Posts

Showing posts from 2013

WANA WA MUNGU WAFUNGA NDOA (MOROGORO)

Image
Wana Ndoa wakiwa wamepiga Picha ya pamoja (Ndoa 26 zilizofanyika jana Tarehe 25/December/2013, EFATHA MINISTRY Morogoro) .   Wana wa MUNGU Wana Ndoa (Ndoa 26 zilizofanyika jana Tarehe 25/December/2013, EFATHA MINISTRY Morogoro) Wakionyesha Vyeti vyao vya Ndoa, Baada ya Kufunga Ndoa jana.

USIKU WA EFATHA

Image
USIKU WA EFATHA, 31 DECEMBER 2013 Kibaha Precious Centre, Tanzania katika Mji wa BWANA MUNGU WETU MKUU, Usikose Mwana wa MUNGU.

HALELUYA,MUNGU WETU NI MZURI

Image
Haleluya,... MUNGU wetu ni Mzuri, YESU wetu ni Mzuri, Tuna kila sababu ya kumwambia MUNGU Aliye BABA Yetu ASANTE, Leo Jumapili ilikuwa ni Siku nzuri sana kwa Wana wa MUNGU, Kwani BWANA wetu YESU KRISTO kupitia ROHO MTAKATIFU kwa Watumishi w ake waaminifu (kuanzia Dar es Salaam Mwenge mpaka vituo vyote) Alitupatia Chakula cha Kiroho kizuri sana, Tulilishwa vya Kutosha, YESU Anatupenda sana, ndio maana Alitupa chakula kizuri cha Kiroho ili Tutoke mahali tulipo na kwenda kwenye Utukufu, na kwenda kuwa Huru... Kwa kweli MUNGU Wetu MKUU ni Mzuri sana, Anatupenda Wanawe. Wana wa MUNGU wakitoa SADAKA ZA SHUKRANI kwa yale yote Mema Makuu ambayo MUNGU Amewatendea kwa wiki nzima, pamoja na ZAKA na Ya kutangaza INJILI pamoja na MASHANGILIO mbele ya Madhabahu ya BWANA MUNGU WETU MKUU. Kipindi cha SHUHUDA, Wana wa MUNGU walitoka mbele na Kushuhudia Mambo Makuu ambayo MUNGU WETU MKUU, MUNGU Wa EFATHA MINISTRY Aliwatendea katika Maisha yao, ATUKUZWE na KUINULIWA Aliye BWANA MUNG

UTAJUAJE UMEKOMBOLEWA?

Zab 1:3 “Kila Alitendalo litafanikiwa”, Ayub 22:28 “Nawe Utakusudia Neno nalo litathibitika kwako”. Ayub 22:21 “mjue sana MUNGU ili uwe na amani, ndivyo mema yatakavyokujia. Hatua ya kama UMEKOMBOLEWA kila unachokifanya Kinafanikiwa. UKOMBOZI ni kwa ajili ya Mafanikio yako hapa Duniani siyo Mbinguni. Usikubali kufa kabla ujafaidi maisha hapa duniani, Usikubali kujitiisha kwa adui eti kwasababu shida fulani, bali JITIISHE kwa MUNGU awezaye kukushindia shida zote. :- Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira.

IBADA YA JUMAPILI DEC 15, 2013.

Image
Haleluya,... MUNGU Wetu ni MZURI SANA, YESU Wetu ni MZURI SANA. Tunamshukuru BWANA wetu kwa Ibada nzuri iliyokwishamalizika, Chakula cha Kiroho kilikuwa kitamu sana, BWANA Wetu Alitulisha vema, Alitugusa katika Mahitaji yetu, Aliona Mioyo y etu Inahitaji nini, BWANA Alishuka na Kutuponya, Alishuka na Kutuweka Huru, BWANA Alikuwa nasi kupitia Mtumishi wake Mchungaji Kiongozi wa EFATHA MINISTRY Arusha, Mchungaji Tumpe Rabarn. ''Kazi ya MUNGU BABA ni KUKUTUKUZA''   ''DAI MASHANGILIO YAKO kwa kuwa Wewe ni wa UZAO WA EFATHA.'' :- Mchungaji Kiongozi Efatha Ministry Arusha, Mchungaji Tumpe Rabarn.   “Wakati adui anakaa kikao na kupanga Kukuharibu; MUNGU naye Anaongea na Watumishi wake, Anapanga KUKUINUA na KUKUTUKUZA”

