEW SPIRIT and get rid of THE HEART OF STONE.”
WAOTEAJI…

HAVE YOU MET WITH THE EVIL SPIRITUALLY? WHEN HAPPENS WHEN EVIL COMES OVER YOU?

There is an army that lags behind you who aim is to make sure that you have fulfilled the evil intent. When evil rises or when the evil attack you the usually follow up in large armies. When the army stops, you get attacks from all corners without your knowledge on where it is coming from and how.”

(These Holy Words, full of Wisdom and Knowledge will continue)
This is the time for BREAKTHROUGH child of GOD. Don’t have room for anything else but BREAKTHROUGH.

May the Consent of the LORD be with you.

Monday, October 21, 2013

MANENO YENYE HEKIMA

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

''Saa ile ile UNAPOAMINI BWANA YESU KRISTO ameingia kwako, Saa ile ile UMEPONA"

NDANI YA NYUMBA YA BWANA JUMAPILI

 Mmmh... Nyumbani mwa BABA kuzuri sana,...
 Watumishi wa MUNGU wakiwa Nyumbani mwa BWANA...
 Wana wa MUNGU ''Mass Choir'' Wakimuimbia na Kumchezea MUNGU BABA Yetu MKUU PEKEE.
 Asante MUNGU wetu MKUU BABA, Asante YESU kwa NENO ZURI la leo, Neno zuri BWANA la KUTUPONYA, la KUTUWEKA HURU, la KUTUPA UZIMA, AMANI na FURAHA yako BWANA YA KWELI, Asante BABA, Asante YESU... ''Maarifa ya ROHONI"
 Jumapili kwetu ni Muhimu sana kwa Wana wa MUNGU, Wana Efatha,... kwani ni siku MUHIMU sana kwetu Kumsikiliza Mkalimani wetu Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akitupa Chakula cha Roho, Akitupa Maagizo Aliyopewa na BABA Yetu wa Mbinguni kwa ajili yetu sisi wana wa MUNGU,... Ni siku ya Kukaa chini miguuni mwa BABA na Akitupa Maneno ya HEKIMA na UFAHAMU kwetu,... Oooh Asante YESU, Asante BABA.


Sunday, October 13, 2013

SIKU YA SABA YA KUSANYIKO L EFATHA 2013 (SIKU YA MWISHO Y KUSANYIKO)

 UTUKUFU Wa MUNGU Wetu MKUU, Ulionekana katika KUMTUKUZA na KUMUIMBIA na KUMUABUDU na KUMPA SIFA Kwa Nyimbo zenye UTUKUFU... Oooh Asante YESU, Ilikuwa Amani na Raha tu kwa YESU.


 Usiku wa Mkesha wa KUSANYIKO KUU LA BWANA MUNGU Wetu MKUU PEKEE 2013, Kibaha Precious Centre Mji wa BWANA, (Pichani Wanakwaya wa Mass Choir wakiwa Madhabahuni Wakimwimbia na Kumsifu na Kumtukuza na Kumuabudu na Kumchezea MUNGU WETU MKUU PEKEE, BABA YETU).


Oooh Haleluya, USIKU wa Mkesha wa Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu MKUU umewadia, MUNGU Wetu na BABA Yetu ni MZURI Sana, Hatimaye BWANA Wetu YESU KRISTO Atakuwa nasi Usiku wa leo Akishiriki nasi Karamu ya Chakula cha BWANA (Mwili na Damu ya YESU KRISTO), BWANA Ametuandalia kupitia Mtumishi wake Mwaminifu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira,... Oooh Asante YESU, Asante BWANA, Asante BABA.


 

 Mtumishi wa MUNGU Mwanamuziki wa Injili wa Nyimbo za Kuabudu na Kusifu toka Uingereza, alikuja na Mtumishi wa MUNGU Rev. Ola-Vincent Odulele,... kwa kweli Tunamshukuru MUNGU BABA sana kwa uwepo wake kipindi hiki cha Kusanyiko KUU hili BWANA MUNGU wetu 2013 hapa Kibaha Precious Centre, Tulisifu na Kuabudu MUNGU Wetu BABA MKUU kwa UTUKUFU Mwingi sana, Haleluya... Asante YESU, Asante BWANA.


