Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Friday, September 27, 2013

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

''MUNGU Anasema, “Wenye Haki wana mateso mengi”! Watu watasema, mbona huyu ana shida sana, mbona yuko hivi na hivi….waambie ni kweli maana wenye haki wana mateso mengi! Wayahudi ni watoto wake MUNGU, na MUNGU Alimwambia Ibrahim Atambariki na Watoto wake wote lakini wakawa Watumwa katika Nchi ya Misri. Wakamlilia MUNGU katika shida zao, katika maangamizo yao Wakamlilia BWANA kwa miaka 400 na BWANA AKAWAOKOA.

“Usione nina mateso mengi, yupo ANAYEKUJA KUNIOKOA”!

N.B. Kutoka Kanisa kwenda Kanisa, kwenda mikutano mbalimbali ya maombi HAIWEZI Kukutoa kwenye Matatizo mpaka UTAKAPOAMUA KUTOKA KWENYE TATIZO, Mpaka UTAKAPOAMUA na KUAMINI na KUKUBALI KWAMBA HAKI yako INATOKA kwa MUNGU na UNAIPATA kwa Sababu YESU KRISTO AMEKUFA KWA AJILI YAKO na AMELIPA DENI ZAKO ZOTE (Hapo ndipo UTATOKA KWENYE TATIZO).

Lakini bila ya kuelewa hivyo, utazunguka Makanisa mengi na Utaombewa na hilo tatizo Halitatoka mpaka utakapotambua Haki hiyo utaipataje na hayo mateso yamekujaje na yanaondolewaje.

(Maneno haya Matakatifu, Makuu Yenye HEKIMA na UFAHAMU Yataendelea)
Mwana wa MUNGU huu ni wakati wako wa KUTOKA, USIKUBALI Tena, Ni wakati wako Mwana wa MUNGU KUTOKA, ni wakati WAKO.
BWANA Akakuridhie.”

KUWEKWA WAKFU MBELE ZA BWANA

Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira, akiongea na Wana wa MUNGU kabla ya kuanza kuwaweka Wakfu wanae kwa ajili ya BWANA


 Mtumishi wa MUNGU Joshua Josephat Elias Mwingira, akijibu SWALI Aliloulizwa ''KAMA YUKO TAYARI KUMTUMIKIA MUNGU BWANA WETU na BABA YETU",... Joshua ALIJIBU "YUKO TAYARI KUMTUMIKIA MUNGU WETU na BABA YETU ALIYE MKUU"

  

 Mtumishi wa MUNGU Anna Josephat Elias Mwingira, akijibu SWALI Aliloulizwa ''KAMA YUKO TAYARI KUMTUMIKIA MUNGU BWANA WETU na BABA YETU",... Anna ALIJIBU "YUKO TAYARI KUMTUMIKIA MUNGU WETU na BABA YETU ALIYE MKUU"

 Wana wa MUNGU Joshua na Anna wakiwa wamepiga magoti tayari kwa Kupakwa Mafuta kwa ajili ya UTUMISHI kwa MUNGU WETU BABA ALIYE MKUU na MMWEMA Sana.


 Wana wa MUNGU wakiwa wamepiga magoti kwa Unyenyekevu tayari kwa UTUMISHI.

Thursday, September 26, 2013

KUSANYIKO KUU LA BWANA 2013 LIMEKARIBIA

Mtumishi wa MUNGU Natushila akionyesha Vazi la Kanga, ambalo linafaa kwa Watu wote, Wakina baba wanaweza kushona Vitenge... Ni Vazi Zuri la Kusanyiko hili la Baraka tele kwa MUNGU wetu ALIYE MKUU na MUWEZA

 Haleluya,... KUSANYIKO KUU LA BWANA 2013 Limekaribia,... Kibaha Precious Centre, Tanzania. Wana wa MUNGU Tusikose Baraka hii Aliyotujalia MUNGU WETU MZURI.

''Watumishi wa MUNGU akiwapo Suzy Msofe wakionyesha Mavazi yenye NGUVU ya MUNGU WETU MKUU ya Mwaka huu 2013''


Monday, September 16, 2013

SHUHUDA SHUHUDA SHUHUDA.