KAMBI YA VIJANA KIBAHA PRECIOUS CENTRE Dec 2013

Image
Vijana wa YESU, Vijana wa Efatha siku ya Kwanza walipokuwa wakielekea Kibaha tayari kwa Kambi yenye NGUVU ya MUNGU Wetu MKUU...     Mojawapo wa Watumishi wa MUNGU Wapakwa Mafuta wa BWANA MUNGU Wetu, wanaohudumu katika Kambi hii. Mtumishi wa MUNGU akitoa Mafundisho yenye UPAKO WA NGUVU YA MUNGU Wetu MKUU kwa Vijana walioko Kambini Kibaha Precious Centre. Wana wa MUNGU Vijana wa YESU KRISTO wa Efatha, wakipokea Mafundisho na Mahubiri na Maneno yenye Hekima na Ufahamu pia wakihudumiwa Kiroho .... Efatha:Healing & Deliverance by the Blood of JESUS CHRIST... Haleluya!!!

CHAKULA CHA ROHONI

umb 29:29 “Mambo ya siri ni ya BWANA MUNGU wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu na watoto wetu milele, ili tufanye maneno yote ya sheria hii. Mambo ya siri ni ya BWANA, wana wa Israeli walipokuwa utumwani Misri walitumikishwa na kuteseka sana lakini walipokuwa njiani wakiongozwa na Musa, kwa shida ndogo walitamani kurudi Misri (walitamani mambo ya nyuma, maisha ya nyuma). Kama HUJAKOMBOLEWA unawaza mambo matatu tu, KULA, KUVAA na KULALA. Wezi wote wala rushwa, mafisadi wanaiba ili Wale, Wavae vizuri na kujenga Majumba ya kifahari ili Walale. Huyu bado hajakombolewa. :- Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira.

SIKU YA KUJONGEA NYUMBANI MWA BWANA (ya kumsikiliza mkalimani wetu)

Wapendwa karibuni  tujongee nyumbani mwa bwana kesho siku ya jumapili,ibada ni kama ifuatavyo: IBADA YA ASUBUHI-INAANZA SAA MOJA ASUBUHI IBADA YA MCHANA-INAANZA SAA TANO  ASUBUHI Karibuni wote!!! (wawili au watatu wakusanyikapo kwa ajili ya jina langu,nami nitakuwa pamoja nao). sasa sisi tu zaidi ya watatu je hatoshuka?????
Kwa sababu wewe sio ulioniita, Oooh Haleluya, Aliyeniita YUKO HAPO JUU na ANANIANGALIA, Jinsi ninavyotembea huku Duniani, NAKANYAGA pepo kushoto, nakanyaga jini kulia, nikitembea mapepo yanalaza mbio, wachawi wanatawanyika, Maana nina Upako wa KIFALME, na WEWE POKEAAA. :- Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira.
umewekwa juu pamoja naye (YESU KRISTO Bwana wetu) katika Ulimwengu wa Roho. Kwa hiyo tumeketishwa na MSHINDI, hapa hoja ni USHINDI. Kanisa la YESU KRISTO lazima liweke Records (kumbukumbu), Usiishi kama msindikizaji... lazima Uweke records, wewe ni Mshindi, Sisi tunaomwamini YESU KRISTO Tunao USHINDI. :- Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira.
Image
ROHO WA BWANA Akiwa juu yako, ''UTAABUDU katika ROHO Na KWELI.''