 Mtumishi wa MUNGU Rev. Ola-Vincent Odulele kutoka Uingereza, Tunamwambia MUNGU Wetu MKUU BABA Asante sana, Tunamshukuru MUNGU Wetu MKUU kwa kutupatia NENO Zuri kupitia Mtumishi huyu, kwa kweli MUNGU Wetu Anatupenda sana Wanawe, Hapendi tufe kwa magonjwa, Hapendi tupate shida, hapendi Tuhangaike, Hapendi tuwe maskini... Haleluya, Asante YESU, Asante BWANA.


 Haleluya,... Tunamshukuru MUNGU Wetu na BABA Yetu MKUU PEKEE, kwa Wema wake MKUU na UPENDO Mwingi Juu yetu wanawe, kwani Jumapili njema yenye UTUKUFU Mwingi na AMANI iko nasi, Haleluya... BARAKA na NEEMA na USHINDI Ujuu YETU Wanawe, Haleluya.

Leo ni siku ya FURAHA na SHANGWE sana kwetu Wana wa MUNGU Wana Efatha, kwani ndio Siku tunayokwenda kumalizia Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu BABA MKUU mahali hapa Kibaha Precious Centre 2013,... Haleluya.

Pia leo TUNAFURAHA Sana Wana wa MUNGU wana Efatha, kwani TUNAENDA KUSHIRIKI Kalamu ya CHAKULA CHA BWANA WETU YESU KRISTO Pamoja nasi Jioni ya Leo,... Oooh Ni shangwe na Furaha tele, Kwani BWANA AMETURIDHIA Kuwa naye Jioni ya leo Pamoja naye, Na KUSHIRIKI DAMU na MWILI WA BWANA WETU YESU KRISTO, Haleluya... Kweli ni FURAHA KWETU.

Asante BABA, Asante BWANA Wetu YESU KRISTO, Asante ROHO MTAKATIFU Kwa KUTUANDAA.

SIKU YA SITA L KUSANYIKO LA EFATHA 2013

Breaking News: Mtoto usiku huu amezaliwa, Haleluya... katika Kambi hii ya BWANA Kibaha Precious Centre.


Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akipita katikati ya Wana wa MUNGU na Kuwabariki katika Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu 2013, Kibaha Precious Centre.

 Asante YESU kwa Kumchagua Mtumishi wako na Kumtuma kwetu aje Atuandae Kutupeleka Mbinguni, Asante BWANA kwa UPENDO wako Huu Kwetu, Asante YESU.


Haleluya,... Viwete, Wagonjwa, Waliopooza: WAMEPONA na Kutembea kwa NGUVU ya MUNGU WETU MKUU, MUNGU wa Efatha, Haleluya... Kwa JINA Lililo KUU LA YESU KRISTO BWANA.


 Haleluya,... leo ni Siku nyingine tena, Tunamshukuru MUNGU wetu na BABA Yetu Aliye MUNGU MKUU PEKEE na Mtakatifu wa Watakatifu, NGUVU, UWEZA, MAMLAKA ni Yake MILELE hata Milele.

Jana jioni tuliona Uwepo wa MUNGU Wetu MKUU kwa Jina la YESU KRISTO Bwana MUNGU Wetu Aliye Hai, Tuliona Miujiza na Nguvu za YESU KRISTO Ikitawala kupitia Mtumishi wake Mpenzi Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Wagonjwa walipona na kusimama na kutembea, Waliopooza walisimama na kutembea, Watu walifunguliwa na kuwekwa HURU.

Leo ndiyo siku YENYEWE ya Uponyaji na Ukombozi, Haleluya... Tunamuinua MUNGU wetu MKUU na Kumwambia Asante, kwa Kuwa ANATUPENDA Saana na Kutujali,...Haleluya.

(Pichani Mama aliyekuwa anatembelea fimbo ya usaidizi,... baada ya kupokea Nguvu ya Uponyaji ya BWANA wetu YESU KRISTO,...Ooooh Alitembea Mwenyewe bila mkono wa fimbo ya kutembelea Haleluya).