MUNGU Wetu na BABA Yetu ni MZURI MNO, Anatupenda sana Wanawe,... Katika YESU KRISTO Bwana na Mwokozi wetu, MUNGU WETU MKUU wa EFATHA,...

Wana wa MUNGU hawa Jane na Denis Mr & Mrs, waliamua leo kuja mbele za Wana wa MUNGU, mbele ya Hema ya BWANA kuja Kushuhudia Matendo MAKUU ya MUNGU WETU na BABA YETU MKUU Aliyowatendea katika Maisha yao. Walioana miaka 5 iliyopita, Lakini katika miaka yote hiyo Hawakuweza kufanikiwa kupata Mtoto, Hospitalini waliambiwa kuwa HAWAWEZI Kupata MTOTO KAMWE, Kwani Hawana MBEGU ZA KUZALISHA Watoto,... Madaktari waliwapima na kuwapa majibu hayo kila Hospitali mbalimbali walizokwenda kutibiwa.

Lakini Hawakukata tamaa,... Walimwamini MUNGU wetu MKUU, MUNGU wa EFATHA kuwa ATAWAPA Watoto,... Kwenye Kusanyiko la wana wa MUNGU la Mwaka jana 2012 Kibaha Precious Centre, Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira aliita Wale wote ambao Hawajapata watoto ili Awaombee,... Huyu mwana wa MUNGU Jane alitoka mbele na kuombewa,... Haleluya... MUNGU wetu BABA wa Efatha SI MUONGO, HASHINDWI KITU,... YEYE ni MUWEZA Wa YOTE, Kila kitu KINAPATIKANA KWAKE Haleluya,...

Oooh Haleluya, ... Leo Wametoka mbele na Kushuhudia MATENDO MAKUU Ya MUNGU WETU na BABA YETU MKUU Wa Efatha,... Wamepata Mtoto,... Ambao Waliambiwa na Madaktari na Wataalamu katika Mahospitali mbali mbali kuwa KAMWE Hawatapata Watoto, lakini LEO Kupitia MUNGU MKUU, MUNGU MUWEZA Wa EFATHA AMEWAPA Watoto kwa JINA la BWANA na MWOKOZI wetu YESU KRISTO,...

Tunamshukuru MUNGU wetu na BABA YETU kwa BARAKA HII, Haleluya katika YESU KRISTO Bwana Wetu.


Haleluya,... MUNGU Wetu na BABA YETU ni Mzuri sana, Anatupenda sana Wanawe
Kijana huyu mwana wa MUNGU, leo aliamua kuja Kushuhudia mbele za Wana wa MUNGU na Mbele za Madhabahu ya MUNGU wetu MKUU, juu ya Matendo Makuu ambayo MUNGU wetu BABA Amemtendea katika Maisha yake,... Kijana Mwana wa MUNGU (Denis Malesela) anashuhudia kwamba, kabla hajaamua Kumpokea BWANA wetu YESU KRISTO Kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yake (Kuokoka) alikuwa ni Mlevi sana, Alianza kunywa pombe toka akiwa darasa la tatu, Bibi yake alikuwa anapika pombe kwa hiyo alikuwa anampatia mjukuu wake asubuhi kabala ya kwenda shule na hata akirudi shule.

Kwa hiyo Denis akajikuta roho ya ulevi imemwingia, na hiyo roho imemtesa sana, kwani alikuwa Anakunywa pombe na kupigana na watu, na hata ilifikia pointi akawa anapelekwa polisi na kuwekwa sello kwa sababu tu ya pombe,... Pombe ilimtesa sana.