KUMBUKUMBU YA KUSHEHEREKEA MIAKA 20 YA NDOA YA MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA

Image
  UTUKUFU kwa MUNGU Wetu MKUU,... Ni mahali pazuri Hemani mwa BWANA tunaingia kwa Furaha na Shangwe...   ''Baba na Mama Watumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat na Mchungaji Eliakunda Elias Mwingira wakiwa ndani Hemani mwa BWANA wakiingia...''   Watumishi wa MUNGU wakipongezana baada ya Kuvishana pete katika Kusherekea Miaka 20 ya Ndoa Takatifu leo.   Watumishi wa MUNGU toka nje ya Tanzania (Namibia na Uingereza) wakiwa Hemani mwa BWANA wakishuhudia sherehe ya Miaka ya 20 ya Ndoa ya Watumishi wa MUNGU Mtume na Nabii. UTUKUFU kwa MUNGU Wetu MKUU   Mtumishi wa MUNGU Mark Kariuki akihubiri katika Ibada hii,... .   Wazazi wa Mtumishi wa MUNGU na Watoto wa Mtume na Nabii wakifuatilia Ibada hemani mwa BWANA.   Pete zikiwa ndani ya Mafuta Matakatifu toka Isreal ya Mizeituni yakiyokwisha Ombewa tayari kwa ajili ya Ibada hii ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Ndoa ya Watumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat na Mchungaji Eliakund

KUPAKWA MAFUTA, UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Image
LUKA 4: 18 - 19 ''Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa''.

MAHUBIRI

Image
MAHUBIRI: MTUMISHI WA MUNGU Mkalimani Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kuhusu ''MWAKA WA MASHANGILIO'' ''Na huu ndio Mwaka wako, Utashangaa Vifungo vingine vilikuwa havieleweki na Wanadamu, hata Wewe mwenyewe ulikuwa Ukielewi, LAKINI kwa vile Amesema katika Yeremia “Kwamba Macho hayajaona wala Sikio halijasikia Mambo magumu makubwa Usiyoyajua Anaenda kuyaweka Wazi”, na Sasa Utaona Uhalisia wa kuwekwa HURU. Nina Amini kwa Moyo wangu wote, kwa Moyo wangu wote Jambo hili la Wewe kuwekwa Huru, Wengine watakasirika nalo, Wengine Watashangilia nalo. Wakati Mimi nawekwa Huru na Mkandamizo wa Kiukoo, mkandamizo wa Kifamilia, mkandamizo wa Kijamii, mkandamizo wa Kabila, mkandamizo wa Kijiinsia, mkandamizo wa namna nilivyokuwa wakati Unafunguliwa, na Nikawekwa Huru ili kuwa kama Kichekesho.'' (Yataendelea kesho Mwana wa MUNGU, Usikose huu ni MWAKA WAKO WA MASHANGILIO...)

USIKU WA EFATHA INTELLECTUALS REDEMPTION NIGHT

Image
Redemption Night Efatha Intellectuals at UDSM, Mlimani Campus.   Vijana wa YESU wakihudumu kwa Kuimba katika Usiku wa Efatha Intellectuals Redemption Night, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania Mlimani Campus.   Mtumishi Suzzana Mungy akitoa Somo na Kuhubiri katika Usiku wa Efatha Intellectuals uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania Mlimani Campus wiki iliyopita.   Wana wa MUNGU Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Efatha Intellectuals Organization wakiwa katika Usiku wa Redemption Night, Wakimuabudu na Kumsifu na Kumtukuza MUNGU wetu Aliye MKUU MMUWEZA WA YOTE.   Hawakuwa nyuma wapiga vyombo Vijana wa YESU katika Usiku wa Efatha Intellectuals Redemption Night.