Mtoto huyu alikuwa hawezi kutembea, lakini leo AMETEMBEA,... Haleluya YESU NI MZURIII, YU HAI YESU WETU wa EFATHA.

Friday, October 11, 2013

SIKU YA TANO YA KUSANYIKO LA EFATHA 2013

Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akimkaribisha Mtumishi wa MUNGU toka Uingereza kwa ajili ya kutupatia NENO la MUNGU,... Asante YESU BWANA hata kwa kuwaleta Watumishi wako wengine toka sehemu mbalimbali za Dunia kwa ajili ya kutupa CHAKULA CHA KIROHO Wanao, Asante YESU, Asante BWANA Kwa UPENDO Wako kwetu Wanao, Asante BWANA.

Asante BWANA Wetu YESU KRISTO BWANA, Kwa Kumchagua Mtumishi wako Mwaminifu Uliyempenda sana kumpa na KUMTUMA na Kumpa KUSUDI ili Aliandae Kanisa lako Tayari kwa Unyakuo, Kanisa lisilokuwa na Manyaaa,... Asante BABA, Asante YESU.''Kabla ya Mkutano huu/ Kusanyiko hili kuisha, Matatizo yenu, Vilio vyenu vyote vitakwisha...."

(Kipindi cha Mahubiri na Mafundisho Sasa hivi kinaendelea kutoka Kusanyiko la BWANA MUNGU Wetu MKUU 2013 katika Mji wa BWANA Kibaha Precious Centre).

  


''Wewe ndiwe MPENZI WA MOYO WANGU, Ulifanya njia Jangwani, Huwezi KUSHINDWA, Wewe ni MUNGU BABA, Wewe Unabaki vile vile ni BWANA, BABA Unastahili KUINULIWA JUU,.... Tunaungana na WAZEE 24 kule Mbinguni, tunasema WEWE NI BWANA, Wewe ni BABA, Ooooh Wewe ni MUNGU, Haleluya..... BABAAAAA.''

(Kipindi cha Sifa na Kuabudu Sasa hivi kinaendelea kutoka Kusanyiko la BWANA MUNGU Wetu MKUU 2013 katika Mji wa BWANA Kibaha Precious Centre).

Thursday, October 10, 2013

SIKU YA NNE YA KUSANYIKO LA EFATHA 2013

 Haleluya, Asante BWANA, Asante YESU kwa MASHANGILIO BWANA Haleluya. Ni Shangwe na Furaha nyumbani kwa BABA Yetu Aliye MUNGU Wetu MKUU wa PEKEE.... Kibaha Precious Centre kwenye Kusanyiko la BWANA MUNGU Wetu 2013.


Mafundisho na Mahubiri toka Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu Aliye HAI MKUU, MUNGU WA KWELI; Kibaha Precious Centre 2013.

Mtumishi wa MUNGU: ASKOFU KITONGA toka NAIROBI KENYA wa KANISA LA REDEEMER CHURCH.

SOMO: AMANI
Watu wengi wanakwenda kanisani lakini hawana safari ya kwenda mbinguni!!. Wengi mnateseka na wengine mnanunua madawa kwa sababu mnateseka, Kwa nini Paulo aliwaambia Watumishi FURAHINI katika BWANA? Je ni kweli Watakatifu WANAFURAHI? Kweli ni kwamba HAKUNA kwa sababu bado wanahitaji AMANI, ninataka unaposhangilia USHINDI wa Efatha ruhusu AMANI kwanza, Waebrania 12: 14. Mara nyingi ninapohubiri ujumbe wangu wa kwanza kwa maskini ni ‘AMANI’ nilikuwa nikihubiri katika Kanisa kubwa nyingi Korea MUNGU akasema na mimi juu ya AMANI, na ninapohubiri AMANI mambo mengi makubwa yalitokea, je unajua familia nyingi Duniani hawana AMANI? Nchi n.k.

Ibilisi amesababissaha kutokuwa na AMANI. Paulo analiambia kanisa la Ebrania watafute AMANI ya YESU KRISTO, alisema AMANI iwe kwenu. Unapokuwa na AMANI kwa vyovyote vile UTAKATIFU utakuijia, anaendelea pasipo hiyo hamuwezi KUMPENDEZA MUNGU.