Denis akaendelea kushuhudia kuwa, ... baada ya Mjomba wake kumshauri na Kumuhubiria Habari Njema za BWANA Wetu YESU KRISTO, na kumleta EFATHA,... ndipo alipoamua KUOKOKA na ... KWELI YESU WETU HADANGANYI,... Bwana wetu YESU KRISTO Alimbadilisha maisha yake na Kumfanya AWE KIUMBE KIPYA, ... na toka siku hiyo POMBE ALIACHA na HANYWI TENA, na Sasa Amekuwa Kijana Mzuri na Anatenda Vema sasa,... na Yuko na Amani na Furaha katika Maisha yake sasa,... Haleluya.... MUNGU Wetu na BABA YETU Ni MZuri sana, YESU ANATUPENDA, ANATUPENDA Sana, Hakuna Jambo GUMU Kwa Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO,... Haleluya.

USHINDI ni kwa MWANA KONDOO ALIYE HAI... YESU KRISTO MFALME Mwana wa MUNGU, Mwana wa BABA, MUNGU WETU MKUU Aliye HAI.


Saturday, September 7, 2013

SIKU YA KUJONGEA HEMANI MWA BWANA

Kesho ni Siku ya JUMAPILI, ni Siku ya kujongea Hemani mwa BWANA MUNGU Wetu MKUU ALIYE HAI,... ni siku ya kuwa Nyumbani mwa BWANA BABA YETU MUNGU MKUU... Haleluya Tukimsikiliza Mtumishi wake Mpenzi Mkalimani wetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akitupa Siri na Ufunuo wa BABA MUNGU WETU MKUU ANAYETUPENDA SANA Wanae,... Haleluya, BARAKA, SIFA, UTUKUFU, UKUU Ni Wake YEYE ALIYE PEKE YAKE MUNGU WETU MKUU.

Amani Iwe Nanyi Katika Kujongea Mbele za BWANA MUNGU Wetu, ... Tutazame Mioyo Yetu Isije Ikatufungia YALIYOMEMA TOKA MADHABAHUNI PAKE, Haleluya...

USHINDI Ni Wake MUNGU WETU MKUU, BARAKA na UTUKUFU Ni ZAKE Haleluya ...

Msikose Kuja Kupokea YALIYO MEMA YA MUNGU WETU MKUU Toka Madhabahuni Pake, Haleluya.

Tuesday, September 3, 2013

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).


''Hebu fuatia kisa cha mmoja wa Mitume wa BWANA YESU. Yuda Iskariote, alikuwa mmoja wa mitume 12 wa awali ambao BWANA YESU aliwateua miongoni mwa wengi Waliomfuata. BWANA YESU, Alijitenga ili Aombe kwa MUNGU usiku kucha peke yake ndipo Alipofanya Uteuzi wao. Bila shaka alifanya hivyo ili apate Hekima ya kuchagua watu walio sahihi. (Luka 6:12-16). Tena Yuda Iskariote, alipewa kutunza hazina ya Huduma, ikimaanisha kuwa alihakikishwa katikati ya wengi walioteuliwa. Baada ya mafunzo ya Huduma ya BWANA YESU, Mitume hawa walihitimu na kutumwa peke yao kwenda kuhudumia watu Dhidi ya mapepo wote, maradhi yote, na Kutangaza Ufalme wa MUNGU. Yuda alikuwa mmoja wao, ikimaanisha kuwa alikuwa na Sifa zilizotakiwa (Luka 9:1-6) (Inawezekana kabisa kuwa YESU Alijua fika Yuda alikuwa na MOYO MBAYA lakini Alimchagua ili ATUFUNDISHE JAMBO Fulani).

BWANA YESU na Mitume walivyoendelea na Huduma, yalizuka maswali ya faida gani watapata kwa kumfuata YESU na Huduma yake, hasa kwa kuwa wameacha vyote kwa ajili yake. Hapa inamaanisha mitume walitoa na kuacha vyote kwa ajili ya Huduma na Hawakuwa na chao tena bali vyote vilikuwa ni vya Shirika. Hapo BWANA YESU Alitoa masharti ya anayetaka kumfuata, kuwa ni lazima ajikane mwenyewe na abebe msalaba wake kila siku. Tena akaendelea kutahadharisha juu ya watu wanaongalia nyuma, kuwa hawafai kwa Ufalme wa MUNGU, (Luka 9:23-27,62). Akasisitiza juu ya mtu anayetaka kumfuata ahesabu Gharama kabla ya kuanza kazi (Luka 14:25-35, 18:18-30). Yuda ALIKUWEPO Anasikia.