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU

(Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira). NGUVU YA LAANA NA JINSI YA KUONDOKA KATIKA LAANA. Laana ni halisi na siyo kitu cha kufikirika. Laana huanza kuonekana katika kitabu cha Mwanzo 3. Laana ina nguvu na nguvu yake imesababisha watu wengi kuteseka, nguvu ya laana Haionekani kwa macho lakini huonekana katika Utendaji wake au Matokeo yake. Laana ina uwezo wa kuruhusu au kuleta au kusababisha Uovu na Uharibifu Utokee. Neno LAANA ni kinyume cha neno BARAKA. Mwanzo 3:16 “Hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako, kwa utungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala”. Kutawaliwa ni sehemu ya laana! Mwanamke kutawaliwa si hiari yake bali ni sehemu ya laana yake aliyopewa na ukikataa unaishia Kuachwa au kupewa talaka. Laana ya kwanza inamshambulia mwanamke- Kwa Utungu atazaa watoto; ule uchungu hauishii pale akizaa bali hata mtoto anapoendelea kukua hata kuwa mtu mzima yule mama bado anaendelea kusikia utungu m

SWALI LA LEO

 Wakati wa Upako (Annointing) Unatembea, Nini kinaendelea?

WORDS OF WISDOM AND FULL OF KNOWLEDGE

 (Servant of GOD Apostle and Prophet J.E. Mwingira) WHY WE FACE DESTRUCTION/ PERISH The proud oppress with a lot of intrigue. No matter how much you caution them the never change. Seek to know the LORD and they will not oppress you anymore. Pride always leads to rebellion which a key habit/ character in evil doing (one glorified in Evil doing). If one has bad feelings about himself and also utters failure to himself; this will lead him to rebellion.

MUNGU WETU NI MZURI

Haleluya,... MUNGU wetu ni MZURI Sana, daima Anatuwazia MEMA, Anatupenda sana, Bwana wetu YESU KRISTO ni MZURI sana, YEYE HATUACHI KAMWE, daima yuko UPANDE Wetu, daima yuko NASI Watakatifu wake. ROHO MTAKATIFU ni MZURI, YEYE ni MSAIDIZI wetu, Daima HUTUONGOZA, HUTUKUMBUSHA YOTE, HUTUFUNDISHA YOTE, HUTUEPUSHA na Mabaya na Hatari zote, HUTUOMBEA KUSIKOTAMKWA, Daima HUKAA NDANI YETU, Sisi ni HEKALU L AKE. Jana Jumapili Wana wa MUNGU Wana Efatha, Watanzania WENZANGU, Tunamshukuru MUNGU wetu kupitia ROHO WAKE; Tulipokea chakula kizuri sana cha KIROHO Kupitia Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira, MUNGU anatamani watakatifu wote WATOKE katika Kusetwa na yule ibilisi muovu shetani. ROHO WA BWANA Alimtumia Vizuri Mtumishi wake Mama Eliakunda KUTUPATIA UFAHAMU JUU YA MAISHA YETU YA KIROHO.

NYUMBANI MWA BWANA

Image
  Tunamuabudu BWANA wa mabwana, MFALME wa wafalme,... YEYE ALIYEMUWEZA WAYOTE.   " NENO, MAFUNDISHO, MAHUBIRI YA JUMAPILI Tarehe 27/October/2013 toka MADHABAHU YA KITUME na KINABII Mwenge Dar Es Salaam, EFATHA MINISTRY ." - Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira. “MOYO WANGU UMEJAA SHUKRANI” - Jifunze KUSHUKURU, utapata kuweza kuona mambo mapya katika maisha yako. Isaya 12:1-6 “Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeuka mbali, Nawe unanifariji moyo. Tazama, MUNGU ndiye wokovu wangu, Nitatumaini wala sitaogopa: Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni Jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa. Litajeni jina lake kuwa limetukuka……..” Unaposhikilia jambo lako katika Ulimwengu wa roho, LITATOKEA. Unatakiwa UAMINI kw