Kwa nini nilifundisha dhambi ya kukosa UPENDO jana ni kwa sababu roho ya MAIGIZO roho ya Yuda Eskaliote imejaa Makanisani! Huko Mbinguni hatuendi kwa vyeo vyetu tunaenda kwa UTAKATIFU, ndiyo maana Anasema TAFUTENI AMANI, unajua ni kitu gani tunakikosa ? TUMEKOSA AMANI. Mahali ambapo hakuna AMANI jua kwamba na UTAKATIFU haupo, na Uangalie kwa uangalifu kwamba mtu yoyote ASIPUNGUKIWE Neema ya MUNGU, unapofika mahali Ukaikosa NEEMA YA AMANI kinachofuatia hapo ni Uchungu na huyo ndugu Uchungu anafanya kazi pamoja na ndugu Matatizo, wengi ni Wasikivu wazuri lakini HAWATENDI kama NENO linavyosema, ndipo YESU Anasema ‘’Heri wenye Moyo safi’’ . UTAKATIFU unaambatana na AMANI, ukiishi kwa AMANI Duniani UFALME WA MUNGU utaishi Milele na Milele, wakati fulanii nilikwenda Uganda kuhubiri huko na nikaenda mji moja huko uitwao Mwenge, nikawa na washirika 4 kwa Mwaka mzima, Sadaka wakati mwingine shs 20 nikamwambia MUNGU nataka kurudi Kenya nikasikia sauti ya MUNGU ikasema “ NIMELIPA GHARAMA” kwa ajili ya BARAKA ZAKO, wengine mnataka MBARIKIWE lakini hampo tayari kulipa Gharama!!, nikaamua kwenda Mlimani kuomba kwa muda wa siku 4, siku ya kwanza mbu walikuwa wengi sana, siku ya 2 mvua, siku ya 3 Simba akaunguruma, siku ya 4 ndipo nikasikia sauti ya MUNGU ikisema “TULIA kuanzia Leo utakwenda katika Mataifa mengi kutangaza UZURI WA BWANA na UFALME” nikashuka . Sasa nilipolipa gharama nikarudi palepale kwenye mti, Mwanzo nilipokuwa nikihubiri kule mwenge nilihubiri ujumbe huu, mwanzoni nilikuwa Nikihubiri hawakuja watu, lakini baada ya kulipa gharama nilikwenda kuhubiri watu wengi walifunga maduka yao na kuja na WAKAOKOKA, wengi zaidi siku ya pili wakaja, nilialikwa kwenye Kongamano mahali Fulani, walikuwa ni watu wa Dini, nilipofika pale nilianza kupiga piano, ROHO MTAKATIFU akashuka, watu walikuwa hawajawahi kunena kwa Lugha, lakini Siku hiyo wote walianza kunena kwa Lugha hata bila kuwekewa mikono na kuombewa, Mchungaji wa pale baada ya kuona hayo alinichukua na kuniambia toka nje, Mchungaji Yule akanichukua na kunitupa nje. Niliendelea na huduma, nayo ikazidi kujulikana na kukua na kutambulika huko Uganda nilipoanzia.

Chochote unachofanya uwe na tabia ya mtu ALIYEOKOKA Ukilichukua NENO la MUNGU kama lilivyo, wakati tulionao ni wakati wa kufikiria UTAKATIFU, YESU alisema Neno Mathayo 5:9 (Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana MUNGU), tunawapatanishi wangapi hapa?, nilipokuwa Israeli nilisimama palepale YESU alipokuwa akiwahubiria watu, nililia sana, Wamebarikiwa wanaowapatanisha watu. Jana niliwaambia Luka 21:25 maneno aliyoyasema YESU, 90% yamekamilika.
Zab. 34:14 Kama una uovu wowote huwezi ukaenda mbinguni, ni nani Anaekujua? sio Mtume wala mtu yeyote ila ni MUNGU mwenyewe, Unajua nini kinakuzunguka katika maneno, katika mawasiliano yako,
Kama wewe ni mtu unayetoa amri tu nyumbani na hutaki AMANI nini maana ya NENO, fuatilia yaani tembea nayo mstari wa Zab 118: 5 Nalimtafuta BWANA nae alinijibu,…