Pamoja na Heshima yote hii, bado MOYO WA YUDA Ulikuwa SIYO MWAMINIFU wala MTAKATIFU, Kwa sababu, Alifikia mahali pa kuonyesha wazi Hila yake. Alijifanya ana Uchungu na Maskini, ALIPOONA Kiongozi wa Huduma BWANA YESU, ANAPAKWA MARHAMU YA BEI KUBWA. “YESU Alipopakwa marhamu ya nardo safi, Yuda Alihoji kwa nini Isiuzwe ili Fedha yake Wapewe maskini, si kwa KUWAHURUMIA bali kwa kuwa ni Mwivi, na ndiye Mshika Mfuko wa Huduma Akivichukua Vilivyomo humo” (Yohana 12:3-6). Ukosefu wa Uaminifu ULITHIBITISHWA baada ya Kifo chake, kwani ALIKWENDA KUJINYONGA katika Konde ALILONUNUA kwa Ijara ya Udhalimu; wakati Akiwa katika Utumishi. Tunasoma “Alianguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka” (Matendo 1:18)''.

(NENO Hili litaendelea....)

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

''Watu wengi wameumizwa na marafiki wa karibu kwa sababu hawakujua wanawawazia nini kila siku. Tunashuhudia Serikali zikipinduliwa na Marafiki miongoni mwa kundi hilo hilo, pia Mauaji ya halaiki yakifanywa na watu wanaofahamiana, kwa sababu Moyo wa Mwanadamu ni mdanganyifu. Siyo rahisi kufahamu anachowaza wakati wowote. Tunasoma, “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; Nani Awezaye kuujua?” (Yeremia 17:9). Moyo hubadilika kila wakati kutegemeana na mazingira na mazoea ya mtu aliyojijengea. Wapendanao wanaweza kufarakana vikali na chuki ya kutisha kuibuka kwa sababu ya moyo!. Mtu bila KUJIJUA, anaweza kuwa na Kijicho, Hila, Matusi, Ukorofi, Kiburi, Upumbavu n.k. mambo ambayo ni MATUNDA ya Moyo. Ndani ya moyo wa Mtu hutoka Mawazo mabaya, Uasherati, Wivu, Uuaji, Uzinzi, Husuda na Kadhalika. Maovu haya yote yanamtia mtu Unajisi, ni VIZURI KUYASHUGHULIKIA. Biblia inasema; “Akasema, kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi” (Marko 7:20 -23). Pia ndani ya Moyo panaweza kuzaliwa “TUNDA LA ROHO ambalo ni Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, Utu wema, Fadhili, Uaminifu, Upole Kiasi,” (Wagalatia 5: 22-23)
Mfano: Nyakati za BWANA Wetu YESU KRISTO, baadhi ya Wanafunzi wake wa karibu kabisa walikuwa wakiwaza mambo asiyodhania, japokuwa BWANA YESU ALIWEZA kupambanua mawazo ya Mioyo ya watu. Wengine waliwaza juu ya nafsi zao katika kundi kuliko kuwaza jinsi ya kudumisha Huduma ya BWANA wao, na wengine walifika mbali zaidi hata Kumsaliti kwa fedha. Pia nyakati za Matendo ya Mitume baadhi ya watu waliookoka, wapo waliotamani vipawa vya ROHO MTAKATIFU kiasi cha Kutaka Kutoa RUSHWA, mfano Simion (Matendo 8: 18-24) Ukifuatilia mfululizo wa Safari ya Huduma ya BWANA YESU hapa duniani, Utabaini kuwepo kwa Vituko vya aina aina vinavyoonyesha Moyo wa MTU ULIVYO WA KUSHANGAZA. Ndiyo Maana ni MUHIMU SANA MTU KULINDA MOYO WAKE Kuliko Vitu Vyote.''