WORDS OF WISDOM AND FULL OF KNOWLEDGE

(Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira) “EVIL DOERS” After all these the bible tells us:- Psalm 27:1(The LORD is my light and my salvation; whom shall I fear? The LORD is the strength of my life; of whom shall I be afraid?) It is good when you UNDERSTAND the moment evil strikes at you, the best time for you to PRAY, the time to DESIRE ASSISTANCE, and the time to require fellow BRETHREN or ELDERS. Psalm 27:2 (When the wicked, even mine enemies and my foes, came upon me to eat up my flesh, they stumbled and fell). When Evil is directed at you, its main aim is to DEVOUR you. It is good if you UNDERSTAND what you have PASSED through, EVIL comes from people whose HEARTS are filled with HATE and when they speak the UTTER SWEETNESS. When they speak, you may think you are UNITED, but SPIRITUALLY they are FULL of EVIL. The evil are they that seek to devour your flesh. They are those who are subtle, hypocrites, witches etc. He is talking about the opp

MANENO YENYE HEKIMA

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira). ''Saa ile ile UNAPOAMINI BWANA YESU KRISTO ameingia kwako, Saa ile ile UMEPONA"

NDANI YA NYUMBA YA BWANA JUMAPILI

Image
  Mmmh... Nyumbani mwa BABA kuzuri sana,...   Watumishi wa MUNGU wakiwa Nyumbani mwa BWANA...   Wana wa MUNGU ''Mass Choir'' Wakimuimbia na Kumchezea MUNGU BABA Yetu MKUU PEKEE.   Asante MUNGU wetu MKUU BABA, Asante YESU kwa NENO ZURI la leo, Neno zuri BWANA la KUTUPONYA, la KUTUWEKA HURU, la KUTUPA UZIMA, AMANI na FURAHA yako BWANA YA KWELI, Asante BABA, Asante YESU... ''Maarifa ya ROHONI"   Jumapili kwetu ni Muhimu sana kwa Wana wa MUNGU, Wana Efatha,... kwani ni siku MUHIMU sana kwetu Kumsikiliza Mkalimani wetu Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akitupa Chakula cha Roho, Akitupa Maagizo Aliyopewa na BABA Yetu wa Mbinguni kwa ajili yetu sisi wana wa MUNGU,... Ni siku ya Kukaa chini miguuni mwa BABA na Akitupa Maneno ya HEKIMA na UFAHAMU kwetu,... Oooh Asante YESU, Asante BABA.

SIKU YA SABA YA KUSANYIKO L EFATHA 2013 (SIKU YA MWISHO Y KUSANYIKO)

Image
  UTUKUFU Wa MUNGU Wetu MKUU, Ulionekana katika KUMTUKUZA na KUMUIMBIA na KUMUABUDU na KUMPA SIFA Kwa Nyimbo zenye UTUKUFU... Oooh Asante YESU, Ilikuwa Amani na Raha tu kwa YESU.   Usiku wa Mkesha wa KUSANYIKO KUU LA BWANA MUNGU Wetu MKUU PEKEE 2013, Kibaha Precious Centre Mji wa BWANA, (Pichani Wanakwaya wa Mass Choir wakiwa Madhabahuni Wakimwimbia na Kumsifu na Kumtukuza na Kumuabudu na Kumchezea MUNGU WETU MKUU PEKEE, BABA YETU). Oooh Haleluya, USIKU wa Mkesha wa Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu MKUU umewadia, MUNGU Wetu na BABA Yetu ni MZURI Sana, Hatimaye BWANA Wetu YESU KRISTO Atakuwa nasi Usiku wa leo Akishiriki nasi Karamu ya Chakula cha BWANA (Mwili na Damu ya YESU KRISTO), BWANA Ametuandalia kupitia Mtumishi wake Mwaminifu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira,... Oooh Asante YESU, Asante BWANA, Asante BABA.     Mtumishi wa MUNGU Mwanamuziki wa Injili wa Nyimbo za Kuabudu na Kusifu toka Uingereza, alikuja na Mtumishi wa MUNGU Rev. Ola-Vi