MUNGU Ametupa uwezo wa kuchagua, una uwezo wa kujitawala, YESU alisema AMANI nawaachieni, wengine wenu hapa unatakiwa umeze panado kwajili ya kichwa, magonjwa mengi yanataka AMANI ili yasikusumbue, kile unachokiwaza kinaweza KUKUCHIMBIA kaburi lako au KIKAKUFUNGULIA Mbingu,
Wengi mkifika sehemu za chakula mnawasumbua watu leteni chakula, wengine mnachimba makaburi yenu wenyewe, unapokuwa una AMANI unaweza kula sahani moja tu, lakini ukiwa hakuna AMANI unakula ovyo ovyo, AMANI ni dawa, itakufungulia Uwezo, itakufanya watu Wakutegemee, kwa sababu wewe una AMANI. Mimi popote ninapokwenda ninatangaza AMANI na mialiko mingi katika nchi wananiambia mimi ni mtu wa AMANI kwa sababu napenda kuhubiri AMANI.

Warumi 14:17,19 Ufalme wa MUNGU siyo kula na kula, jumlisha AMANI na furaha katika ROHO MTAKATIFU, unasemaje umepokea ROHO MTAKATIFU lakini wewe siyo mtu wa haki na AMANI, kama Kanisa la leo tukiamua kuongelea AMANI

Zab.85:5 (Nitasikia BWANA Anasema nini…) hebu fuatisha MUNGU Anachokufundisha katika kusanyiko hili, NENO hili linaweza kukufungua asubuhi ya leo kwa kusikiliza na kuamua, Utafunguliwa. Wakati umewadia kwa watumishi, ni Kulishughulikia swala la AMANI. Kuanzia leo uwe ni mtu wa AMANI na utakuwa mshindi. Watu watakuja kwako ili kupata AMANI uliyo nayo. Nina jumbe tofauti ninapofika kwenye ujumbe wa AMANI .

Yoh.14:27,. Je unataka kuwa Milionea? AMANI iwe pamoja na Wewe, unataka mafanikio? AMANI iwe pamoja na wewe. Wachungaji mnataka kuona mtu akifunguliwa mkiwaombea? AMANI iwe pamoja na ninyi. Je mnajua siri ya EFATHA? Apostle ni mtu wa AMANI, nimeshakutana na watu wengi sana.
Hes. 12:3 unajua Musa alikuwa ni mtu wa tabia gani? alikuwa ni mtu wa UPOLE ndivyo mtumishi MWINGIRA ni mpole, siri ya EFATHA kufanikiwa ni kwa sababu Mwanzilishi wake ni MNYENYEKEVU na ni mtu wa kutaka AMANI sana.

Ninakupa AMANI, YESU Alisema siyo kama vile Dunia inavyowapa, TANGAZA AMANI POPOTE UNAPOKUWA.
 
 

Breaking News:'' Mtoto wa Pili leo amezaliwa katika Hospital yetu ya Mashangilio katika mji wa BWANA MUNGU Wetu MKUU Kibaha Precious Centre, Mtoto amezaliwa na Kg 4, mtoto amezaliwa saa kumi na moja alfajiri, jina lake ni Sophia Wambura"

Asante YESU BWANA, Tunamshukuru MUNGU Wetu BABA MKUU kwa Matendo yake Makuu yanayoendelea Kwetu Wana Efatha, Asante YESU BWANA.

Tuesday, October 8, 2013

SIKU YA TATU YA KUSANYIKO LA EFATHA 2013

 Haleluya,... Utukufu na Uwepo wa MUNGU na NGUVU ya MUNGU WETU MKUU ikitawala ndani ya Madhabahu ya Kitume na Kinabii ya BWANA MUNGU Wetu MKUU, Kibaha Precious Centre.


 Haleluya,... Kusanyiko la BWANA MUNGU Wetu 2013 Kibaha Precious Centre linaendelea, NGUVU za BABA Yetu MUNGU MKUU Zikionekana na Kutawala...


 Watumishi wa MUNGU Wachungaji Viongozi na Wa Vituo...