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

ANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

''Biblia inatuambia kuwa, bila kujali uwezo wako wa kusali au mahali unaposali, yako maovu yanayokushuhudia ya kuwa umepungua. Tunasoma, “Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya Jina lako, Ee BWANA! Maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi, tumekutenda dhambi.” (Yeremia 14:7) Maovu yetu yanatushuhudia kwa sababu moyo wetu umeiacha sheria ya MUNGU na kushika mapokeo ya wanadamu. Na hicho tulichokipokea ndicho kinachotushuhudia leo.

- Mfano:- Moyo una maandalio, au kitu unachotafuta lakini mara yanapotokea matatizo mtu huyu anaweza kufuta kila kitu chema kutoka kwa MUNGU kutokana na jinsi anavyo kabiliana na changamoto hizo Imeandikwa, “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, lakini jibu la ulimi hutoka kwa BWANA” (Mithali 16:1). Biblia inatufundisha kuwa wakati wana wa Israeli walipokuwa wakirudi katika nchi yao ya ahadi kutoka utumwani Misri, njiani jangwani walitamani kula nyama. Badala ya KUSHUKURU na KUOMBA MUNGU awape nyama, wao walimnung’unikia MUNGU hata kunena vibaya mbele zake wakisema heri warudi Misri kwa masufuria ya nyama, pilau na vitunguu saumu. MUNGU akawakasirikia akawapa nyama nyingi za kwale lakini kabla ya kula aliwaangamiza. Je wewe unatamani nini hata kumnung’unikia MUNGU?. Inatupasa TUTOKE katika hali tulio nayo, ya moyo uliotawaliwa na utu wa kale na kumrudia MUNGU ili Atufikishe pale ALIPOTUKUSUDIA.''


UWEPO NDANI YA KANISA SEPT 1

  Ni Wewe tu BABA Uliye MUNGU wetu, Hakuna Mwingine...


 Ni BABA YETU TU, Asante MUNGU Wetu...


 Uwepo wa MUNGU.


 Asante MUNGU Wetu...


Wana wa MUNGU wakifuta Machozi,.. si Machozi ya Kupigwa Hapana...

 
 YESU BWANA Wetu, Tunakupenda..


 Wana wa MUNGU wakiwa katika Roho wakiongea na MUNGU BABA Yetu,... si machozi hayo ya kufiwa au kupigwa bali ni UWEPO NDANI YA KRISTO YESU BWANA Wetu.TUNAKUA NDANI YA KRISTO

  UPENDO wa BABA MUNGU WETU kwa Wana wa MUNGU Watoto Wake...


  Waacheni watoto waje kwangu, Wala MSIWAZUIE.


Watoto wakiwa na Upako, NGUVU ya MUNGU wetu MKUU wakiwaombea Wana wa MUNGU Watu Wazima,... Je Wewe Mzazi, Mlezi, Upendi Mwanao Awe na Katika Upako NGUVU ya MUNGU Wetu Hii?...


Kwa JINA LA YESU KRISTO wa NAZARETH,... mapepo yanakimbia, Watu wanaponywa, vifungo vinafunguka, Watu wanawekwa HURU... OOooh Jamani YESU NI MZURIII.

 
 Waleeni watoto katika Misingi ya IMANI, nao Watakula Mema ya Nchi,...


 Wazazi, Walezi... Msikose kuwa na Watoto wenu Hemani mwa BWANA,... kwani Kumcha BWANA ndio chanzo cha Maarifa... Je Hupendi mwanao awe na Maarifa ya MUNGU wetu MKUU?,... Sunday School zipo Mahali pote Efatha Ministry,... Mkuze Mwanao ndani ya KRISTO BWANA, ili HOFU YA MUNGU WETU MKUU IUMBIKE NDANI YAKE,... Naye Atakuwa katika BWANA... 
 Haleluya, Usikose kutenda Vema nawe Uta....
 Watoto wakicheza mbele za bwana,inapendeza sana watoto kukua ndani ya yesu.


Ni Raha sana na BARAKA Mtoto Akikua katika Kumjua MUNGU Wetu.Kububujika mbele ya bwana,inapendeza.