  Mtumishi wa MUNGU, Mchungaji Kiongozi Efatha Ministry- Kenya Mchungaji Kikoti, akiwasindikiza kabila la Wahehe kutoka Iringa, wakimwadhimisha MUNGU WETU MKUU katika kusanyiko la BWANA 2013 Kibaha Precious Centre.

 
Mwanamuziki Jane Misso akimuinua MUNGU Wetu MKUU kwa Nyimbo za Sifa na Kuabudu katika Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu MKUU Kibaha Precious Centre 2013.


Oooh Haleluya,... MASHANGILIO.

 
Ndani ya YESU BWANA Wetu Ni FURAHA, AMANI TELE, Haleluya!!!

 
  OOooh Haleluya,... Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU WETU Aliye HAI, MUNGU MKUU,... Mwaka wa Mashangilio... Mh. Naibu Waziri Lazaro Nyarandu akiwa na Furaha na Amani mbele ya Madhabahu ya KItume na Kinabii katika Mji Mtakatifu wa BWANA MUNGU WETU, Kibaha Precious Centre, Akicheza na Kusifu mbele za BWANA MUNGU Wetu MKUU, Astahiliye YEYE KUCHEZEWA na KUTUKUZWA na KUABUDIWA PEKE YAKE, PEKE YAKE MUNGU BABA MKUU, Haleluya Asante YESU, Asante BWANA.


 Mh. Naibu Waziri Lazaro Nyarandu Akimchezea na Kumwimbia MUNGU WETU na BABA YETU Aliye MKUU Aliye HAI,... Asante YESU!

 Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mh. Lazaro Nyarandu akiwa katika Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU WETU Aliye HAI MKUU,... pichani Mh Naibu Waziri akiwa na Watumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira.

 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwa pamoja na Mh. Naibu Waziri Lazaro Nyarandu, Mh. Waziri Akiwasalimia Wana wa MUNGU Wana Efatha katika Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu 2013 Kibaha Precious Centre Mji Mtakatifu wa MUNGU Wetu MKUU. Mh. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu akiwa Precious Centre Kibaha katika Mji wa BWANA MUNGU Wetu MKUU.
  Don't do like Others, Do like JESUS. (Now from Kibaha Precious Center: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kipindi cha Mafundisho kinaendelea...)


Mtumishi wa MUNGU Mchungaji Tumpe Laban toka Arusha.
 Wana wa MUNGU wakiwa katika Utulivu wakisikiliza Mafundisho na Mahubiri katika Kusanyiko KUU la BWANA 2013, linaloendelea Kibaha Precious Centre, Tanzania.

 Asante BABA, Asante MUNGU WETU MKUU, Asante YESUUU, Asante ROHO MTAKATIFU,... Huu ni Mwaka wa MASHANGILIO 2013,... Oooh Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu Kibaha Precious Centre, Tanzania,... Asante YESU.

 Haleluyaaaa, BARAKA za MUNGU wetu na BABA YETU MKUU Zinazidi kumiminika na Kuendelea kwa Wanawe,... YEYE Ni UPENDO, AMANI, FURAHA, USHINDI, NGUVU, MAMLAKA ILIYO JUU na KUU SANA, Haleluya,... MUNGU YU HAI, Hakuna MUNGU MWINGINE KAMA YEYE, MUNGU PEKEE, MUNGU MTAKATIFU MKUU SANA, Haleluya,... Asante YESU, Asante BWANA,.. Huu ni MWAKA WETU WA MASHANGILIO.

Kibaha Precious Centre Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu MKUU Laendelea,... Tunawakaribisha Wote ambao bado hamjafika katika Mjii huu Mtakatifu, Mahali hapa Nyumbani mwa BWANA MUNGU WETU MKUU, MZURI MNO,... Haleluya. Njooni na Ndugu zenu, Rafiki, Jamaa na Wote wenye Mapenzi Mema,.. Mje Mkutane na BWANA MUNGU WETU ALIYE HAI, Haleluya na MKUU MNO... Ooooh YESU ni MZURI, YESU ni MZURI.

MUNGU Awabariki Nyote,... Na Jumatano yetu Tunaibariki!!!.